Mbowe anaenda kubadilisha historia ya Tanzania

Mbowe anaenda kubadilisha historia ya Tanzania

Moyo wa mtu msitu. Mbowe anaweza akawa gaidi au sio gaidi, ukweli utajulikana na mahakama itaamua. Hata enzi za Zaire kuna watu hawakuamini kama Mobutu ameshiriki mauaji ya Lumumba kutokana na wema alioanza kuuonesha kwa wazaire wa wakati ule, lkn baadae ikaja kujulikana na kugundulika kuwa yeye (Mobutu) ndio alikuwa chanzo cha mauaji yale ya kinyama kwa waziri mkuu wao, pia wakaja kugundua kuwa Mobutu alikuwa ni mtu katili kuliko ukatili wenyewe.
Ulichoandika ndicho kinachopaswa kuandikwa na mwanadamu anayejua maana ya uanadamu......moyo wa mtu ni kiza kinene.....

Kama kweli Mbowe ameonewa basi laana iwashukie watesi wake....na kama Mbowe ametenda haya anayoshutumiwa laana ya Mungu imshukie.......
 
Hakika mkuu.. binadam huwa tunapenda kulaumu au kutetea kitu tusichokijua uhalisia wake.
 
One vampire is dead and rotting in hell! This female vampire will be extinct very soon lest she changes for the better.
Who are you to let her extinction?!

Are you deluled ?!!!

ENDELEZA KUUFUKUZA UPEPO
 
(AU) mama kaamua kuheshimu mhimili wa dola ili asiingilie mihimili ya dola ndo maana yupo kimya??.

Maana wabongo hatueleweki..raisi akiongea utasikia "Anaingilia mhimili wa dola na mahakama" Akikaa kimya utasikia "Ndo wale wale"

Najaribu kuwaza lakini
 
Historia ya nchi hii ni ndefu na pana.

Lakini sasa mh mbowe anakwenda kuibadirisha na kuwa ya kusikitisha badala ya kutia moyo kwa upande mmoja. Na kwaupande wa pili vizazi vijavyo vitakuja jifunza ujasiri wa Mbowe ktk kusimamia haki na kuitaka mikononi mwa wadhalimu.

1. KUSIKITISHA
Mh. Mbowe ni MtanMbowetunayemfahamu vizuri, kitendo cha kudai tume huru na katiba mpya mpaka kumtengenezea kesi ya ugaidi, INAUMIZA SANA!

Miaka ile ya kikwete Zanzibar makanisa yalichomwa moto na paroko mmoja kuuawa. Mihadhara ya kiislam ilitukana sana dini ya kikristo, karate zilifundishwa misikini. Intelijensia ya kikwete ikawabaini mashehe kadhaa kuhususika na ugaidi.

Mh Samia amewatoa mara alipoingia. Watu tunajiuliza intelijensia gani hii iyobaini kuwa mbowe ni gaidi?
Amefanya jambo gani la kigaidi au amekutwa na kitu gani kinachotia mashaka au kuonesha Moja kwa mmoja kuwa anastahiri kutuhumiwa ugaidi?

2. UJASIRI
Toka mbowe ameingia upinzani, hajapata raha na radha ya siasa kama wanavyopata wengine -- Misukosuko, taabu, dhiki na madhira kibao. Lakini amesimama imara kuitetea na kuidai haki na kuidai kutoka kwa wadharimu. Hii inaenda tengeneza historia nyingine, kumpata mtu mwingine jasiri anayekubali kudhalilika kwa maslahi ya wengi.

Tumeona wengine wamefutiwa mashtaka lakini Mbowe mashitaka yapo palepale. Hii inatuonesha serikali ya samia suluhu lengo lake ni Mbowe.

Jumuia za kimataifa zitamuweka Mbowe kwenye orodha ya mashujaa hasa tukipata Uhuru wa kweli na katiba mpya.
Last time I checked, mahakama ilitengua hukumu ya faini ya mamilioni ambayo Mbowe na wenzie walihukumiwa enzi za Mwendazake. Na baadhi yetu tuliposema "Mama ameanza vizuri" tulifokewa kuwa "kwani Mama ndio mwenye mahakama"?

Last time I checked, Mdude alipoachiwa huru na mahakama mlituambia sio Mama Samia aliyewezesha hilo bali mahakama. Iweje sasa maamuzi ya mahakama yageuzwe kuwa lawama kwa Mama Samia?

