Vawulence
JF-Expert Member
- Jan 4, 2009
- 1,930
- 2,118
Wakuu habari za usiku?
Jana niliwaahidi kuwaletea picha juu ya mikutano ya kampeni za Mbowe jimboni Hai mchana wa leo.
Naomba mnisamehe kwa kushindwa kuziweka hapa kwani kifaa changu cha mawasiliano kinanitoa ushamba. Kama ilivyokuwa pale Arusha jana ndivyo ilivyokuwa hapa Hai ambapo Mbowe anashindana na mgombea wa CCM Fuya Kimbita.
Katika hali ya kustaajabisha,wana wa nchi walipiga mayowe kila waliposikia jina la mgombea huyo wa ccm ambaye pia ni mbunge aliyemaliza muda wake.
Katika kampeni hizo zilizotawaliwa na amani ya hali ya juu,Mbowe alifanya takribani mikutano 25 aliyoiita ya kusalimia wana wa nchi. Sehemu nyingi wana wa nchi walisikika wakimuita KAKA WA UKWELI na kumuahidi kumpatia madiwani wa kutosha kwani yeye ni mbunge tayari.
Katika mikutano yake aliwataka wale wote wanaopenda ufisadi waichague CCM,Kama wanataka umasikini waichague CCM. Pia hakuogopa kuwaambia polisi waliokuwa wakilinda mikutano yake wasiache kuichagua CHADEMA.
Wakati akitokea mji Mdogo wa Bomang'ombe, wana wa nchi walifunga barabara kwa takribani dakika 45 kwa lengo la kumsalimia Mbowe hivyo kuzuia magari yasipite hadi pale polisi wa FFU walipowasihi kupisha upande mmoja wa barabara.
Nina picha nyingi tu ila nimeshimdwa kuziatach kwani niko mobile. Kama kuna mwenye uwezo wa kuziweka hapa JF,zinapatikana kwenye page yangu ya FACEBOOK ambayo ni Isaac 'Ankali' Babu. Video nitaziweka youtube.