Mbowe ahusishwa na UFISADI wa kuimaliza NSSF

Mbowe ahusishwa na UFISADI wa kuimaliza NSSF

Kada,

usianze kutangaza ushindi bubu kwa kuwa unajua kuwa ninakuwa off kila weekend kuachia vidali po uwanja wajisikie kidogo. Nitarudi jumanne (GOD'S willing) kufanya kile nifanyacho best hapa... kuwapa hell mafisadi wanaouza nchi kwa wakoloni kwa msaada wa JM Kikwete!

Karibu Dallas.... halali mtu mpaka Easter Monday!

Kuwa na Easter na Maulidi njema!

Thanks!

Ukishindwa sema tu usikimbie kijanja, nani anataka kujua kuwa utakuwa Dallas.
Mnavamia mambo msiyajua vikishushwa vitu mnakimbia.
 
Mwanakijiji halijui hili. kwa vile haijui siasa wala nchi haijui.Chadema inatumuika kama NGO nyingine kuchukua pesa ulaya kwa ajili ya maslahi binafsi.

kuna watu wamefungua NGO za kusaidia yatima, wajane au wagonjwa wa ukimwi in Theory,lakini practically hawafanyi chochote.

vilipoanza vyama vingi mzee Mtei alikuwa hana kazi analima shamba lake kule Arusha.

akaamua kuanzisha Chama ili aishi kwa ruzuku. Wachagga wengi walishtukia deal hii ya vyama vya siasa. wengi wao walikuwa na nia ya kujikombia kimaisha. Wachagga wafutao walianzisha vyama.

1-James Mbatia baada ya kufukuzwa chuo kikuu akaenda NCCR kama ajira yake huyu ni mchagga.

2-ULOTU huyu ni mchagga alianzisha chama cha NRA kama mradi wake.

3-MZEE MTEI na Mkwe wake Freeman Mbowe na mtoto wa mtei Liliani Mtei ambaye ni mke wa Mbowe walianzisha chama cha Chadema baada ya Mbowe kuwa jobless na mzee Mtei kuwa mkulima arusha.

4-Professor Shayo huyu nae mchagga alianzisha chama kama mradi wake binafsi.
5-Anna senkoro(mchagga) nae alianzisha chama kama mradi wa kumfanya aishi.

6-Mrema na Ngawaiya nao wakaingia TLP kama mradi wao wa maisha ni wachagga.

kulikuwa na Mvungi nae anatoka kilimanjaro kwenye biashara ya Vyama vya siasa kama miradi.

Mwanakijiji anajua kuwa Mbowe analamba Conservative Party YA UK?
6-

Hivi wachaga wa CCM walioanzisha na sasa waliomo TRA, BOT, Hazina nao ni dili zao binafsi?

Na wachaga wa CCM kama wakina Mramba nao je, tusemeje?

Hivi wachaga wako upinzani pekee? Ama wachagga wameasisi vyama vya upinzani pekee? Hakuna kitu kingine ambacho kimeasisiwa na wachaga?

Chinga katika hili natofautiana na wewe kabisa, acha kupandikiza mbegu ya ukabila.

Kwa hiyo Chinga Mkapa alipokuwa Rais tuseme CCM ni chama cha machinga?

PM
 
KWANI INJIA WA EPA SI MRAMBA NA MAMA MKAPA, wewe hujui Kitilya na Mramba walikuwa na deals za kuwakamua wafanya biashara na kuifanya TRA ni MALI ya Kilimanjaro? nenda kwenye thread ya ukabila TRA.
 
Hivi wachaga wa CCM walioanzisha na sasa waliomo TRA, BOT, Hazina nao ni dili zao binafsi?

Na wachaga wa CCM kama wakina Mramba nao je, tusemeje?

Hivi wachaga wako upinzani pekee? Ama wachagga wameasisi vyama vya upinzani pekee? Hakuna kitu kingine ambacho kimeasisiwa na wachaga?

Chinga katika hili natofautiana na wewe kabisa, acha kupandikiza mbegu ya ukabila.

Kwa hiyo Chinga Mkapa alipokuwa Rais tuseme CCM ni chama cha machinga?