Vuteni subira. Mahakama iliyomkuta Mdude hana hatia inaweza pia kumkuta Mbowe hana hatia. Muwe wastahimilivu.
 
Huyu bhana pamoja na kuzaliwa kipindi cha uhuru lakini dalili zinaonesha anaenda kukuza uhuru wa kufurahia demokrasia hapa nchini.

Ninatamani sana kesi yake ingurume ili tuone matendo ya kigaidi aliyoyafanya ili nilinganishe na ya Ole Sabaya na ya Mnyeti halafu ikiwezekana afungwe kabisa si mchezo.

Wakati mwingine unawaza pia kwa kuwa inasemekena anaumwa, hivi ikitokea anafariki mikononi mwao itakuwaje?

Tunakosa hekima na busara katika kiwango cha kutisha! Ninamkumba JK kwa kweli!
Kwasasa serikali inapika ushahidi

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Moyo wa mtu msitu. Mbowe anaweza akawa gaidi au sio gaidi, ukweli utajulikana na mahakama itaamua. Hata enzi za Zaire kuna watu hawakuamini kama Mobutu ameshiriki mauaji ya Lumumba kutokana na wema alioanza kuuonesha kwa wazaire wa wakati ule, lkn baadae ikaja kujulikana na kugundulika kuwa yeye (Mobutu) ndio alikuwa chanzo cha mauaji yale ya kinyama kwa waziri mkuu wao, pia wakaja kugundua kuwa Mobutu alikuwa ni mtu katili kuliko ukatili wenyewe.
Kwa hiyo unasema hata Samia Suluhu naye atakuja kujipambanua kuwa kiongozi katili, mwonevu, anayebambikia wapinzani wake ugaidi ili mradi aendelee kukaa madarakani, au wewe unasemaje, maanake maelezo yako hapa yanaonekana kuwa hivyo ndivyo unavyodhani itakuwa baada ya nchi hii kuondokana na utawala wa kikatili wa CCM na viongozi wake.
 
Moyo wa mtu msitu. Mbowe anaweza akawa gaidi au sio gaidi, ukweli utajulikana na mahakama itaamua. Hata enzi za Zaire kuna watu hawakuamini kama Mobutu ameshiriki mauaji ya Lumumba kutokana na wema alioanza kuuonesha kwa wazaire wa wakati ule, lkn baadae ikaja kujulikana na kugundulika kuwa yeye (Mobutu) ndio alikuwa chanzo cha mauaji yale ya kinyama kwa waziri mkuu wao, pia wakaja kugundua kuwa Mobutu alikuwa ni mtu katili kuliko ukatili wenyewe.
Acha uongo,???
 
Jambo la kufikirika hili.

Enyi watanzania mmepewa viungo vya mwili na akili. Vitumieni kumtetea Mbowe. Msijipe moyo kwamba kuna siku mawe yataongea.

Mbona Syria, Cameroon, Gabon, Korea Kaskazini, n.k ambako kuna udikteta uliyokomaa mawe hayaongei???
Muda bado
 
Hakika mkuu.. binadam huwa tunapenda kulaumu au kutetea kitu tusichokijua uhalisia wake.
Watu wameacha mahaba yawaamulie mpaka wanampa mwanadamu sifa ya malaika.....

Mbowe anaweza akawa anaonewa au lakini vile vile tusiongee tukamaliza.......
 
Kwenye hili Samia nimemdharau na kumshusha viwango mpk kuwa sawa na tissue paper iliyotumika.
Sasa Samia kafanya nini?
[emoji16][emoji16][emoji16]Dahhh..!!!

Hata kama Samia ndo anahusika na kukamatwa kwa jamaa ni sawa tu kwasababu yeye ndio rais ndio mkuu wa nchi,huwezi kukubali kuwa raisi anayepelekeshwa na akina Mbowe halafu ukasema nchi yangu ipo salama,she's strongest president ever..
 
Sasa Samia kafanya nini?
emoji16.png
emoji16.png
emoji16.png
Dahhh..!!!
Kama unadhani Samia hahusiki na kukamatwa na kwa Mbowe, basi hujui namna nchi inavyoendeshwa.

Kwa Samia, tumepigwa. Mungu iburute Tanzania.
 
Back
Top Bottom