Unajua kuna watu bado wana underate ukatili na consolidated power ya CCM.
What else are they going to do after kususia ??
Kwamba CCM wawaite wawabembeleze kwamba msijali, tunarekebisha tume, really ???
Tume huru ya uchaguzi + Katiba mpya itakuja kupatikana nchi hii kwa mbinde baada ya mapigano ya wananchi wenyewe. Case study ni Zanzibar (2007 ) na Kenya. Kikwete pekee ndiye aliyetaka kuleta katiba mpya kwa amani na akapigwa vita mnoo.
Imagine hapo Zanzibar, walitengeneza katiba inatiwahusisha mpaka wajumbe wawili wa upinzani lakini bado CCM wanapora tu kwa kutumia Jeshi!!!
Leo wewe unasusa, kwa msajili kuna vyama vya siasa zaidi 18 vinashiriki ( vingine vya kutafutia fursa tu mjini ) wewe unabaki kunung'unika tu.
Binafsi naamini kwenye kushiriki kwasababu:
- Ndio jukwaa la kutolea elimubya uraia na kutafuta kuungwa mkono.
- Licha ya ubovu wa katiba na Tume lakini upinzani umekuwa ukipiga hatua kubwa tu ( hii inasaidia kuimega dubwana CCM kidogo kidogo). Ni ngumu kutegemea huruma ya hao hao CCM au kusubiri uliangushe dude kama CCM oncr and for all.
- Most importantly, CCM kama chama ni kama hakipo. CCM ni Dola ( ndio nguvu wakiyo nayo ). Ndio maana hakuna mwanaCCM mwenye nguvu kuliko Rais ( labda Rais atake mwenyewe )
Hivyo, kushiriki kuna faida zaidi kuliko kususa . Ukisusa utakosa nguvu, kiuchumi na kupunguza uungwaji mkono. Hakuna asiyejua kuwa siku zote raia nao wana mahitaji yao ambayo ni tofauti ya wanasiasa ( ajira, maji, umeme, kodi, barabara, soko etc )
Anyway, let's wait and see maana kususa CUF wslisusa and nothing happenned, CCM walipora serikali za mitaa, Uchaguzi mkuu and nothing happened.
Ngoja tuone wakati huu, in case kutakuwa na any wonders.