si busara mbowe kujiondoa sababu:lengo la chadema ni kuuonyesha umma kuwa hiki ni chama cha demokrasia hivyo kila mmoja ana nafasi ya kushiriki shughuli zote za kidemokraisa ikiwemo uchaguzi ,chadema endapo mbowe atalazimika kumruhusu lisu apite bila kupingwa CCm itakuwa imepata uhalali wa kuengua wagombea katika chaguzi mbali mbali za dola maana lisu atakuwa kama case study wakati yeye ndo tunamtegemea awe na nguvu ya kukemea hilo la kuenguana na kupita bila kupingwa,sasa basi mimi nachoona kama mbowe ana nia njema na chama,kwanza kabisa anapaswa kurusu uchaguzi uwe huru maana aache wajumbe wapige kura kwa nguvu ya ushawishi wa mgombea sio kwa kutuminia nguvu ya pesa hasa kwa upande wa wapiga kura wake maana kwa LiSU nguvu ya pesa hana na hata kama anayo hatafanya hivyo sababu sera yake katika uchaguzi huu ni kutokomeza rushwa ndani ya chama,pili mbowe atambue kwa kuwa ana nguvu ya wajumbe ambao ndio wapiga kura wake kwenye kinyang'anyiro cha kiti ,mwenzake ana nguvu ya wanachama wa kawaida ambao ndo wanakifanya chama kiwe chama kikuu cha upinzani kwa wingi wa wanachama na wapiga kura wengi ambao wanapokipigia kura hata kisipochukua dola ,kutokana na asilimia zilipatikana kinapata hata wabunge kadhaa na viti maalum,hivyo ushindi wa mbowe bila wanachama wengi chama ni mfu,na kama ccm ndio inafadhili katika hili pia baada ya ushindi wake basi akumbuke hatakuwa tishio tena itabakia amekamilisha malengo ya ccm ya kuiua chadema,ila akishinda kihalali basi umoja wa chama utakuwepo maana hakutakuwa na mpasuko zaidi ila kitakachotokea ni Lisu kubakia na mtaji wa watu wengi ambapo bado itakuwa tishio kwa mbowe japo atakuwa nguvu ya maamuzi katika chama lakini atakuwa anaulizia maoni ya lisu kuhusu hilo jambo ,na akisema amfukuze katika chama napo muyumbo wa chama hauwepukiki,japo wana msemo kuwa chama ni imara kuliko mtu lakini tumeona watu wenye ushawishi walivyofukuzwa chadema ya miaka hiyo haiko kama ilivyokuwa maana hata nguvu ya kumobilize mji kwa ajili ya maandamano haipo tena, hivyo ni, imani yangu kama hakutakuwa na maelewano baada ya uchaguzi huu basi chadema ,itaindokewa kuwa chama kikuu cha upinzani hatimae nakubakiwa kuwa chama chenye usajili wa kudumu basi.