KWELI Mbowe alisema, ukitaka kujiunga na chama cha wizi ingia CHADEMA, lakini alisahihisha na kusema ingia CCM

KWELI Mbowe alisema, ukitaka kujiunga na chama cha wizi ingia CHADEMA, lakini alisahihisha na kusema ingia CCM

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Nimeona video inasambaa mtandaoni ikimnukuu mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe akisema kama unataka kujiunga na chama cha wadhulumaji, wizi wa kura, ulaji wa rasilimali za Taifa, giza na rushwa, ingia CHADEMA.

chadema-pc-data.jpg
Nimeshituka sana kusikia maneno haya kutoka kwa Mbowe. JamiiCheck tusaidieni kufanya uhakiki.


Video inayosambaa Mtandaoni


Video halisi
 
Tunachokijua
Juni 27, 2024, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alifanya mkutano Katesh, Manyara ambapo pamoja naye walikuwepo viongozi wengine wa chama hicho akiwemo Mbunge wa zamani wa Arusha Mjini Godbles Lema.

Mkutano huo ulirushwa mbashara na mitandao mingi ya kijami, ikiwemo ukurasa rasmi wa Mtandao wa YouTube wa Freeman Mbowe.

Baada ya kufanyika kwa mkutano huu, Juni 29, 2024 ilianza kusambaa video kwenye mitandao ya kijamii hasa Mtandao wa X ikidai Mwenyekiti Mbowe amewakaribisha wezi na wala rasilimali za nchi kwenye chama anachokiongoza.

"Unataka kujiunga na chama chenye dhulumati, wizi wa kura, ulaji wa rasilimali za Taifa, giza na rushwa, ingia CHADEMA" Mbowe.

Baadhi ya Akaunti zilizosambaza video hiyo zimehifadhiwa hapa, hapa na hapa.

Ukweli wa Madai haya upoje?
JamiiCheck imefuatilia madai haya na kubaini yana ukweli. Kupitia video iliyochapishwa kwenye ukurasa rasmi wa CHADEMA kwenye Mtandao wa Instagram, Freeman Mbowe anasikika akitamka maneno hayo.

Hata hivyo, Mbowe alisahihisha maneno yake tofauti na jinsi inavyosambazwa Mtandaoni.

Kwenye video nzima, Mbowe anasema "Sasa wewe mwananchi wa Katesh ambaye nakutaka uelewe kwamba siasa ni maisha yako usikae pembeni ukadhani siasa haikuhusu. Una wajibu wa kuchagua kati ya vyama viwili. Unapenda kusimama upande wa haki, nuru, matumaini, ingia CHADEMA. Unataka kujiunga na chama chenye dhulumati, wizi wa kura, ulaji wa rasilimali za Taifa, giza na rushwa ingia CHADEMA. Samahani, ingia CCM kisha maamuzi uyafanye"

Kupitia video hii, JamiiCheck imejiridhisha kuwa video inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii (Video 1) ni halisi, lakini imekatwa sehemu ya maneno ya Mbowe ili kufanya upotoshaji tofauti na ukweli ulivyo kwenye video ambayo haijakatwa (Video 2).

Upotoshaji wa taarifa unaweza kufanyika kwa njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kukata au kuhariri video ya mtu ili ionekane kana kwamba anasema mambo ambayo hajasema au kugeuza maana yake. Hii inaweza kufanyika kwa kubadilisha maneno yaliyosemwa au kwa kuunganisha vipande vya video ili kuunda maudhui yanayotofautiana na ukweli.

Ni muhimu kuzingatia uwazi na uwajibikaji katika kutumia video au taarifa za watu wengine ili kuepuka upotoshaji wa taarifa.
Back
Top Bottom