PM

sidhani kama ulielewa point ya chinga ! alisema "sababu ya uanzilishi wa hivyo vyama" na sio uwepo wa hao watu katika vyama ambavyo vipo established already !
 
chadema ni chagga party why??sina details za kutosha ila kama kuna mtu ambaye atakuwa ameisoma hii taarifa atakubali.
kuna kipindi chadema walifanya maandamano Dr Peter Mziray wa PPT-MAENDELEO aliwaomba aungane nao wakamtosa sasa sijui mziray ni kabila gani ila walimtosa hata kwenye helkopta yao ya wachagga..
 
Hii ni makala ya Padri Karugendo inayopatikana hapa: http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/3/23/makala6.php
NI vizuri kwamba Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amejitokeza na kuelezea kwa ufasaha tuhuma zinazolenga kumtupa kwenye kapu la mafisadi.
Asingejitokeza, tungemshangaa kama tunavyowashangaa wanaonyoshewa vidole wakakaa kimya. Waraka wa Mbowe, aliousambaza kwenye vyombo vya habari unajitosheleza.
Walio wengi tumeelewa na kukubali kwamba yeye si fisadi na wala si mwizi, bali alikopa fedha NSSF, kitu ambacho ni cha kawaida. Hata kabla hajajieleza tulishabaini kwamba hizi ni njama za ‘wajinga’ wachache.
Tunafahamu kwamba hizi ni njama za watu wanaotumiwa kuchafua majina ya watu kwa malipo ya vijisenti vichache. Tunafahamu kwamba hizi ni njama za watu wasioheshimu taaluma zao za uandishi wa habari.
Tulishuhudia uhuni huu wakati wa kumchagua mgombea wa urais kupitia CCM. Baadhi ya wagombea walichafuliwa na kupakwa matope.
Tunawafahamu waandishi hawa wanaoandika kwa kuweka chumvi kila habari. Ni wale walioandika kwamba Edward Lowassa, alipokewa kwa magari 400 kule Arusha, wakati alipokewa kwa magari 80.
Ni aina ya waandishi walioshindwa kuandika chochote juu ya maandamano ya vijana ya kulaani vitendo vya Richmond, yaliyofanyika siku ile Lowassa alipopokewa kishujaa nyumbani kwao.
Ndio hao hao wanaosema Mbowe, anadaiwa sh milioni 1,200, wakati yeye alikopa sh milioni 15 na amelipa zaidi ya asilimia 75. Wanaandika bila utafiti, wanaandika bila kutafakari, wanaandika ili walipwe!
Kwao pesa ndizo zinabainisha uongo na ukweli. Hawa ni aina ya waandishi wasiotambua maana ya mkopo na wizi?
Mbowe alikopa NSSF, mafisadi waliiba BoT! Ina maana hawaoni tofauti?
Ni makusudi! Ni kutaka kuandika ili walipwe! Hawa ni waandishi wa hatari.
Mauaji ya kimbali nchini Rwanda, yalichochewa kwa kiasi kikubwa na waandishi wa namna hii. Ni jambo la muhimu na la haraka kwa Watanzania kuwakataa waandishi hawa hatari.
Tuyasusie magazeti yao, maana wana nia mbaya ya kutupotosha, wana nia mbaya ya kutaka kuuficha ukweli na kuutukuza uongo. Wanachuja mbu na kummeza Ngamia!
Mbowe, aligombea urais wa taifa letu Mwaka 2005. Kampeni zilikuwa nzito, alipasua anga kwa anga na kuwa tishio kwa wale waliokuwa wakipiga kampeni nyumba kwa nyumba wakigawa vitenge na chumvi.
Kama shutuma hizi anazobambikiwa leo zingekuwa na maana yoyote, basi zingejitokeza wakati wa uchaguzi mkuu.
Mbona hakuna hata chombo cha habari kilichosema juu ya deni la NSSF wakati huo? Deni hili si la leo na wala si la 2005 ni la zamani kabisa. Mbona halikujitokeza wakati ule na badala yale linakuja kujitokeza leo wakati wapinzani wakiwa katika jukwaa wakifichua wizi mkubwa unaoendelea katika taifa letu?
Mbona linajitokeza leo baada ya Mbowe kujitokeza kwa nguvu kupinga ufisadi?
Kusema kwamba mkopo wa Mbowe unaifilisi NSSF ni kichekesho. Hata aliyeandika haya kama ni msomi, mtu makini, anayefanya utafiti na kuchambua masuala mbalimbali katika jamii yetu ni lazima ajicheke mwenyewe na kujidharau.
Kila siku tunayaona mambo makubwa ya NSSF, hawa wanajenga majumba makubwa kila sehemu ya Tanzania, kama wamefilisiwa na Mbowe wasingekuwa wanafanya chochote kile.
Hata hivyo kutokana na maelezo ya Mbowe, deni analodaiwa limelipwa zaidi ya nusu. Kama si utata uliojitokeza NSSF angekuwa amemaliza kulilipa.
Kuna watu wa kusemwa juu ya NSSF na wala si Mbowe. Kuna tunaowafahamu ambao walinunua nyumba za NSSF kwa bei ya chini na baadaye kuziuza kwa bei ya juu.
Walijua kabisa kwamba wanazinunua nyumba hizo kwa bei ya chini. Walifanya hivyo kwa kushirikiana na NSSF kwa lengo la kupata chochote kama ulivyo utamaduni wetu Watanzania wa kuiuza nchi yetu kwa vijisenti vichache.
