Mbowe aachiwa huru na wenzake watatu baada ya DPP kuwasilisha hati ya kutotaka kuendelea na kesi

Mbowe aachiwa huru na wenzake watatu baada ya DPP kuwasilisha hati ya kutotaka kuendelea na kesi

Ndio shida ya kutumika!Aibu Kwa Jaji Kwa maamuzi aliyofanya wiki chache zilizopita!Watu wamebumba ushahidi wakaja kuuleta mahakamani,kila mtu akaona ni ushahidi wa mchongo na hakuna kesi!Jaji akasukumwa kuamua kuwa Wana kesi ya kujibu!Kabla hawajaanza kujitetea DPP anasema hana nia ya kuendelea na kesi maana ushahidi alionao ni crap!
Jaji unajisikiaje huko uliko?Ungeyajua haya,Bado uamuzi wako ungekuwa watuhumiwa Wana kesi ya kujibu?
 
Baada ya upande wa Mashtaka kufunga ushahidi wao na kuialika Mahakama kutoa hukumu ndogo na kisha mahakama kuwakuta watuhumiwa na kesi ya kujibu mnamo Februari 18 2022. Leo 04, Machi 2022 ni siku ya watuhumiwa kuanza kujitetea kutokana na tuhuma wanazotuhumiwa nazo.

Awali Mahakama iliwakuta na kesi ya kujibu katika mashtaka 5 kati ya 6 katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili.
Sijaipenda hii nilitaka kujua ukweli je ilikuwa kesi mchongo au kweli? Hata hivyo ilipofikia imeweza kutupa picha ukweli upi nadhani pande ile wangekuwa na uhakika na Jambo Lao sijui km wangekubali wito wa kufuta shitaka
 
image-removebg-preview.png
 
Ilikuwa ni suala la muda tu,

Tumeambiwa tutendee wengine tunayopenda kutendewa lakini binadamu tulishama huko hatuko.

Unajisikiaje kumtesa mtu kwa kipindi Cha karibia miezi Tisa gerezani kwa jambo la kutunga na Kila Leo ukute unahidhuria kanisani au msikitini....!

Wote Si wakamilifu lakini Kuna dhambi zingine tunazitenda kupunbavu mno.
 
Baada ya upande wa Mashtaka kufunga ushahidi wao na kuialika Mahakama kutoa hukumu ndogo na kisha mahakama kuwakuta watuhumiwa na kesi ya kujibu mnamo Februari 18 2022. Leo 04, Machi 2022 ni siku ya watuhumiwa kuanza kujitetea kutokana na tuhuma wanazotuhumiwa nazo.

Awali Mahakama iliwakuta na kesi ya kujibu katika mashtaka 5 kati ya 6 katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili.

Kujua kesi ilipoishia fungua kiunganishi hiki:Mbowe na Wenzake 3 wakutwa na kesi ya kujibu. Kesi imeahirishwa hadi Machi 04, 2022 watuhumiwa kuanza kujitetea

=========

UPDATES

Jaji anaingia Mahakamani Muda huu Saa 4 na Dakika 52

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Jamuhuri Dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Ikupendeze naitwa Robert Kidando Wakili wa Serikali Mwandamizi nipo na

Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Nassoro Katuga
Esther Martin
Ignasi Mwinuka
Mawakili Wa Serikali Waandamizi Tulimanywa Majige
Wakili wa Serikali

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na

Paul Kisabo
Sisty Aloyce
Gaston Garubindi
Iddi Msawanga
Evaresta Kisanga
Maria Mushi
Nashon Nkungu
John Mallya
Jeremiah Mtobesya
Fredrick Kihwelo
Dickson Matata Ni hayo tu mh Jaji.

Jaji: Shauri lilikuwa lina kuja kwa Utetezi, Je Mnazo habari zozote za Wateja wenu?

Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji ni kweli Kwamba Shauri lilikuwa limepangwa kwa ajili ya Utetezi Kwa Upande wangu tulifanya Maandalizi Mazuri Mimi John Malya, Dickson Matata, Fredrick Kihwelo na

Kibatala: wengine Juzi na Jana tulikuwa Ukonga na Segerea. Tulionana nao wakiwa na Bashasha kabisa, Kwamba Leo tunaendelea na Utetezi Lakini Leo Asubuhi tumepata Taarifa Kutoka Kwa Askari Magereza Kwamba Mbowe amepata Matatizo ya Ki Afya. Kwa hiyo hatuwezi Kuendelea,

Hivyo, Tunaweza Kupanga Kuendelea Jumatatu

Jaji: Jumatatu itakuwa Tarehe ngapi

Wakili Peter Kibatala: Tarehe 07 March 2022
Kesi ikifutwa na DPP lifunguliwe shauri la madai ya fidia ya kuchafuliwa jina Mh.Mbowe na wenzake pamoja na CDM kama chama.Maana hawa CCM wametangaza sana kesi hii kwa dunia.

Wakiachwa hivi hivi wataenda na hilo bango towards 2025 kama agenda yao,baadhi ya wananchi wenzetu wamenyimwa ufahamu wa haki za binadamu na hawapatiwi taarifa sahihi dhidi ya uonevu unaoendelea hapa nchini.
 
Nasikia Gaidi limelia weeeeeeeeee hadi limetoa mikamasi ndio likaonewa huruma.

Hongera sana mama, akirudia tena kuleta upumbavu wake asije kusema hajaambiwa.
 
Baada ya upande wa Mashtaka kufunga ushahidi wao na kuialika Mahakama kutoa hukumu ndogo na kisha mahakama kuwakuta watuhumiwa na kesi ya kujibu mnamo Februari 18 2022. Leo 04, Machi 2022 ni siku ya watuhumiwa kuanza kujitetea kutokana na tuhuma wanazotuhumiwa nazo.

Awali Mahakama iliwakuta na kesi ya kujibu katika mashtaka 5 kati ya 6 katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili.

Kujua kesi ilipoishia fungua kiunganishi hiki:Mbowe na Wenzake 3 wakutwa na kesi ya kujibu. Kesi imeahirishwa hadi Machi 04, 2022 watuhumiwa kuanza kujitetea

=========

UPDATES

Jaji anaingia Mahakamani Muda huu Saa 4 na Dakika 52

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Jamuhuri Dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Ikupendeze naitwa Robert Kidando Wakili wa Serikali Mwandamizi nipo na

Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Nassoro Katuga
Esther Martin
Ignasi Mwinuka
Mawakili Wa Serikali Waandamizi Tulimanywa Majige
Wakili wa Serikali

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na

Paul Kisabo
Sisty Aloyce
Gaston Garubindi
Iddi Msawanga
Evaresta Kisanga
Maria Mushi
Nashon Nkungu
John Mallya
Jeremiah Mtobesya
Fredrick Kihwelo
Dickson Matata Ni hayo tu mh Jaji.

Jaji: Shauri lilikuwa lina kuja kwa Utetezi, Je Mnazo habari zozote za Wateja wenu?

Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji ni kweli Kwamba Shauri lilikuwa limepangwa kwa ajili ya Utetezi Kwa Upande wangu tulifanya Maandalizi Mazuri Mimi John Malya, Dickson Matata, Fredrick Kihwelo na

Kibatala: wengine Juzi na Jana tulikuwa Ukonga na Segerea. Tulionana nao wakiwa na Bashasha kabisa, Kwamba Leo tunaendelea na Utetezi Lakini Leo Asubuhi tumepata Taarifa Kutoka Kwa Askari Magereza Kwamba Mbowe amepata Matatizo ya Ki Afya. Kwa hiyo hatuwezi Kuendelea,

Hivyo, Tunaweza Kupanga Kuendelea Jumatatu

Jaji: Jumatatu itakuwa Tarehe ngapi

Wakili Peter Kibatala: Tarehe 07 March 2022

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Utetezi, na tumewasikia Wenzetu Maombi Waliyo Wasilisha Sasa tusingependa Kujibu Hoja hiyo, Kwa sababu na sisi tuna Maombi Mengine Kwa hiyo Kujibu Hoja hiyo haitokuwa na Maana sana

