SI KWELI Mbowe amesema hagombei Uenyekiti ila Lissu ataua chama

SI KWELI Mbowe amesema hagombei Uenyekiti ila Lissu ataua chama

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Mbowe alisema kuwa Lissu ataua Chama?

1734977817940.png
 
Tunachokijua
Freeman Mbowe ni Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA akianza kuitumikia nafasi hiyo mwaka 2004 ambapo ameendelea kuishikilia mpaka sasa 2024. Watu wengi wamekuwa na shauku ya kushuhudia uchaguzi ujao wa viongozi ndani ya Chama hicho ngazi ya taifa, jicho kubwa likiwa katika nafasi ya Mwenyekiti, nafasi ambayo imeshikiliwa kwa zaidi ya miaka 20 na Mbowe. Itakumbukwa pia Mbowe alikuwa ni moja kati ya waasisi wa chama hicho mwaka 1992.

Desemba 18, 2024 Wanachama wa CHADEMA walikusanyika Nyumbani kwa Freeman Mbowe kwenda kumshawishi agombee tena nafasi ya Uenyekiti CHADEMA kwa kipindi kingine ambapo inategewa uchaguzi wa kumchagua Mwenyekiti utafanyika Januari 2025 kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na John Mnyika ambaye ni katibu wa chama hicho.

Mpaka kufikia Desemba Desemba 18, 2024 ni Tundu Lissu alikuwa amethibitika kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa chama kwa ngazi ya Taifa.

Kumeibuka chapisho lilonayodaiwa kuchapishwa na JamiiForums likimnukuu Freeman Mbowe akisema hagombei nafasi ya Uenyekiti ila Tundu Lissu ataua watu.

Je, ni upi Uhalisia wa Machapisho hayo?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa chapisho hilo lenye Nembo ya JamiiForums halina ukweli na wala halijawahi kuchapishwa katika kurasa rasmi za JamiiForums.

Chapisho hilo linadai kuwa Freeman Mbowe amesema hatogombea Uenyekiti lakini ufuatiliaji wetu rasmi umebaini kuwa Mnamo Desemba 21, 2024 Mbowe alizungumza na Waadishi wa Habari na kutangaza rasmi kuwa atagombea nafasi ya Uenyekiti (Tazama hapa na hapa).

Aidha, JamiiCheck imebaini pia Chapisho hilo na mengine yenye mtazamo huo yanaanzia katika Kundi Sogozi la FaceBook linalojiita CCM Taifa Tanzania 2024 - 2030 chini ya Mama Samia.

1735009779374-png.3183699

Baadhi ya Machapisho yanayozalishwa katika kundi hilo la FaceBook

Aidha chapisho hilo lina utofauti wa mambo kutoka katika machapisho halisi ya Jamiiforums

  • Aina ya Mwandiko (Font type) zilizotumika hazitumiwi na JamiiForums,
  • Uwepo wa Tag ya Habari kwenye posta ya Siasa ni tofauti na tag inayotumiwa na JamiiForums
  • Rangi zilizopo kwenye posta hii hazitumiwi na Jamiiforums kwenye posta za Siasa
Back
Top Bottom