Ni kama ilivyo mikataba yote ya taifa hili, mikataba mibovu yenye lengo la kuwanufaisha wageni na kuwakandamiza wananchi. NSSF ina kashifa zake na ufisadi mwingi, deni la Mbowe ni tone dogo kwenye bahari kubwa!
Mbali na vyombo vya habari, kuna baadhi ya vyama vya upinzani vinamshambulia Mbowe. Mwenyekiti wa SAU, anatoa ujumbe wa wazi kwamba yeye ni kibaraka wa CCM, amekuwa akifanya hivyo siku zote.
Watanzania wanafahamu, wala hana haja ya kujificha nyuma ya wapinzani. Huyu hatusumbui hata kidogo. Ni Watanzania wachache sana wanaoweza kumsikiliza na kuamini kile anachokisema.
Nimekuwa nikimheshimu sana mchungaji Mtikila. Huyu akisema watu wanasikia. Lakini nimemshangaa jinsi alivyochanganya mambo. Badala ya kumaliza upande mmoja ambao uko wazi kabisa, upande wenye ushahidi usiopingika wa ufisadi, anamgeukia Mbowe.
Inawezekana kapitiwa, maana mtu makini kama alivyo Mchungaji Mtikila, si wa kutoona tofauti kati ya mkopo na wizi. Mbowe, alikopa na hakatai kulipa. Mafisadi wameiba na bado wanajificha, eti wanarudisha fedha walizoziiba kimyakimya.
Walio wengi wameiba na kuwekeza nje ya nchi. Mbowe, amekopa na kuwekeza hapa hapa, ametengeneza ajira kwa vijana wetu, analipa kodi, ni kati ya wafanyabiashara wanaolipa kodi kwa muda na kwa uaminifu na kutoa mchango katika ujenzi wa taifa. Haiwezekani kwamba mchungaji Mtikila halioni hili!
Sitaki kuamini kwamba hizi ni propaganda za CCM, maana chama kikongwe kama CCM, hakiwezi kufanya propaganda za ‘kijinga’ kama hizi. Mwana CCM aliye makini ni lazima afanye jitihada za ziada kukisafisha chama chake badala ya kutaka kufunika madhambi makubwa yaliyofanywa na wana CCM na maswahiba wake.
Mbinu za kutumia vyombo vya habari ili Watanzania wafumbe macho juu ya Richmond, EPA na mengine ni mbinu zilizopitwa na wakati.
Kama ufisadi uliojitokeza katika taifa letu ungekuwa ni wa mtu mmoja ama wawili, basi wapambe wangeweza kuufunika kwa kumpakazia Mbowe. Bahati mbaya ufisadi huu ni mkubwa sana. Ni ufisadi wa kutisha, ni ufisadi unaofunga wimbo wa ‘nchi yetu ni masikini.’
Ni ufisadi unaowaingiza watu wengi, viongozi wengi, makampuni mengi, chama tawala, Serikali na watu wengi kutoka nje ya nchi.
Ufisadi huu umeamsha hasira za wananchi. Watu wamegundua kwamba wakati viongozi wetu wanatulisha kasumba kwamba nchi yetu ni maskini, na kutulazimisha kuuimba wimbo huu usiokuwa na mwisho, wao walikuwa wakiogelea kwenye utajiri wa kutisha.
Wamekuwa wakitumia pesa za taifa letu kujitajirisha wao, familia zao na marafiki zao.
Wakati viongozi wetu wakituhimiza kujenga sekondari za kata, watoto wao si kwamba wanasoma nje ya nchi bali wanaishi maisha ya peponi, baadhi yao wamekuwa wakiruka kutoka London kwenda Cape Town – Afrika Kusini kwenye sherehe za ‘Birthday’, wengine wanaendesha magari ambayo hata Wazungu hawataweza kuyaendesha.
Je, kumpakazia Mbowe, kutatoa ukweli kwamba Rostam Aziz, si Mtanzania asilia? Kwamba hakuzaliwa hapa na wala hajawahi kuomba uraia? Itaondoa ukweli kwamba mbali ya kuwa mbunge, kinyume cha sheria ameshika nafasi nyeti kwenye chama tawala?
Kwamba amekuwa akikingiwa kifua na viongozi wa juu serikalini? Serikali yetu imekuwa na msimamo mkali juu ya wahamiaji haramu kiasi cha kuwafukuza hata Watanzania wenye asili ya Rwanda na Burundi, Watanzania wenye vyeti vya uraia vinavyotambuliwa na serikali, lakini serikali hiyo hiyo inawafumbia macho wageni wanaohujumu uchumi wetu!
Mbowe hakuchota pesa kutoka NSSF, hakuiba kutoka NSSF, alikopa. Hili ni jambo la kawaida. Mafisadi wa EPA, hawakukopa, waliiba! Hawa niwezi! Wanaopitisha mikataba mibovu kwa kupokea chochote ni wezi, wanapokea rushwa. Huwezi kuwaweka hawa kapu moja na Mbowe.
IGP Mwema amewafananisha mafisadi na magaidi, amesema hawakamatiki. Hawa huwezi kuwalinganisha na Mbowe. Vinginevyo ni kumdhalilisha na kumkosea haki.
Hata kama kuna njama za kumhujumu Mbowe na wapinzani, njama hizi zimefanyika ‘kijinga’. Ni bora hawa wanaoandaa njama hizi wakatambua kwamba Tanzania ya jana na juzi si sawa na ya leo.
Watu wameanza kufumbua macho, watu wameanza kuhoji. Watu wana uwezo wa kuchambua fisadi na asiye fisadi. Leo hii watu wana uwezo wa kuchambua uongo na ukweli.
Mbowe, umesema tumekusikia, tumekuelewa na kukuamini.
Usitetereke! Endeleza mapambano hadi kieleweke!
Nipigie: +255 754 633122
 
