SI KWELI Mbowe apiga picha ikiwa na chupa ya Konyagi nyuma yake

SI KWELI Mbowe apiga picha ikiwa na chupa ya Konyagi nyuma yake

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Habari Wakuu, nimekutana na picha ikimuonesha Mbowe amepiga picha mbele ya TV huku nyuma kukiwa na chupa ya Konyagi.

Je, picha hii ni halisi?

IMG_20240910_095643_639.jpg

---
1725980701772.png
 
Tunachokijua
Freeman Mbowe ni ni mwanasiasa maarufu nchini Tanzania. Yeye ni kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambacho ni chama kikuu cha upinzani nchini. Mbowe amewahi kuwa Mbunge wa Hai, Kilimanjaro, na pia ni mfanyabiashara.

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa picha iliyoletwa na Mdau wetu hapo juu ikimuonesha Freeman Mbowe Mwenyekiti akiwa na Mwanaye Dudley Mbowe imeanza kusambaa tangu Septemba 9, 2024 kupitia mtandao wa X kwenye akaunti mbalimbali zikiwemo hizi hapa, hapa, na hapa. Picha hiyo yanye pombe pembeni inasambaa ikiwa na ujumbe unaodai kuwa CHADEMA ni chama cha familia na Mbowe anataka kumrithisha Mwanaye (aliyenaye kwenye picha) cheo cha Uenyekiti wa CHADEMA. Taarifa hiyo inaeleza:

CHAIRMAN NA MPANGO WA KURITHISHA KITI KWA MWANAE Za ndaaaaaaani ni za Motooo! Mtoto wa Freeman Mbowe Bw. Dudley Mbowe ndiye anayetarajiwa kuchukua nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa! Kweli Tundu Antipas Lissu anahaki ya kususa! Chama kimekua cha Familia hiki.

Upi ukweli kuhusu picha hii?
JamiiCheck imefanya ufuatiliaji wa kimtandao na kubaini kuwa picha hii imehaririwa na kuongezwa chupa na kikombe sehemu ya pembeni upande aliosimama Mbowe.

Kupitia Google Reverse Search tumepata zaidi ya majibu 19 kufikia leo Septemba 10, 2024 saa 5:00 Asubuhi yote yakitokea Mtandao wa X (Zamani Twitter) huku majibu 15 yakionesha picha isiyo na chupa na kinywaji hicho na manne yakiwa na kinywaji (tazama majibu yote hapa).

Aidha, kupitia majibu hayo JamiiCheck imebaini kuwa picha hii iliwekwa mara ya kwanza kwenye Mtandao wa X kupitia Akaunti rasmi ya Dudley (Mtoto wa Mbowe) Septemba 5, 2024 na haikuwa na chupa ya pombe na kikombe nyuma kama inavyosambazwa (picha hiyo imehifadhiwa hapa).

1725956697524-png.3092272

Chapisho la kwanza la picha ya Mbowe na Dudley ikiwa haina kinywaji na kikombe sehemu ya TV​

Zaidi ya hayo, JamiiCheck imebaini kuwa tukio kama hili la Freeman Mbowe kuwekewa chupa ya pombe kwenye picha yake liliwahi kutokea mnamo February 1, 2023 na kuhakikiwa na JamiiCheck na tulibaini kuwa haikuwa na ukweli (Tazama hapa).
Konyagi ndo lengo tunaikubali sana mjomba hio kitu inalewesha ni mziki mnene japokuwa simkubali sana mbowe maana namzidi elimu ila konyagi haifai iwe kikwazo kwa wafuasi wake..me ni shabiki wa makonda na magufuli MILELE
 
Hata kama ni halisi shida iko wapi.

Mbona sijaona mna leta picha za screenshots za vipngozi wa ccm wakisema kauli za kuhimiza utekaji.
 
Habari Wakuu, nimekutana na picha ikimuonesha Mbowe amepiga picha mbele ya TV huku nyuma kukiwa na chupa ya Konyagi.

Je, picha hii ni halisi?

Hiyo picha ya chupa ya konyagi imebandikwa tu hapo yaani wamefanya editing maana hata uki zoom unaona hiyo chupa wamejaribu kui edit sana ile iwe ndogo ikae hapo kwenye meza na kuna rangi wamesahu kuiedit hapo ili iendane na rangi ya meza ya TV. Kuwa makini na wewe mlete uzi. Umaarufu hauji kwa kumsemea mtu vibaya humu mtandaoni. Uwe unatuliza akili kabla ya kupost au kumchafua mtu.
 
Kwani Mbowe akinywa hiyo konyagi kuna shida gani? mbona ushamba umekuwa mwingi sana kwenye hii jamii yetu?

Kwani nani aliwaambia Mbowe ni mchungaji au sheikh?!
 
Hakuna shida Hapo,Tena ukimpa ule msosi alipika mama Akasahau kuweka ndimu swaaaafi.
 
Back
Top Bottom