Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Mwaka 2020 Lissu kwa kujazwa upepo na wafuasi wake kiduchu na wale waishio nje ya Nchi na kwa kudanganywa na waliokuwa wamempa makazi huko ulaya akajiona kuwa ana uwezo wa kuwa RAIS wa Tanzania na kuchaguliwa kwa kura za kumpa ushindi.
Lakini Watu aina ya Mbowe Mwamba Mwenyewe na jabali la siasa za Upinzani wenye akili Timamu na wanaojitambua na wenye kuelewa mtu mwenye sifa na uwezo wa kuongoza Taifa hili walijua kuwa kamwe na katu Lissu hawezi kuwa Rais wa Nchi hii hata siku moja.
Ndio Maana Mheshimiwa Mbowe hakutaka kabisa kujihusisha na habari za kampeni za lissu na badala yake aliamua kumuacha lissu apuyange mwenyewe huku akijiongelea lolote lile linalomjia mdomoni mwake.
Ndio maana nyote ni mashahidi kuwa lissu hakuwa na sera za aina yoyote ile wala ajenda zenye kugusa maisha ya watu na zenye kuvuta hisia za watu wala kuwashawishi watu kumuunga mkono.ilani ya lissu na sera za lissu zilikuwa ni juu ya risasi alizopigwa 2017.muda mwingi akiwa jukwaani ndio zilikuwa sera za Lissu za juu ya habari za majeraha yake na risasi zake.
Ni kweli inaumiza na kila mtu alimuonea huruma juu ya madhira aliyoyapata na hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kutamani yamkute yaliyomkuta lissu.ni kweli Lissu ni Muujiza unaotembea,ni kweli Lissu ni ushahidi wa uwepo wa Mungu,ni kweli hatupaswi wanadamu kutendeana aliyotendewa Lissu,ni kweli Lissu amepitia mateso,maumivu ,machungu na kuona Roho yake ikiponea chupuchupu kukatika na kukatishwa,ni kweli Lissu kuna wakati katika hali ya kiubindamu inatia hasira na maumivu makubwa sana moyoni mwake,ni kweli ana haki ya kuwa na chuki kubwa sana moyoni mwake juu ya mtu yeyote yule anayefikiri alihusika katika jaribio la kutaka kuondoa uhai wake.ni kweli Lissu ameachiwa maisha ya mateso makubwa sana na maumivu makubwa sana ambayo hayakuwa na sababu ya aina yoyote ile ya kumfanyia vile.
Lakini yote kwa yote kama binadamu japo ninatofautiana naye kimtazamo na kiitikadi na katika mambo mengi sana.nampa pole kwa yote yaliyomkuta na asamehe tu na kusonga mbele kama ambavyo alifanya Papa John Paul wa II kwa kumsamehe aliyempiga risasi katika mwili wake. Mungu aliyemnusuru na kumpa nafasi ya pili ya kuishi anajua kwanini aliamua kumuokoa na kumpa nafasi ya kuendelea kuishi hapa Duniani kwa miaka mingine zaidi.
Lakini pamoja na madhira hayo aliyoyapata na kupitia bado hakupaswa kufanya madhira hayo kuwa ndio sera na ajenda kuu ya kampeni yake.kwa sababu wakati huo watanzania walihitaji kusikia habari na sera zake za uchumi katikati ya kufunga mikanda na kupaka girisi vyuma kama alivyosema Hayati Mwalimu Daktari John Pombe Joseph Magufuli pale watanzania walipolalamika juu ya ugumu wa Maisha na pesa.
Alipaswa kuja na sera zenye kuwashawishi watumishi wa umma hususani juu ya kuwapandisha madaraja ,kuwalipa malimbikizo ya madeni yao,kuwaongeza mishahara,kuwapa nyongeza ya kila mwaka lakini kubwa kuliko ilikuwa ni juu ya ajira kwa vijana ambao kwa kipindi na wakati huo walikuwa wengi sana mitaani pasipo ajira kutokana na zoezi la uhakiki wa vyeti feki na kuondoa watumishi hewa ambalo lilichukua muda mrefu na kuacha vijana wengi mitaani ambao mpaka sasa inakuwa ni ngumu sana kuwamaliza wote mitaani kuwaajiri .
Lakini pia alipaswa kuja na sera nzuri na za kiutafiti za kifedha na kiuchumi zenye kuleta mzunguko mzuri wa pesa mitaani,Masuala ya kodi ,biashara,uwekezaji na mengine mengi ya aina hiyo. Lissu kwa wakati huo alipaswa kuja na sera nzuri zenye kugusa watu hususani katika ustawi wa maisha yao ya kila siku.
Lakini kwa bahati mbaya sana kampeni za lissu na sera zake hazikutoa matumaini kwa vijana wala watumishi wa umma wala wakulima wala wafanyabiashara wala wawekezaji ambao wangeweza kuwekeza na kuzalisha ajira wala watanzania waishio nje ya nchi.Embu angali Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Alivyoingia madarakani namna alivyokuja na sera nzuri zilizovutia wawekezaji,watalii mpaka kufikia Millioni 1.8.
biashara kushamiri na kuanza kufunguliwa kila kona badala ya kufungwa ,kujenga imani kwa wawekezaji kuja kuwekeza Nchini,kuleta utulivu wa kisiasa na mazingira ya kuaminiana kupitia falsafa yake ya 4R,kuimarisha demokrasia,kutoa na kumwaga ajira kwa vijana,kuwapandisha madaraja na mishahara watumishi wa umma hususani wale wa kima cha chini kwa 23% ,kuimarisha diplomasia na hivyo kushuhudia wafanyabishara wakubwa wakiingia Nchini na kupandisha bei ya mazao kama vile korosho ambayo yalikuwa yameanguka soko lake baada ya kuvurugwa na mengine mengi sana.
Sasa hayo yote lissu hakuyafanya.hakuyafanya kwa sababu lissu hatoshi na hana maono ya kiuongozi wala hawezi kuwa Rais .ndio maana alikuwa anaongea vitu vinavyohusu mambo yake na maswaibu yake.hakukata kiu ya watanzania wala matarajio ya watanzania,hakujibu maswali ya watanzania na kuwapatia matumaini na hakuonyesha jambo jipya ambalo angeweza kufanya ikiwa angekuwa Rais.hakuwa na ladha ya mgombea wa upinzani na wala hakuwa na jipya lolote lile lenye kugusa hisia za watu kuweza kumuunga mkono.
Jambo hilo Mbowe alilijua vyema sana na kumfahamu vyema Lissu na kujua kuwa hakuwa mtu sahihi na hawezi kuwa na ushawishi kwa watanzania na ndio maana aliamua kujiweka pembeni tu ili amuache Lissu ajiakaange kwa mafuta yake mwenyewe.ikumbukwe Lissu alikuwa anataka kupata kura za huruma kutoka kwa watanzania ndio maana alitumia muda wake wote kujieleza yeye binafsi badala ya mipango yake kwa watanzania.
Mbowe ni kiongozi anayewafamu vyema sana watu wake maana kawalea mwenyewe.ila Lissu alikuwa na hasira na chuki kubwa sana na hayati Magufuli na akafikiri atatumia nafasi ile kuleta machafuko ili kumuondoa Hayati Magufuli kitini kwa hata kwa njia ya machafuko na maandamano jambo ambalo alishindwa kufanikiwa baada ya kukataliwa kuungwa mkono na mamilioni ya watanzania.
Ok ngoja niweke kalamu chini nitaendelea wakati mwingine kuwapeni uchambuzi na Elimu zaidi.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.