Mbowe amethibitisha kuwa hata kama CHADEMA ingechukua Serikali, kama yeye akiwa Kiongozi Mkuu, hakuna la pekee

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,362
Reaction score
48,879
Leo hii, kama upo ndani ya CCM, na una sifa zote, lakini ukachukua fomu kumchallenge Samia kwenye nafasi ya Urais au Umwenyekiti wa CCM, huo utakuwa ndiyo mwisho wako kisiasa ndani ya CCM.

Leo hii, kama upo ndani ya Serikali, halafu ukaikosoa Serikali au Rais au mwenyekiti wa CCM, huo itakuwa ndiyo mwisho wa nafasi yako ya uongozi au ajira yako.

CCM na Serikali yake inataka watu wote kuwa machawa, wasitumie akili zao hata kama wanazo, kazi yao iwe ni kushangilia na kusifia watawala tu, hata pale wanapoharibu.

Tabia hizi mbaya za kimfumo ndani ya CCM ndizo zinazowasukuma watu wengi kutaka mabadiliko ya kiutawala, na kikatiba. Na mabadiliko haya, kwa kiasi kikubwa wananchi wanayatafuta kupitia vyama vya upinzani, hasa CHADEMA.

LAKINI, kupitia chaguzi ndani ya CHADEMA, zinazotarajiwa kufanyika mwezi huu, wengi tumegundua kuwa kumbe yale tunayoyapigia kelele ndani ya CCM, hata kama CHADEMA ikichukua uongozi, chini ya Mbowe, hali itakuwa kama hiyo hiyo ya CCM au mbaya zaidi.

1) Mbowe anaiona na anaamini kuwa CHADEMA ni mali yake binafsi, na wengine wote ni wageni wanaotakiwa kukubaliana na kile anachokitaka yeye na familia yake. Sawa na CCM wanavyoona kuwa nchi hii ni yao pekee yao, na wao pekee ndio wanaotakiwa kuongoza.

2) Mbowe, kama ilivyo CCM na viongozi wake, anaamini katika makundi ya machawa. Hawa ni watu wasiotumia akili, hawahitaji akili, kwa kuwa kazi yao ya kushangilia na kusifia kwa lolote, haihitaji akili. Hii ndiyo hali ile ile iliyopo ndani ya CCM, machawa wa Rais.

3) Mbowe, haamini katika uongozi wa kupokezana, na anaamini kuwa hakuna anayetakiwa kuwa kiongozi mkuu isipokuwa yeye tu. Hii ni sawa na CCM inavyoamini kuwa hakuna chama kinachostahili kuongoza Serikali isipokuwa CCM tu, na kwamba familia fulani ndiyo CCM yenyewe, na ndiyo Serikali. Wengine wote ni wageni, batawakiwemondani ya Serikali, wameletwa kama wasaidizi wao.

4) Mbowe anaamini kuwa anayetaka kuwa kiongozi mkuu wa CHADEMA ni msaliti, na anatakiwa kufukuzwa. Na haya ameyafanya huko nyuma, na sasa ameahidi kufanya vivyo hivyo kwa Lisu. Ni yale yale ya CCM. Membe alipojaribu kugombea Urais dhidi ya Magufuli, alifukuzwa uwanachama.

Hivi tunaamini Serikali iwe chini ya Mbowe, au Serikali iwe chini ya CHADEMA, halafu Mbowe awe kiongozi mkuu wa CHADEMA, anaweza kusimamia upatilanaji wa katiba mpya ambayo itapunguza madaraka ya Rais na kuyapeleka zaidi kwa umma! CHADEMA, chini ya Mbowe, ina nini cha kuwaambia wananchi hata waamini kuwa Mbowe akiwa kiongozi mkuu wa Serikali au chama kinachoongoza Serikali, kutakuwa na lolote tofauti na wanavyofanya CCM?
 
CHADEMA ni mali ya familia. Nanyi kaanzisheni chenu kama ni rahisi au kama mnataka cha umma.
 
Kwanza nashukuru huu uchaguzi umenifanya niyajue mengi kwa kifupi sana tofauti kati ya MBOWE na CCM ni majina tu na niwe mkweli kama FAM akiendelea chamani naacha kufuatilia hizi siasa za vyama vya upinzani mazima
 
una kadi ya chadema au unafatalia kama dada yako anavyofatia tamthilia
 
Back
Top Bottom