Mbowe anapaswa kubeba lawama ndio chanzo cha yanayoendelea CHADEMA


Hata Mbowe bado ni kiongozi ndani ya CHADEMA. Kwani hujui kuwa yeye bado ni mjumbe wa kudumu wa kamati kuu?. Kwa nini hajitokezi katika operesheni za chama?.

Kwani Mbowe hajui kuwa Mwenyekiti wa chama yuko ndani, Msajili kamkataa katibu mkuu, na makamu mwenyekiti anapokea vitisho kila kukicha, kwa nini hajitokezi na kutoa kauli ya kumotivate wanachama wakiunge mkono chama chao na kukipigania chama katika kipindi hiki kigumu chama kinapopata mashambulizi kutoka kwa dola kutoka kila kona?
 
Hata Mbowe bado ni kiongozi ndani ya CHADEMA. Kwani hujui kuwa yeye bado ni mjumbe wa kudumu wa kamati kuu?. Kwa nini hajitokezi katika operesheni za chama?.
Mbowe ndio mjumbe pekee wa Kamati Kuu? Na huo ujumbe ameupata kutokana na wadhfa aliokuwa nao na si kwa kupigiwa kura au kuteuliwa. Kwa nini ajiunge katika operesheni ambazo hakubaliani nazo? Mmesahau jinsi Lissu alivyokuwa anakataa wazi wazi kuunga mkono mkakati wa maridhiano? Na hakujihusisha katika kampeni za mwaka 2024 kwa sababu alisema chama chake hakijajitayarisha. Kuna wakati chama chake kilitangaza kuwa kutakuwa na kikao cha KK. Siku ya kikao Lissu akaitisha presa akiwa Singida! Yote hayo mmeyasahau?
Hivi mnataka Mbowe aseme nini wakati mlimuandama na matusi ilipojulikana kuwa alienda kumtembelea Lissu akiwa gerezani. Si Heche au Mnyika aliyekemea matusi yale na kumtetea kuwa alikuwa na haki ya kumtembelea Lissu na wala hakuwa na nia mbaya.

Sera ya siasa za nginja nginja ni za uongozi wa sasa na sio wa Mbowe. Walitakiwa wawe wamejipanga kukabiliana nayo.

Wenye wajibu wa kukiunganisha chama dhidi ya changamoto wanazopitia sasa ni uongozi uliopo madarakani. Madala yake wanawatenga na kuwafukuza wapambanaji wenye experience ya mapambano kama hiyo. Mbowe si mnafik. Pambaneni wenyewe. Mkishinda tutawapa pongezi mnazo stahili.

Amandla...
 
Kwanini Mbowe alaumiwe kwa makosa ya wengine? Unapaswa kumshukuru Mbowe kwa kujenga chama kikubwa cha upinzani kuwahi kutokea Tanzania na sio vinginevyo!
Africa tuna shida sana kwenye "succession plans". Hili ni tatizo kubwa sana sana kwenye familia, biashara, taasisi na serikalini.
Mbowe naye ni sehemu ya tatizo na anastahili lawama kwa yanayoendelea.
Kwa nini utengeneze watu wakuamini wewe ni si taasisi!!?
Kwa nini ametengeneza " u mungu mtu"!!??
 
Well said
 
Hoja ya matusi sijui katukanwa sana ni hoja ya "kimahusiano" zaidi, si hoja ya mtu aliyekomaa kichwani na kuwa na hekima, akili, busara na werevu mkubwa.

Hoja ya msingi ni kushindwa kwa Mbowe kutengeneza taasisi imara badala yake akajitengeneza yeye kuwa "mungu mtu".

Aliyekubaliana na Mbowe kuwa anatoa pesa yake mfukoni kwa ajili ya kuendesha chama naye ameshiriki katika hii hali ya kumtengeneza kuwa "mungu mtu" kwa baadhi ya wafuasi wa CHADEMA wakiamini maisha ya siasa bila Mbowe kuwa kitini, hayatakuwa safi.

Leo hii kuna mamia ya wana CDM ambao walikuwa ni wanufaika wa moja kwa moja na uwenyekiti wa Mbowe ambao ndio wanaoona maisha yao bila ya Mbowe hayataenda vyema.
 
Hatari MAHANJU
 
Mnafanana na wauwaji, Mbowe mmeshamtoa kama kibaka na mkamweka Lissu, leo mmeachana na Lissu mmemrudia tena Mbowe, nyie ni wauwaji MAHANJU
 
Umemalizaaa
 
Hapana. Kutayarisha taasisi imara ni kuweka watendaji wenye uwezo wa kuisimamia na kuiongoza wakati wewe haupo. Sasa kama utawala ulioingia inawaweka pembeni wote ambao walikuwa na uzoefu wa kuiendesha, unategemea nini? Mambo kama haya yametokea Marekani ambako Musk alifukuza watu bila kujua umuhimu wao katika hizo taasisi. Haikuchukua muda akawaomba warudi tena. Ndicho walichofanya wakina Mnyika. Palitakiwa kuwa na transition period lakini inaelekea kaikuwepo.

Hakuna mtu ana sabotage CDM ati kwa sababu kibarua chao kimeingia mchananga. Wanajihujumu wenyewe kwa ineptitude yao. Magunia ya misumari imeondoka sasa kazi kwao.

Amandla...
 
Mbowe ni mwanasiasa TL ni mwanaharakati tayari ushapata jibu hapo
 
Vita dhidi ya kuidhoofisha CHADEMA ni ile ile, utofauti ni anayeongoza hayo mapambano.

Kufanikiwa CHADEMA sifa atapewa TAL, kufeli kwa CHADEMA ni upande wa pili wa shilingi, hakuna shilingi ya upande mmoja.

FAM alishawahi kukaa gerezani na kunyolewa kipara.
 

Wajumbe wa Kamati Kuu wako wengi, kwanini Mbowe?
 
Mwisho wa ubaya ni aibu. Mbowe atavuna alichopanda.
 
Madai ya Lisu kuwa kuna pesa imepenyezwa kwenye uchaguzi wa Chadema ni kweli na Mbowe wala wapambe wake hawakukanusha.

Inawezekana hiyo ni sababu iliyomfanya Mbowe kung'ang'ania kugombea uenyekiti.

Vv
 

Kamwachia nani chama wakati yeye bado ni kiongozi katika chama?. Yeye bado ni mjumbe wa kamati kuu tena mjumbe wa kudumu. Bado ama wajibu wa kukitumikia chama, kukilinda chama, kukisaidia kikue zaidi.

Yeye anakisusia chama kife wakati anaona Dola inakiandama kila siku.

Huo ni usaliti kwa chama.
 
Kinachoniuma zaidi ni kwamba kuna wananchi walipoteza mali fedha viungo na maisha wakiipigania chadema bila kujua kuwa mbowe alikuwa ni kibaraka wa ccm
 
Mbowe ni msaliti na pandikizi lla ccm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…