Padri Uchwara, hana tofauti na waandishi uchwara wanaotumika kuwasafisha wanasiasa.

Kama padri inatakiwa akemee uozo wa aina yoyote ile, bila kujali ni mdogo au mkubwa.

Lakini kama tulivyoona miaka na miaka, dini na hasa kanisa la kikatoliki linakuwa upande wa wanasiasa kwa sehemu kubwa ya muda wa uhai wake.

Sasa huyo padri si angetuambia ni watu wake wangapi wa kanisa wamewahi kukopa NSSF. Kwanini kukopa NSSF kuwe kwa vigogo na wanasiasa tu?

Anaongelea viongozi wa CCM kuua shule huku wao wanapeleka watoto nje, hiyo ina tofauti gani na viongozi wetu wa kisiasa wao kukopa kule kuliko nafuu kama NSSF na kutuacha wananchi wengine tunahangaika na kero ya mabanki ya binafsi?

Huyu padri wetu alikuwa wapi wakati Sumaye anaulaumiwa kwa kukopa NSSF? Kwanini kama ana principles na ni consistency hakuwa tayari kumtetea Sumaye hata kama hampendi. Principles zinakuwa imara pale unapokuwa tayari kuzitumia ili kumwokoa adui yako.

Hata kama Mbowe angelipa on time, bado kukopa NSSF ni issue. Alipoona anaingia siasa ilitakiwa ajiangalie kwanza na kurekebisha makosa yake yote ya nyuma ikiwa ni pamoja na kulipa hilo deni.

CHADEMA inatakiwa muache kutetea uozo kwasababu eti ni mdogo kuliko uozo wa CCM. Hapa kipimo sio CCM, kipimo ni maadili mema ambayo tungetaka viongozi wetu wayafuate. Maadili hayo yasipofuatwa basi tuwe tayari kukemea bila kujali mhusika ni nani. CHADEMA inabidi mumshauri Mbowe akae mara moja na NSSF through a third party na kupata ufumbuzi wa suala lake. Hapa suala sio la kiuchumi tena bali limegeuka kuwa la kisiasa na yeye kama mwanasiasa inabidi aelewe hivyo.