Mheshimiwa Jaji tunaomba Moja la Kufanya Mbele ya Mahakama yako Na Ombi hili Mheshimiwa Jaji ni kwamba Mkurugenzi Wa Mashitaka (DPP) kwa niaba ya Jamhuri anaomba Kuwasilisha Taarifa ya Kutokuwa na Nia na Kuendelea na Shauri hili

Na Taarifa hiyo tunaitoa Chini ya Kifungu cha 91(1) kwa Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai

Jeremiah Mtobesya: Tumesikia Taarifa ya Notes hiyo kutoka kwa Mkurugenzi Wa Mashtaka, na Kwa Bahati Mbaya hatuwezi Kusema lolote zaidi ya Kusema tunaichia Mahakama, sababu Kifungu Kinatoa Maelezo Yote Kwamba Baada ya Kusema hivyo tunaichia Mahakama dhidi ya Amri zake za Mwisho

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Taarifa Hii tunaiwasilisha kwa Njia ya Maandishi, Kwa Maombi hayo ya Kifungu cha 91(1) tunaomba Kuondoa Mashitaka Yote dhidi ya Washitakiwa Wote Sababu zote zipo katika Noel Prosecui ambayo tumeiwasilisha

Wakili wa Serikali Robert Kidando: anapeleka Nyaraka Mbele ya Karani wa Jaji, na Karani anampatia Jaji

Jaji: Je umezungumza kwa niaba ya Defense Wote..?

Jeremiah Mtobesya: Mheshimiwa Jaji naomba kila Mmoja aseme

John Malya: Mheshimiwa Jaji notes iliyotolewa inayushuka Mikono wote, pamoja na Kujiandaa kwa ajili ya Kujitetea, Mikono yetu imefungwa na hatuwezi Kusema lolote, Tulitaka sana Warudishe Gharama zetu na Mengine lakini wacha Tusubiri Maamuzi ya Mahakama

Fredrick Kihwelo: Kwa niaba ya Mshtakiwa wa tatu Tumesikia Taarifa iliyotolewa, Tunaichia Mahakama iweze Kutoa Amri

Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Na sisi tunaichia Mahakama, Sheria inajielezea wazi.. Mahakama ipo Kimya Kidogo na Jaji Bado anaandika

Kule Nje ni Kelele za Shangwe na Fifijo watu Wanaimba, Imebidi Mahakama Kufunga Vioo Vya Madirisha ili Kuzuia Kelele Kuingia Mahakamani, Wewe furaha yako ni Kiwango gani? Onyesha emoji ya furaha hapa Chini.. Au picha yako ukiwa na furaha kubwa..

Jaji: Baada ya Mahakama Kusikiliza Hoja iliyoletwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali Kwamba Mkurugenzi wa Mashtaka hana nia ya Kuendelea na Kesi, na Upande wa Pili wakaridhia

Mahakama inasema Shauri hili lililo kuwa linawakabili Washitakiwa Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa nakiondosha Mahakamani na Washitakiwa Wanaachiwa huru bila Masharti, sababu Kuna Vielelezo vililetwa Mahakamani, naandaa Amri ya Kuviachia

Jaji: Na hivyo naelekeza Mkuu wa Magereza Kuwaachiwa Mara Moja, Leo na si Vinginevyo Natoa Amri Jaji anatoka Mahakamani Mahakama inaridima Kwa Shangwe.

=======

Freeman Aikael Mbowe na wenzake watatu, wameaachiwa huru leo, na Mahakama kuu Divisheni ya makosa ya uhujumu uchumi na Rushwa, Baada ya DPP Kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri hilo, leo 4.3.2022. Hivyo, Freeman Aikaeli Mbowe
Safi sn MUNGU wa mbinguni ametenda maajabu sn
 
Back
Top Bottom