SI KWELI PreGE2025 Mbowe apokelewa na kuteuliwa kugombea Urais kupitia Chaumma

SI KWELI PreGE2025 Mbowe apokelewa na kuteuliwa kugombea Urais kupitia Chaumma

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
TAARIFA KWA UMMA

UTAMBULISHO WA MGOMBEA URAIS WA CHAMA CHA HAKI NA MAENDELEO (CHAUMMA)

Dar es Salaam, 21 Mei 2025


Chama cha Haki na Maendeleo (CHAUMMA) kinapenda kuwataarifu wanachama wake, wapenzi wa chama, na umma kwa ujumla kuwa, katika kikao chake cha Kamati Kuu kilichofanyika tarehe 10 Mei 2025 jijini Dar es Salaam, uamuzi ulifikiwa kwa kauli moja kumteua Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama chetu katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Uteuzi huu ulithibitishwa na kuidhinishwa rasmi na Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa uliofanyika siku hiyo hiyo jijini Dar es Salaam, ambapo wajumbe wote walionesha imani kubwa kwa Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe kupeperusha bendera ya CHAUMMA katika nafasi ya juu kabisa ya uongozi wa nchi.

Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe ni mwanasiasa mwenye uzoefu mkubwa, uadilifu, na maono ya kuleta mabadiliko chanya kwa taifa letu. Uteuzi wake unaashiria dhamira ya CHAUMMA ya kuleta uongozi bora, unaojali maslahi ya wananchi, na wenye kujenga misingi imara ya haki, usawa, na maendeleo endelevu.

Chama kinatoa wito kwa wanachama wote, wapenzi wa chama, na wananchi kwa ujumla kuungana nasi katika kumuunga mkono Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe katika safari hii ya kuelekea Ikulu, kwa lengo la kuleta mabadiliko tunayoyatamani.

Tunaamini kuwa kwa pamoja, tutaweza kujenga Tanzania mpya yenye matumaini, haki, na maendeleo kwa wote.
IMG_20250521_213628_282.JPG
IMG_20250521_213642_950.JPG
 
Tunachokijua
Freeman Aikaeli Mbowe alikuwa mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) aliyemaliza muda wake mwaka 2025 baada ya kushindwa uchaguzi na Tundu Lissu ambaye ndiye mwenyekiti wa sasa.

Mara kwa mara Mbowe amekuwa akihusishwa na kuhamia chama kingine cha siasa na hii ni haswa baada ya waliokuwa wakimuunga mkono kuhamia CHAUMMA.

Madai

Kumekuwapo na grafiki mbalimbali zinazosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwa na picha ya aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo Taifa (CHADEMA) Freeman Mbowe amepokelwa kwa kishindo CHAUMMA na ametangazwa kuwania Urais.

Uhalisia wa madai hayo

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa madai hayo si ya kweli. Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao umebaini kuwa grafiki hizo zinazoonekana kuwa ni za Jambo TV na Millard Ayo hazijachapishwa katika kurasa rasmi za mitandao kijamii ya vyombo hivyo.

Grafiki hizo zina makosa kadhaa ikiwemo ya uandishi, mathalani kifupisho cha Chama cha ukombozi wa Umma ni 'CHAUMMA' lakini grafiki hizo zimeandikwa 'CHAUMA'. Ufuatiliaji zaidi umebainisha kuwa inayoonekana kuwa ni taarifa kwa Umma inayodaiwa kutolewa na CHAUMMA kuhusiana na tukio hilo haijatolewa wala kuchapishwa katika kurasa rasmi za chama hicho.

Mwenyekiti wa kanda ya Pwani, Boniface Jacob alipofanya mazungumzo na waandishi wa habari Mei 18, 2025 alieleza kuwa wanaohama CHADEMA wasitumie jina la Mbowe ili kuwashawishi wanachama kukihama chama hicho kwani Mbowe bado hajahama.

Akizungumza katika mkutano mkuu wa CHAUMMA Mei 21, 2025 Katibu mkuu Salumu Mwalimu alieleza watatangaza mikakati yao kuelekea uchaguzi mkuu kuanzia Mei 30, 2025 watakapoanza mikutano yao nchi nzima.
 
Itakua maajabu sana🤣
 
Usimuamini mwanasiasa ambae bado anapumua....🤣
 
I wonder if Tundu Lissu would have done the same if he had lost the CHADEMA election🤔
 
TAARIFA KWA UMMA

UTAMBULISHO WA MGOMBEA URAIS WA CHAMA CHA HAKI NA MAENDELEO (CHAUMMA)

Dar es Salaam, 21 Mei 2025


Chama cha Haki na Maendeleo (CHAUMMA) kinapenda kuwataarifu wanachama wake, wapenzi wa chama, na umma kwa ujumla kuwa, katika kikao chake cha Kamati Kuu kilichofanyika tarehe 10 Mei 2025 jijini Dar es Salaam, uamuzi ulifikiwa kwa kauli moja kumteua Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama chetu katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Uteuzi huu ulithibitishwa na kuidhinishwa rasmi na Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa uliofanyika siku hiyo hiyo jijini Dar es Salaam, ambapo wajumbe wote walionesha imani kubwa kwa Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe kupeperusha bendera ya CHAUMMA katika nafasi ya juu kabisa ya uongozi wa nchi.

Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe ni mwanasiasa mwenye uzoefu mkubwa, uadilifu, na maono ya kuleta mabadiliko chanya kwa taifa letu. Uteuzi wake unaashiria dhamira ya CHAUMMA ya kuleta uongozi bora, unaojali maslahi ya wananchi, na wenye kujenga misingi imara ya haki, usawa, na maendeleo endelevu.

Chama kinatoa wito kwa wanachama wote, wapenzi wa chama, na wananchi kwa ujumla kuungana nasi katika kumuunga mkono Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe katika safari hii ya kuelekea Ikulu, kwa lengo la kuleta mabadiliko tunayoyatamani.

Tunaamini kuwa kwa pamoja, tutaweza kujenga Tanzania mpya yenye matumaini, haki, na maendeleo kwa wote.
View attachment 3340940
This is fake news.
 
Back
Top Bottom