Haimsaidii kitu kutuma wafuasi wake kumtetea kwenye vyombo vya habari au hapa JF. Njia pekee ya maana ni kupata ufumbuzi wa hilo suala pamoja na mengine yote ya aina hiyo.
 
Naona sasa ni wakati walau wa kuuliza swali juu ya kosa la Mbowe nini?

Ni kukopa NSSF ama kosa lake ni kukataa kulipa riba kubwa kuliko anavyotakiwa kulipa?

Kwani yeye ni mwanachama wa NSSF na kwa kawaida wanachama wa NSSF wanaweza kukopa sasa kosa la Mbowe nini ? nashindwa kuelewa dhambi yake kwa kweli labda kama naweza kuelimishwa ndipo naweza kuelewa.

Huyu Mbowe hadaiwi deni la msingi kwani kama ameshalipa 75 milioni maana yake ni kuwa tayari deni lake la msingi kamaliza na sasa anadaiwa riba .

Naomba kujua kosa la Mbowe ili niweze kuelewa nini kinazungumzwa hapa , nawatakia pasaka njema wakristo na waislamu muendelezo wa maulid mwema.
 
PM,

Ukitaka kujua kosa la Mbowe ni lipi, labda unisaidie kujibu, kosa la Sumaye lilikuwa lipi?

Hili la kusema alishalipa deni la msingi sijui linatoka wapi. Ukikopa, unapolipa, unalipa riba ya huo mwaka pamoja na sehemu ndogo ya deni la msingi. Deni la msingi linaendelea kulipwa mpaka siku ya mwisho.

Kusema alishalipa lipa deni la msingi na sasa riba ndio ina utata, nafirkiri kupotosha wasomaji.

Deni la msingi linalipwa mpaka siku ya mwisho. Kama kweli Mbowe anadaiwa basi anadaiwa sehemu ya deni la msingi pamoja na riba na wala sio riba tu kama baadhi ya watu wanavyotaka kutudanganya hapa.
 
Tunatakiwa Tumpongeze Mbowe Kwa Jitihada Zake Binafsi Za Kuja Mbele Ya Jamii Na Kueleza Kile Anachojuwa Yeye Na Yote Yaliyofanyika Naamini Alichosema Mbowe Ni Ukweli Hakubahatisha Wala Kudanganya

Kama Kungekuwa Kuna Uwongo Wowote Basi Huko Alipokopa Naamini Kuna Watu Wangekuja Juu Kurekebisha Kauli Za Mbowe Au Hata Wapinzani Wake Wangekuja Na Masuala Mapya Kuhusu Tuhuma Hizo

Na Hii Ndio Democrasia Tunayoitaka Ambapo Mtu Bila Kujali Dini , Kabila Wala Chama Anachotoka Anapotakiwa Kujieleza Mbele Ya Jamii Au Kutoa Ripoti Yoyote Basi Huwa Tayari Kuja Mbele Na Kusema Ukweli

Basi Kama Kuna Suala Lolote Tata Ni Kazi Ya Waandishi Wa Habari Kuchunguza Na Kutuletea Habari Zaidi Kuhusu Tukio Hili Lakini Kama Hamna Cha Kuchunguzwa Basi Tumpongeze Mbowe Kwa Kuchukuwa Uamuzi Wa Busara Wa Kutuambia Ukweli .

Naamini Hili Litakuwa Ni Funzo Kwa Wengine Wote Nao Wawe Na Utamaduni Wa Kuongea Navyombo Vya Habari Kunapotokea Habari Zozote Zinazowahusu

Kwa Njia Hii Siku Moja Tutafika Kule Tunapotaka Kwenda Katika Dunia Ya Ukweli , Uwazi , Uadilifu Na Maadili Mema

Ahsante
 
PM,

Ukitaka kujua kosa la Mbowe ni lipi, labda unisaidie kujibu, kosa la Sumaye lilikuwa lipi?

Hili la kusema alishalipa deni la msingi sijui linatoka wapi. Ukikopa, unapolipa, unalipa riba ya huo mwaka pamoja na sehemu ndogo ya deni la msingi. Deni la msingi linaendelea kulipwa mpaka siku ya mwisho.

Kusema alishalipa lipa deni la msingi na sasa riba ndio ina utata, nafirkiri kupotosha wasomaji.

