Mbowe akimbilia kwenye Maombi kurudisha mioyo ya wanachadema

Mbowe akimbilia kwenye Maombi kurudisha mioyo ya wanachadema

Ni Maombi ya kurudisha Mioyo ya Wanachadema Wamrudie Baba Yao

Kweli hali ni Mbaya kwa Mwamba, amekacha kwenye Mdaharo kaibukia kwenye Maombi, kama alivyoibukia Ikulu wakati watu wanamsubili mahakamani


Hakika Buyu la Asali limeguswaView attachment 3204644
1. Hivi Freeman Mbowe kufanya TOBA ya kuacha uongo na kuwa mkweli tu unahitaji kwenda kwa manabii feki hawa ili kukuombea, manabii wadanganyifu wasioweza kumwambia mtu ukweli Ili aache njia zake mbaya za maisha? Unadhani Mungu anaweza kuhongeka..??

2. Hivi Freeman Mbowe kukubali na kufanya TOBA tu kuwa umekosea, umekula rushwa na umewauza wenzako kwa Samia Suluhu Hassan (Mwenyekiti wa CCM) kwa urafiki wenu huo wa mashaka , unahitaji nabii feki kukuombea kweli Mbowe..??

3. Hivi kukiri na kufanya TOBA kuwa umewadharau na kuwatweza wanachama, wapenzi na mashabiki wa CHADEMA kuwa hawana "MAPESA" kuendeshea chama, sio MATAJIRI kama wewe na hivyo ukiondoka wewe CHADEMA itakufa, unahitaji kwenda kuombewa na manabii feki kweli Ili kuepuka adhabu na mapigo ya adhabu iliyo mbele yako...???

4. Hivi wewe Freeman Mbowe kufanya TOBA binafsi hata ukiwa chumbani kwako na ukiri tu kuwa umeshiriki ktk matukio mabaya ya kuwaumiza na kuwaua wenzako ndani ya chama kwa kushirikiana na "WASIOJULIKANA" wa CCM na serikali yao unahitaji manabii feki kukuombea mzee Mbowe...??

##Sikiliza mzee Mbowe: Huhitaji kupitia njia hiyo kutengeneza na Mungu wako muumba wa mbingu na nchi iwapo deep ndani ya nafsi yako unaelewa yapo makosa uliyoyafanya...

##Sikiliza mzee wangu Freeman Mbowe:

✍️Mungu wa mbingu na nchi HAHONGEKI...!!

✍️ Swallow your pride, beba msalaba wako wa aibu ya kukubali udhaifu na makosa yako, usiwaogope watu kuchagua njia salama ktk maamuzi yako kisha nenda kwa Yesu Kristo naye atakuweka Huru ila hatakuruhusu upate kile unachokitaka sasa hata kama utakwenda kwa shetani mwenyewe..!!!

Nakutakia kila la kheri..
 
Back
Top Bottom