Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 37,630
- 47,434
Uadilifu ni sifa kuu na ya msingi anayopaswa kuwa nayo kiongozi yeyote yule wa Taasisi ya uma.
Chadema kama chama kingine cha siasa ni Taasisi ya uma kwa kuwa imesajiliwa kwa kufuata sheria za nchi zinazoongoza vyama vya siasa hapa nchini kwa maana hiyo haikwepi kuwa na vigezo muhimu vya taasisi yeyote ya uma ikiwa na kigezo nilichokitaja awali cha uadilifu wa viongozi wake.
Jana siku ya tarehe 4/03/2022 DPP Kupitia kifungu cha 91 Cha Sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai aliamua kufuta mashitaka ya Ugaidi dhidi ya Mwenyekiti wa Chadema na wenzake watatu.
Kwa kupitia kifungu hicho tafsiri yake ni kwamba pale ambapo itaonekana inafaa DPP anaweza yarejesha mashitaka hayo.
Hiyo inamaana kwamba kesi iliondolewa mahakamani bila ya Mbowe kutoa utetezi wake mahakamani na hatimaye mahakama kutoa maamuzi kuhusiana na tuhuma hizo.
Kwakua hakuna hukumu yeyote ile ya mahakama iliyosema kwamba Mbowe hajafanya alichotuhumiwa nacho au kakifanya na kwakua bado. DPP anaweza kurejesha tena kesi mahakamani basi kiufundi tunasema kwamba tuhuma dhidi ya Mbowe zinabakia pale pale.
Kwakua tuhuma bado zipo kwakua hakuna rekodi ya mahakama inayomsafisha Mbowe na tuhuma dhidi yake basi kwa manufaa mapana ya Chadema na Taifa kwa ujumla inampasa Mbowe kujiuzulu nafasi yake ya Uwenyekiti na kukaa mbali na siasa za kiushindani.
Inampasa Mbowe kujiuzulu kwani anakosa sifa muhimu ya uadilifu kwani tuhuma dhidi yake ni kubwa na hatarishi kwa ustawi wa Taifa lolote na haitakuwa afya kwa chama kuongozwa na kiongozi ambaye anaishi na tuhuma hizo.
The good things could have been to let Mbowe testify and the court to rule as to whether Mbowe is guilty or not but so far as we speak the allegations have not been cleared against him thus he must resign.