Vitoto vya siku hizi sijui inahitaji mpitie yapi ili akili zenu ziweze kupevuka na kuweza kudadavua mambo.
Mbowe alishaongea wakati akitangaza kugombea, hakuwa na cha kujibu kwa kuwa mpaka wakati huo hakuna kilichoelekezwa kwake kuhitaji majibu.
Kilichotokea, mara baada ya Lissu kutangaza kuchukua form circle ya wapambe wake walimshambulia sana Tundu Lissu. Yeye pia, wakati akitangaza kugombea, alitumia muda mwingi kumshambulia yule anayemuona ni mpinzani wake, pia akatumia kujibu shutuma na hoja ambazo hakuelekezewa bali ni msswali na hoja zilizojengwa na dhamira yake inayomsuta.
Kitendo cha speech ya Mbowe kutoendelea kujadilika na kuishia kuyayuka kama moshi, ni sababu wa wepesi wake, viliishia kuduma kwa masaa 36 pekee.
Majibu, sera, mikakati na hotuba za Lissu vinavutia, vinaishi vichwani mwa watu, ndiyo maana hadi leo wanavijadili utadhani labda ametoka kuviongea just masaa mawili yaliyopita huku wengi wenu mkiambiwa mtukumbushe Mbowe alionfea nini kwenye hotuba yake, mnachokumbuka ni kutangaza kuchukua form na kustaafu akiwa na umri wa Mtei. Sidhani kama zaidi ya hayo kuna kingine mnakikumbuka katika hotuba ile ya zaidi ya saa moja