Mbowe ajitenge na watuhumiwa wenzake

Tulianza na Mungu, tunaye Mungu na Tutamaliza na Mungu, hatuna ubaguzi, na hatutabaguana kama tunavyobaguliwa na makaburu weusi Tena wakileo.
 
Msingi wa kesi yote ni Mbowe Mwenyewe, yeye ndiye anashitakiwa kwa kutafuta vijana wa kufanya ugaidi na kufadhili huo ugaidi wa laki sita! Atajitenga vipi na hao walinzi wake?!
Kama ingekuwa kuna ukweli katika hayo mashitaka yeye ndiye mwenye kupata hukumu kali zaidi kuliko hata hao makomandoo.
 
Yaani sijaona alichojibu Kaaya kinachopelekea Mbowe kuwa Gaidi. Hajaonyesha Ugaidi wa Mbowe hata sielewi Ushahidi wake ni WA nini. Kampigia simu, kampa fedha ikawaje!!!???
Ushahidi wa kutunga mkuu...Yan unaona live..
 
Mkuu hii kesi ni taahira pekee ndiye atakaeamini kuwa mbowe gaidi hata hao walioitengeneza kesi hawajui gaidi ni mtu wa aina gani kutokana na uwezo mdogo wa akili(mazuzu)
 
Aliyemleta huyu kama shahidi ni bogus kama yeye mwenyewe.

Huyu kama wale wahuni wa Sabaya alipaswa kuwa kisongo.
Mia kwa Mia ndugu, hata mimi hili nakubaliana nawe....Kaaya kasema Uongo mchana peupe...eti alikutana na mbowe January huko longido wakati huo huo mwezi huo huo mbowe yuko gerezani, sasa sijui, hivi huyo mbowe alikuwa omni present ? Ni Mungu pekee mwenye sifa hiyo ya kuwa sehemu zote muda wowote...
 
Hakika. Uko sahihi kabisa. Mahakama itende haki ili tuone mwisho wa hii kesi na iwe fundisho kwa vyombo vya dola kujiingiza kwenye mambo ya siasa na kutengeneza kesi kwa lengo la kuwanyamazisha wanasiasa hasa wa vyama vya upinzani. Wote waende sambamba hadi mwisho.

Cc Keynez
 
Hapana Mbowe hatakiwi kuwa msaliti, na hata siku ya hukumu kama wenzake wakifungwa halafu Mbowe akaachiwa huru kwa kigezo jaji ameshindwa kuthibitisha uhusika wake kwenye kesi pasipo kuacha shaka sitapendezwa na hiyo hukumu, kwangu wote hawana hatia
 
Sawa bush lawyer
 
Una hoja lakini hapana, Mwenyekiti ninaemjua mimi hawezi kukubali hayo. hata kama jinai kila mshitakiwa husimama peke yake. lakini kwa sababu kesi ni ya kubumba basi hakuna kutenganisha mawakiri
 
Mh Mbowe ni kiongozu

Mh Mbowe ni Kiongozi lazima awe mfano hawezi kukubali ubaguzi huo. Walianza na Mungu watamaliza na Mungu
 
Nikisema matokeo ya siasa za CHADEMA zenye vimelea vya ubaguzi , ni kutoka na mentality kama hizi.

Thamani ya maisha ya mtu haipimwi kwa umaarufu wake. Ibara ya 13 ya Katiba inaelezea usawa wa kila mtu bila kujali daraja, jinsia wala nasaba.

Grow up dude, punguza kujadili kesi iliyopo mahakamani. Tunafuatilia kinachojiri na siyo kupiga ramli maamuzi ya mahakama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…