Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 11,557
- 33,535
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ametumia mtandao wa X kulalamika kuhusu vitendo vya ubakaji wa Demokrasia unaoendelea kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Mbowe ameandika;
"Taifa linaendelea kushuhudia kwa njia mbalimbali ubakaji mkubwa wa demokrasia kwenye uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji.
"Wasimamizi wa "uchafuzi" huu wamekiuka kwa kiwango kikubwa hata kanuni na miongozo mibovu iliyotengenezwa kwa makusudi na hivyo kuweka mazingira ya ushindani usiyo wa haki.
Kupata matukio yote kimkoa kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa bofya hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
"Madhara ya ubatili huu ni kuendelea kukosekana haki, Uhuru na demokrasia ya kweli katika ngazi ya chini zaidi na ya kwanza katika Utawala wa nchi, kunakomgusa kila mwananchi.
"SamiaSuluhuHassan, Serikali na Chama chako mmeshauriwa kwa kila njia lakini hamjaonyesha chembe ya kujali haki za wananchi kwenye hili.
"Watanzania wote tunapaswa kutambua wajibu wa kukomesha uporaji wa haki katika uchaguzi huu hatimaye uko mikononi mwetu kila mmoja kwa eneo lake.
"Kwa namna ileile mnavyokosa amani katika mchakato huu, wahusika wachakachuaji wanapaswa nao kuishi kwa hofu na kukosa amani hadi pale watakaposimama katika haki kwa wote.
"Wananchi wasilaumiwe pale watakapochukua hatua kudai haki zao za msingi kwenye hili."