Deni la msingi linalipwa mpaka siku ya mwisho. Kama kweli Mbowe anadaiwa basi anadaiwa sehemu ya deni la msingi pamoja na riba na wala sio riba tu kama baadhi ya watu wanavyotaka kutudanganya hapa.

Mtanzania inaelekea unafahamu vizuri sana deni la mbowe, hebu niambie ndugu yangu Mbowe anadaiwa shilingi ngapi?. sitaki jibu la kubahatisha, nipe jibu lililo sawia kabisa.

isije ikawa na wewe unaimba wimbo ule ule wa kufuata mkumbo wa "mbowe anadaiwa, mbowe anadaiwa" lakini hujui anadaiwa shilingi ngapi.

kwa mtindo wa namna hii wa kuimba nyimbo za watu wenye ajenda ya siri ndo watu mnaoamini leo kwamba mbowe kakopa shilingi milioni 15 na kwa sasa anadiwa shilingi milioni 1200,hiyo peke yake si tu kwamba haiwezekani hata kama angekuwa hajalipa senti hata moja,lakini mnasahau pia kwamba huyu mtu keshalipa pesa kadhaa na sasa kuna kesi iko mahakamani ambako ni vigumu kwa sasa kumhukumu, umejuaje pengine akashinda kesi?

nauliza tena kosa la mbowe ni nini?, mtamhukumu vipi kosa wakati mahakama haijamhukumu kosa?. kama anadaiwa anadaiwa shilingi ngapi?
 
Naona sasa ni wakati walau wa kuuliza swali juu ya kosa la Mbowe nini?

KUNA WATU WANAFIKIRI UKIWA KIONGOZI HUTAKIWI KUKOPA KUTOKANA NA UTAMADUNI WA WENGI WANAOKOPA KUTORUDISHA DENI HILO AU KUTOMALIZA NA SHERIKA AU BENKI KUINGIZA HASARA

Ni kukopa NSSF ama kosa lake ni kukataa kulipa riba kubwa kuliko anavyotakiwa kulipa?

NAAMINI WATAKUWA NA MIKATABA YAO KATIKA HUO MKOPO SASA TUSIANGALIE UPANDE MMOJA WA SHILINGI JE TUMEPATA TAARIFA ZOZOTE ZA NSSF KUJUA KOSA NI LA NANI HAPO TULINGANISHE ?

Kwani yeye ni mwanachama wa NSSF na kwa kawaida wanachama wa NSSF wanaweza kukopa sasa kosa la Mbowe nini ? nashindwa kuelewa dhambi yake kwa kweli labda kama naweza kuelimishwa ndipo naweza kuelewa.

DHAMBI YAKE NI YEYE KUWA MWENYEKITI WA CHAMA CHA UPINZANI NDIO KOSA LAKE UKIWA MPINZANI WATU HUTAFUTA VITU KAMA HIVYO KUJIPA SIFA ZA ZIADA KATIKA SIASA ZAO

Huyu Mbowe hadaiwi deni la msingi kwani kama ameshalipa 75 milioni maana yake ni kuwa tayari deni lake la msingi kamaliza na sasa anadaiwa riba .

Naomba kujua kosa la Mbowe ili niweze kuelewa nini kinazungumzwa hapa , nawatakia pasaka njema wakristo na waislamu muendelezo wa maulid mwema.

NAONA SIKUHIZI KATIKA FORUM WATU WANAPOTEZA MABOYA MADA ZA WENGINE KWA MAKUSUDI AU KWA MASILAHI YAO BINAFSI
 
Mtanzania ,umeniuliza kosa la Sumaye lilikuwa nini naamini unayajua majibu ila hutaki kusema kuwa unajua nami nakupa jibu la swali lako.

Kosa la Sumaye ni kuwa alikopa NSSF kwa kutumia cheo chake kwani hakufuata taratibu za kisheria ila aliagiza na kupewa mkopo.

Kosa la pili la Sumaye ni kuwa yeye hakuwa mwanachama wa NSSF na ni kinyume cha utaratibu kumkopesha mtu ambaye sio mwanachama , Mbowe ni mwanachama na ana haki ya kukopa .

Sasa nami nakuuliza kosa la Mbowe nini?
 
NDIYO. Mbowe ni Mwanachama wa NSSF, na ana haki ya KUKOPA. Kama NSSF wanamwongezea riba asiyokubaliana nayo alipe tu kwa kuwa ni mwanasiasa?

