Mbowe aachiwa huru na wenzake watatu baada ya DPP kuwasilisha hati ya kutotaka kuendelea na kesi

Ahsante kwa kutuhabarisha Mkuu Nyendo.
Leo ni siku tuliyoisubiri kwa hamu mno,cha kustaajabisha hatuoni UpDates.Je,kuna kikwazo gani?Tunatarajia kupata Good News!
 



Mheshimiwa Jaji tunaomba Moja la Kufanya Mbele ya Mahakama yako Na Ombi hili Mheshimiwa Jaji ni kwamba Mkurugenzi Wa Mashitaka (DPP) kwa niaba ya Jamhuri anaomba Kuwasilisha Taarifa ya Kutokuwa na Nia na Kuendelea na Shauri hili
Na Taarifa hiyo tunaitoa Chini ya Kifungu cha 91(1) kwa Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai



 
MBOWE AACHIWA HURU BILA MASHARTI!

Kwa kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) amesema kuwa hana nia ya kuendelea na Kesi ya Mbowe na ameiomba Mahakama ifute Mashtaka yote dhidi ya Mbowe na wenzake watatu! Jaji Joachim Tiganga aliyekuwa anasikiliza Kesi hiyo ameatoa Uamuzi wa Kufuta Kesi na wshtakiwa wote wameachiwa huru!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…