Mbowe aachiwa huru na wenzake watatu baada ya DPP kuwasilisha hati ya kutotaka kuendelea na kesi

Lkn ktk polisi kusingizia rais lipo sana, na sasa hivi unawekwa ndani na wanakudai kikombozi kuachiwa, kupewa dhamana au kumpelekea mahakamani.
sawasawa lakini mengi yanatokea kwetu uraiani tunasingiziana sana hao wao kazi yao kupeleleza uongo alioufanya mtu kumsingizia mwenzie
 
Baba mchungaji Glenn kohoa na unywe maji kidogo 🤣🤣

Kwa hiyo mwanasiasa Mbowe ndiye alama ya kutupa hofu ya Mungu ?!!! 😳😳😳😳🤣🤣

#YetzerHatov
 
Sipendi Mbowe na wenzie waendelee kuwa mahabusu, lakini pia sipendi kusikia ameachiwa kwa MSAMAHA! Kama ni hivyo, basi kesi iendelee tuzijue mbivu na mbichi!

Na nina imani, kwa ushahidi uliotolewa, bila UJAJI WA MCHONGO, kulikuwa hakuna KESI hapo!
...na DPP hatimaye ameona hakuna Kesi hapo, ameifuta! Sio Msamaha...!
 
Mataga Vichaa kweli. Nimeona mitandaoni wameshaanza kumpongeza Mama. Wakati FAM anatengenezewa kesi walishangilia sasa ameachiwa nao wanashangilia
Hao ni Bendera fuata upepo,wanaumia ila hawana namna,wamepigwa na kitu kizito,huyo mama mwenyewe anafikiria atawaambia nini BBC maana alisema ushahidi upo eti na wengine walishahukumiwa[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Baba mchungaji Glenn kohoa na unywe maji kidogo [emoji1787][emoji1787]

Kwa hiyo mwanasiasa Mbowe ndiye alama ya kutupa hofu ya Mungu ?!!! [emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji1787][emoji1787]
Hapa sio Mbowe pekee, tunapaswa kuwa watu wa haki kwa watu wote siku zote.

Mimi nimewahi kumkemea Zitto akiwa Chadema na nikamwambia wazi kuwa wewe siku za usoni utakuja kuwa tatizo na mwiba.

Mimi hata mzazi akikosea namwambia ukweli.
Kuna watu wako ccm ni miongoni mwa viumbe bora kabisa...huwa nawapa credit zao.

Tujifunze kiwa waumini wa ukweli na hatutakuwa na cha kupoteza.
 
Points sana
 
Kwenye siasa hakuna uumini wa kweli baba mchungaji 🤣🤣

Kwangu CCM ndio imani ya juu baba mchungaji......

Ubarikiwe baba mchungaji ,amen🙏

#Siempre JMT🙏
 
Umshukuru mtu kwa kukutesa kipindi chote hicho kisa madaraka yake?
Amempotezea muda, gharama, amemsababishia mateso yeye na familia yake halafu leo wanafuta kesi kirahisi

I wish kungekuwa na namna ya kuwalipa fidia hawa watu
 
Danganyaneni....

Jidanganye....🤣🤣
Au umesahau mtoto wa Mbowe alisema Baba Yao hajamtuma mtu yeyote kumuombea msamaha na wao kama familia wanamsikiliza baba Yao ambaye anaamini hana hatia!

Ulipitiwa na Hilo? Ilikuwa wakati Zitto aliposimama na kumuombea msamaha Kwa Rais!
 
Ipo siku jamii itasimama dhidi ya uonezi wa dola. Mahakama iliwaona Wana kesi ya kujibu, dpp hana nia, watuhumiwa miezi kadhaa wameteseka na wengine ni vilema!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…