SI KWELI Mbowe apiga picha ikiwa na chupa ya Konyagi nyuma yake

SI KWELI Mbowe apiga picha ikiwa na chupa ya Konyagi nyuma yake

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Habari Wakuu, nimekutana na picha ikimuonesha Mbowe amepiga picha mbele ya TV huku nyuma kukiwa na chupa ya Konyagi.

Je, picha hii ni halisi?

IMG_20240910_095643_639.jpg

---
1725980701772.png
 
Tunachokijua
Freeman Mbowe ni ni mwanasiasa maarufu nchini Tanzania. Yeye ni kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambacho ni chama kikuu cha upinzani nchini. Mbowe amewahi kuwa Mbunge wa Hai, Kilimanjaro, na pia ni mfanyabiashara.

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa picha iliyoletwa na Mdau wetu hapo juu ikimuonesha Freeman Mbowe Mwenyekiti akiwa na Mwanaye Dudley Mbowe imeanza kusambaa tangu Septemba 9, 2024 kupitia mtandao wa X kwenye akaunti mbalimbali zikiwemo hizi hapa, hapa, na hapa. Picha hiyo yanye pombe pembeni inasambaa ikiwa na ujumbe unaodai kuwa CHADEMA ni chama cha familia na Mbowe anataka kumrithisha Mwanaye (aliyenaye kwenye picha) cheo cha Uenyekiti wa CHADEMA. Taarifa hiyo inaeleza:

CHAIRMAN NA MPANGO WA KURITHISHA KITI KWA MWANAE Za ndaaaaaaani ni za Motooo! Mtoto wa Freeman Mbowe Bw. Dudley Mbowe ndiye anayetarajiwa kuchukua nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa! Kweli Tundu Antipas Lissu anahaki ya kususa! Chama kimekua cha Familia hiki.

Upi ukweli kuhusu picha hii?
JamiiCheck imefanya ufuatiliaji wa kimtandao na kubaini kuwa picha hii imehaririwa na kuongezwa chupa na kikombe sehemu ya pembeni upande aliosimama Mbowe.

Kupitia Google Reverse Search tumepata zaidi ya majibu 19 kufikia leo Septemba 10, 2024 saa 5:00 Asubuhi yote yakitokea Mtandao wa X (Zamani Twitter) huku majibu 15 yakionesha picha isiyo na chupa na kinywaji hicho na manne yakiwa na kinywaji (tazama majibu yote hapa).

Aidha, kupitia majibu hayo JamiiCheck imebaini kuwa picha hii iliwekwa mara ya kwanza kwenye Mtandao wa X kupitia Akaunti rasmi ya Dudley (Mtoto wa Mbowe) Septemba 5, 2024 na haikuwa na chupa ya pombe na kikombe nyuma kama inavyosambazwa (picha hiyo imehifadhiwa hapa).

1725956697524-png.3092272

Chapisho la kwanza la picha ya Mbowe na Dudley ikiwa haina kinywaji na kikombe sehemu ya TV​

Zaidi ya hayo, JamiiCheck imebaini kuwa tukio kama hili la Freeman Mbowe kuwekewa chupa ya pombe kwenye picha yake liliwahi kutokea mnamo February 1, 2023 na kuhakikiwa na JamiiCheck na tulibaini kuwa haikuwa na ukweli (Tazama hapa).
Hizo ni spinning brother. Kuna wapuuzi wameua wanajitahidi kubadilisha upepo
Haya mazezeta yamekosa vitu muhimu vya kuongea yanabaki kufikiria ujinga tu, Treni inawashinda huko badala ya kumsaidia Rias yanahangaika na Mbowe
 
Kila uzushi unaoleta kuhusu Mbowe unakanushwa, kwamba wewe umepewa kitengo cha kumuongelea Mbowe tu?
Anakula mshahara TGSS 4 kwa kumzushia Mbowe kila siku.
ni kitengo kabisa na jumapili mtu anawahi kanisani kiti cha mbele kutoa zaka na sadaka na mchango kwa watoto yatima kwa fedhs za kumzushia Mbowe.
 
Kwa iyo mwandishi unahis unatuondoa kwenye kuwaza watekwaji,watesi na wauaji Kwa picha ya kijinga hiv,,hiv mccvu Huwa hamna hata mwenye akili nzur inayoweza kuwaza namna ya kiteka akili za watu? Sasa ujinga gan huu? Tatzo nyimbo za iyena iyena anayejua kuomba vzur ndo anapewa kua kiongoz,, sitakaa niwe mwanachama wa Chama chochote Kwa kwel !!!
 
We naye NYERERE Kuna picha anapiga kabisa bia na safi kabisa Kwan Kuna tabu kumwagilia moyo na kinywaji kinachokuburudisha.

Au ulitaka mpk zingekuwa brand za nje maarufu ndo ungefurahi
 
Anakula mshahara TGSS 4 kwa kumzushia Mbowe kila siku.
ni kitengo kabisa na jumapili mtu anawahi kanisani kiti cha mbele kutoa zaka na sadaka na mchango kwa watoto yatima kwa fedhs za kumzushia Mbowe.
Halafu kuna watu wanaamini hii nchi itapiga hatua kwa watu wa aina hii, Hata Mungu anashangaa haya majitu yamepewa kibali kabisa cha kufanya haya maujinga na akiongozi mkuu anatambua uwepo wao kabisa na anasimama kuomba tuliombee Tiafa na yeye mwenyewe
 
watu wasiokunywa bhana sasa nini cha ajabu..😂
kwanza lime editiwa mmetukosea sana ilitakiwa iwe yenyewe kabisa hiyo picha hutumii hata dk moja kujua kuwa imekuwa edited!.

point chupa ni nyeupe na konyagi ni nyeupe hivyo ingesababisha vilivyonyuma vionekane!,sasa hapo havionekani! kazi mbovu kwelikweli jinga kabisa.
 
Back
Top Bottom