Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na akiwa Afrika ya Kusini, Mbowe Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Vyama vya Demokrasia Afrika (DUA), ametoa wito huo nchini Afrika Kusini, akifungua kongamano la kujadili usalama na ulinzi, demokrasia na biashara barani humo, lilikoandaliwa na DUA.
Mbowe amesema idadi ya watu wa Afrika haijatumika vyema kuwa mtaji wa kusukuma maendeleo, badala yake imekuwa mzigo kwa maendeleo ya watu na bara Hilo.
Aidha, Mbowe amezitaka vyama wanachama wa DUA kuweka mikakati ya kutumia rasilimali ardhi ya Afrika kuleta maendeleo.Amesema Afrika inapaswa kuendeleza watu wake kuwa rasilimali ambayo ni bora kuliko maliasili inayoweza kupatikana.
popote.
“Mtazamo wangu ndugu washiriki ni kwamba, kama tunataka kulibadilisha bara letu, lazima tufikiri na kujikita katika kuwaelimisha watu wetu na si pungufu ya hapo,” amesema Mbowe na kuongeza:
“Ulaya na Amerika wana watu wachache lakini wao ndiyo mihimili ya dunia kwa sababu ya mtaji wa rasilimali watu.”