Historia ya nchi hii ni ndefu na pana.
Lakini sasa mh mbowe anakwenda kuibadirisha na kuwa ya kusikitisha badala ya kutia moyo kwa upande mmoja. Na kwaupande wa pili vizazi vijavyo vitakuja jifunza ujasiri wa Mbowe ktk kusimamia haki na kuitaka mikononi mwa wadhalimu.
1. KUSIKITISHA
Mh. Mbowe ni MtanMbowetunayemfahamu vizuri, kitendo cha kudai tume huru na katiba mpya mpaka kumtengenezea kesi ya ugaidi, INAUMIZA SANA!
Miaka ile ya kikwete Zanzibar makanisa yalichomwa moto na paroko mmoja kuuawa. Mihadhara ya kiislam ilitukana sana dini ya kikristo, karate zilifundishwa misikini. Intelijensia ya kikwete ikawabaini mashehe kadhaa kuhususika na ugaidi.
Mh Samia amewatoa mara alipoingia. Watu tunajiuliza intelijensia gani hii iyobaini kuwa mbowe ni gaidi?
Amefanya jambo gani la kigaidi au amekutwa na kitu gani kinachotia mashaka au kuonesha Moja kwa mmoja kuwa anastahiri kutuhumiwa ugaidi?
2. UJASIRI
Toka mbowe ameingia upinzani, hajapata raha na radha ya siasa kama wanavyopata wengine -- Misukosuko, taabu, dhiki na madhira kibao. Lakini amesimama imara kuitetea na kuidai haki na kuidai kutoka kwa wadharimu. Hii inaenda tengeneza historia nyingine, kumpata mtu mwingine jasiri anayekubali kudhalilika kwa maslahi ya wengi.
Tumeona wengine wamefutiwa mashtaka lakini Mbowe mashitaka yapo palepale. Hii inatuonesha serikali ya samia suluhu lengo lake ni Mbowe.
Jumuia za kimataifa zitamuweka Mbowe kwenye orodha ya mashujaa hasa tukipata Uhuru wa kweli na katiba mpya.