Uchaguzi 2020 Mbowe amekosea kugombea Ubunge

Msulibasi

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
5,947
Reaction score
7,939
Matatizo mengi na madhaifu ya CHADEMA Katika hatua mbalimbali za uchaguzi yanatokana na kukosekana uongozi WA Karibu wa mwenyekiti Mbowe.

Kukatwa kwa wagombea wengi wa CDM kwa sababu kadha wa kadha na kukosekana kwa nidhamu ya hotuba za mgombea uraisi Tundu Lissu ni baadhi ya kasoro ambazo Mwenyekiti angaliweza kuzipunguza.

Lisssu ana mihemko na hana timing nzuri. Kuna mambo huzungumzwa last week ya kampeni na mengine huzungumzwa mwanzoni.

Lissu amekiri kuwa Mbowe amebanwa HAI hivyo hawezi kusaidia maeneo Mengine.CCM hata mimi nisiye gwiji wa siasa niliwaza hivyo kwamba Mbowe afanyiwe siasa za kihuni Ili ashindwe kutoka Hai na niliandika hapa watu wa chadema wakanijia juuu.

Lissu hakupaswa kupita madukani magengeni na kwingineko. Lissu hakupaswa kusuguana na polisi Kiluvya. Alipaswa kuonesha ukomavu atulie
 
Matatizo mengi na madhaifu ya CHADEMA Katika hatua mbalimbali za uchaguzi yanatokana na kukosekana uongozi WA Karibu wa mwenyekiti Mbowe....
Alichofanya na anachofanya Lissu ni dalili ya ukomavu wa hali ya juu. Amebana matugu ya mapolisi hadi wameachia wenyewe. Asiye mkomavu hawezi hicho.

Wamemsimamisha kampeni lakini amewapiga chenga ya mwili anafanya kampeni babkubwa. Matatizo kama ya kuenguliwa yanasababishwa na tume iliyoteuliwa na mmoja wa wagombea na kufuata amri zake. Mbowe kugombea ubunge kulikuwa na umuhimu wake tu.
 
Matatizo mengi na madhaifu ya CHADEMA Katika hatua mbalimbali za uchaguzi yanatokana na kukosekana uongozi WA Karibu wa mwenyekiti Mbowe....
Umeandikiwa au umwandika ww kutoka kwenye kichwa chako.

Sorry japokuwa sifungaman na upande wowote wa siasa.

Hapo ukiposema lissu amekiri mbowe kubanwa? Amekiwi wapi ..lini na kwenye mkutano gani?

Unasema lissu hakutakiwa kupita madukani? Ww kama nan?

Maana kule haendi kufanya kampen ..anafanya manunuzi ya vitu vyake binafsi. Hata yeye ni binadam ana mahitaji pia. So lazima atoke akanunue.
 
Kumbuka Lowassa alipanda daladala pia alikuwa anaitwa Rais, Rais!! Huyu naye anapitia njia hiyo hiyo!! KIFUATACHO tarehe 28/10/2020 KINAFURAHISHA!!
 
Kumbuka Lowassa alipanda daladala pia alikuwa anaitwa Rais, Rais!! Huyu naye anapitia njia hiyo hiyo!! KIFUATACHO tarehe 28/10/2020 KINAFURAHISHA!!
Kila siku mnaambiwa Lissu sio Lowassa lakini hamsikii, ole wenu muibe kura safari hii mtajuta.
 
Chama cha mbowe kitapotena sana baada ya 28 oct maana hawatafika hata wabunge 10 mwaka huu! Mwenyekiti wao tu hoi huko hai!. Mbelgiji pia atapigwa kipigo cha mbwa koko ! haijawai kutokea toka historia ya vyama vingi! .
 
Matatizo mengi na madhaifu ya CHADEMA Katika hatua mbalimbali za uchaguzi yanatokana na kukosekana uongozi WA Karibu wa mwenyekiti Mbowe...
Tatizo lenu LUMUMBA hata kuigiza hamjuagi. Yaani andiko lako liko wazi kabisa (umetumwa) na linaonyesha ni jinsi gani CHADEMA wamewaumiza saana na wamewashika pabaya. Nikuulize maswali machache; Mbowe angewezaje kuzuia kuenguliwa kwa wagombea ambao mmewaengua kupitia vibaraka wenu TUME,POLISI na WAKURUGENZI?

umesahau mara hii kuwa kama usingekuwa ushupavu wa Chadema chini ya uongozi mathubuti wa Mbowe mgefanikishalengo lenu mlokuwa mmepanga la kuwaengua zaidi ya 50% ya wagombea Ubunge Chadema, huku msisitizo ukiwa kwenye majiji yote?

jiulize imekuwaje mkashindwa?..Pili ulitaka Lissu asizungumzie mapema swala la Ujenzi wa uwanja wa ndege chato,undugunaizesheni na ukabilaizesheni wa JIWE aje auzungumzie wakati gani? acha kupepesa macho mmeshikwa pabaya
 
Kumbuka Lowassa alipanda daladala pia alikuwa anaitwa Rais, Rais!! Huyu naye anapitia njia hiyo hiyo!! KIFUATACHO tarehe 28/10/2020 KINAFURAHISHA!!
Kuna Lissu na Lowassa. Lissu ni wa 2020 na Lowassa alikuwa 2015. Tunaongea habari za Lissu.
 
Matatizo mengi na madhaifu ya CHADEMA Katika hatua mbalimbali za uchaguzi yanatokana na kukosekana uongozi WA Karibu wa mwenyekiti Mbowe....
Nimesikiliza hotuba zote za lisu zinaeleweka hakuna mapungufu kama wewe unavyodai lissu yupo makini na uhakika na mambo anayozungumza maamuzi yote ya tume yanatolewa na rais ipo wazi ufisadi unamtesa Magufuli
 
Kila siku mnaambiwa Lissu sio Lowassa lakini hamsikii, ole wenu muibe kura safari hii mtajuta.
Tena Lowassa alikuwa smart zaidi kuliko huyu msaliti. Juzi amehenyeshwa masaa 9 anapigwa jua na mbu pale Kibaha! Then you are saying he is very smart than Lowassa!?! Are you serious???!!!
 
Tena Lowassa alikuwa smart zaidi kuliko huyu msaliti. Juzi amehenyeshwa masaa 9 anapigwa jua na mbu pale Kibaha! Then you are saying he is very smart than Lowassa!?! Are you serious???!!!
Huyo Lowassa hata kuongea alikuwa hajui sijui huo u smart wake umeutoa wapi?!

Mnaropoka tu.
 
Ndo anavyowadanya na kujifariji kirahisi hivyo! Lissu hatoweza kufanya chochote !.watanzania sio wajinga ,kukubali kuingizwa barabarani!. Atakachokipata atamsimulia Amsterdam!
Mnajidanganya kuiba kura halafu mnadhani mambo yataenda kama zamani, mtajuta, this time the whole world is watching.
 
Mnajidanganya kuiba kura halafu mnadhani mambo yataenda kama zamani, mtajuta.
Hivi mnaweza kushinda majimbo 264 nyie ukiacha tu Urais? Kwa chama kipi mlichonacho ! Mwentekiti wenu tu watu hawamtaki huko hai!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…