Fungueni macho, mjue kuwa hili la Mbowe kudaiwa NSSF limesukumwa na Rostam Azizi na Lowassa wakimtumia balile kupitia Rai...ili kuzima hoja ya ufisadi wa EPA na Richmond. Hadanganywi mtu hapa...Mbowe amekopa, na amelipa...bado kumalizia deni. Hata kwa mtoto mdogo njama hizi mbona zinaeleweka tu?
 
Sumaye hakuwa mwanachama, why? Wakati alikuwa mfanyakazi wa serikali kwa muda mrefu kabla ya kuwa mwanasiasa? Pia alikuwa kwenye shirika la umma kabla ya kuwa mwanasiasa. Ni nani huyo aliyesema Sumaye hakufuata sheria?

NSSF walisema amekopa kwa kufuata sheria.

Kwa mimi wote wawili wana makosa yanayofanana, kosa la wanasiasa na matajiri
kukopa kule ambako mwananchi wa kawaida hawezi kukopa. Niambie Machinga gani ambaye ni mwanachama wa NSSF amewahi hata kukopa laki moja huko NSSF?

Kosa la pili la Mbowe ni kushindwa kulipa deni lake kwa muda waliokubaliana mpaka kuanza kuburuzwa mahakamani.

Yeye mwenyewe amedai anadaiwa na NSSF ila anapinga kwamba sio hizo 1.2 bilion. Sasa si alipe anazodaiwa? Kweli deni la miaka 6 linachukua miaka 18, watu hamuoni kosa hapo?

Kosa la tatu ni kwamba NSSF ni mfuko wa Watanzania wa kawaida, wengi wao wakiwa maskini. Failure yoyote ya hiyo NSSF kukusanya madeni, madhara yake ni kwa wananchi wa kipato cha chini. Mbowe kushindwa kulipa hizo pesa, anaongeza taabu hizo wanazopata wanachama wa NSSF

Kosa la nne ni kwamba Mbowe ni mwanasiasa, sio tu kwamba anakuwa judged kiuchumi lakini anakuwa judged pia kisiasa. Kama mwanasiasa, kwa maoni yangu hakutakiwa kukopa NSSF.

Unataka sababu zingine?
 
Kichwamaji

Unaushahidi Wowote Wa Kuonyesha Kwamba Hili Suala Linasukumwa Na Lowasa Na Mwenzake Rostam ?

Kama Unao Basi Uweke Hadharani

Mimi Nakumbuka Sikuile Mbowe Anaongea Na Vyombo Vya Habari Lowasa Alikutana Na Rostam Pale Uwanja Wa Ndege , Watu Wengi Waliondolewa Katika Vip Wakabakia Wao Tu Wakaongea Kwa Dakika 30 Hivi Kisha Lowasa Akapanda Mchuma Akaishia Sijui Waliongelea Nini

Inawezekana Ni Tukio Hili
 
NDIYO. Mbowe ni Mwanachama wa NSSF, na ana haki ya KUKOPA. Kama NSSF wanamwongezea riba asiyokubaliana nayo alipe tu kwa kuwa ni mwanasiasa?

Fungueni macho, mjue kuwa hili la Mbowe kudaiwa NSSF limesukumwa na Rostam Azizi na Lowassa wakimtumia balile kupitia Rai...ili kuzima hoja ya ufisadi wa EPA na Richmond. Hadanganywi mtu hapa...Mbowe amekopa, na amelipa...bado kumalizia deni. Hata kwa mtoto mdogo njama hizi mbona zinaeleweka tu?

Kichwamaji,

Watanzania sio wajinga, suala la Mbowe haliwezi kuzima watu kujadili EPA.

Tanzania ina mambo mengi ambayo hayaendi sawa. Lazima tupigane nayo yote sambamba. Hii dhana ya kwamba eti watu waconcentrate na dhambi kubwa, ni nosense, dhambi kubwa hutokana na dhambi dogo.

Wengine kuna kitu tunachoamini in life, kama jambo ni kosa lako, hata siku moja usimlaumu anayekuumbua. Yeye Mbowe alitegemea nini? Alitegemea akina RA wawe wanamwimbia nyimbo za sifa? Ni akina RA waliompeleka Mbowe kukopa NSSF? Je ni akina RA ambao walimfanya asimalize kulipa deni kwa miaka 18?
 
Padri Uchwara, hana tofauti na waandishi uchwara wanaotumika kuwasafisha wanasiasa.

Kama padri inatakiwa akemee uozo wa aina yoyote ile, bila kujali ni mdogo au mkubwa.

Lakini kama tulivyoona miaka na miaka, dini na hasa kanisa la kikatoliki linakuwa upande wa wanasiasa kwa sehemu kubwa ya muda wa uhai wake.

Sasa huyo padri si angetuambia ni watu wake wangapi wa kanisa wamewahi kukopa NSSF. Kwanini kukopa NSSF kuwe kwa vigogo na wanasiasa tu?

Anaongelea viongozi wa CCM kuua shule huku wao wanapeleka watoto nje, hiyo ina tofauti gani na viongozi wetu wa kisiasa wao kukopa kule kuliko nafuu kama NSSF na kutuacha wananchi wengine tunahangaika na kero ya mabanki ya binafsi?

Huyu padri wetu alikuwa wapi wakati Sumaye anaulaumiwa kwa kukopa NSSF? Kwanini kama ana principles na ni consistency hakuwa tayari kumtetea Sumaye hata kama hampendi. Principles zinakuwa imara pale unapokuwa tayari kuzitumia ili kumwokoa adui yako.

Hata kama Mbowe angelipa on time, bado kukopa NSSF ni issue. Alipoona anaingia siasa ilitakiwa ajiangalie kwanza na kurekebisha makosa yake yote ya nyuma ikiwa ni pamoja na kulipa hilo deni.

CHADEMA inatakiwa muache kutetea uozo kwasababu eti ni mdogo kuliko uozo wa CCM. Hapa kipimo sio CCM, kipimo ni maadili mema ambayo tungetaka viongozi wetu wayafuate. Maadili hayo yasipofuatwa basi tuwe tayari kukemea bila kujali mhusika ni nani. CHADEMA inabidi mumshauri Mbowe akae mara moja na NSSF through a third party na kupata ufumbuzi wa suala lake. Hapa suala sio la kiuchumi tena bali limegeuka kuwa la kisiasa na yeye kama mwanasiasa inabidi aelewe hivyo.

Haimsaidii kitu kutuma wafuasi wake kumtetea kwenye vyombo vya habari au hapa JF. Njia pekee ya maana ni kupata ufumbuzi wa hilo suala pamoja na mengine yote ya aina hiyo.

Mtanzania hapa HUNA HOJA KABISA, umedhalilisha akili yako mwenyewe.

Ukimsoma vizuri Karugendo utaonakwamba amefanya utafiti wa kutosha, kwani anajua hata NANI aliandika nini wakati gani, na ameshiriki vipi katika saga hili la Mbowe. Anajua nani anamtumia nani...Wewe umeingiza jaziba zako na mapenzi yako kwa mafisadi.

Kama huoni kwamba katika hili Padri Karugendo hakemei ufisadi, basi hujui kutafsiri unachokisoma. Hebu msome tena ujue anakeme nini. Hata huoni kwamba anawakemea wanaotaka kufunika hoja ya UFISADI kwa kutumia DENI la Mbowe ili naye aonekane fisadi, anyamaze, huku amekopa kihalali na analipa...? Unataka kusema wewe una akili ndogo kiasi ch akushindwa kuona SIASA katika deni la Mbowe?

Unawalaumu wakubwa kukopa, kwani ni siku gani wamewazuia wadogo kukopa? Au ni wivu tu wa kijinga? kwani unadhani kama Mbowe asingekopa hizo pesa ungekopa au ungepewa wewe? Au ni lini ulienda kukosa NSSF wakakuzuia kwamba usikope kwa sababu wewe sio kigogo? Acha utoto, jadili hoja.

Hili ni deni, sio wizi, wala Mbowe hajakataa kulipa, ila kuna ubishi wa kibiashara kuhusu riba iliyoongezeka, ambayo wanaobishana wakikubaliana atalipa. Sasa unawaambia CHADEMA waache kutetea UOZO, upi? Au umepotoshwa ukapotoka, sasa unatumia akili za balile na rostam kulifikiria hili? Sema usemalo, deni la Mbowe haliwezi kunyamazisha wananchi kutaka hatua zichukuliwe dhidi ya mafisadi wa EPA na Richmond zote mbili, ya Dar na ya Mwanza....Huna hoja kabisa...
 
Back
Top Bottom