*MBOWE ATOBOA MTUMBWI,
UTANGULIZI
Hatimaye ile habari iliyosubiriwa kwa kiu kubwa, imefikia tamati leo kwa Mwenyekiti Mbowe kutanganza kugombea Uenyekiti Chadema Taifa. Hii ni baada ya Lissu kutanganza na kuchukua form siku kadhaa zilizopita.
Naaam.!
Vyombo vya Habari kwa siku ya leo, vimepambwa na uamuzi wa Mh Mbowe kugombea, na hivi kuingia rasmi katika mchuano ambao unatazamiwa kuwa mkali dhidi ya rafiki na ‘mdogo’ wake Mh Tundu Lissu.
Jambo hili limekuwa na mapokeo tofauti sana, kwa makundi mbalimbali ya watu: Wanasiasa, Wanachama, Wapenzi na Wananchi wa kawaida.
Kwa upande wa Wanasiasa wamegawanyika pia, wapo wanaomuunga mkono Mbowe na wengine Lissu. Vile vile kwa Wanachama na Wananchi. Makundi haya yameonesha hisia zao sirini na hadharani, juu ya mtu wampendao.
Lakini, watu kadhaa maarufu walijaribu kuweka ‘polls’ za mtandaoni, karibia kura zote za mitandaoni, zilimuonesha Lissu kuwa ndiye anayefaa kukalia kiti hiko kwa sasa. Sababu kubwa ikiwa aina ya siasa za sasa na ‘intergirty’ au uadilifu wa Lissu katika Siasa dhidi ya Mwenyekiti wake Mbowe.
Wengine wakaenda mbali zaidi kusema, kama kweli Chadema (Mbowe) ni Mwanamageuzi, atamuachia mwenzake aongeze, ikizingatiwa kuwa yeye ameongoza kwa miaka zaidi ya 20.
Lakini hisia zote hizi, zikafutika ghafla na tangazo la Mbowe kuwa anagombea, huku akiwa na nguvu, ari na shauku kubwa kabisa.
Wadadisi wa mambo wanaona kuwa hatua hii, ndio mwanzo wa mwisho wa Chadema, kuwa Chama Kikuu cha Upinzani, kwa kuwa katika Uchaguzi huo, wanaona ni wazi kabisa Mbowe atashinda kutokana na political technics ambazo Mbowe ana advantage nazo toka mwanzo.
Kama hali ndivyo ilivyo, Wadadisi wanauliza, ni kwanini Lissu aamue kumvaa Mbowe ilihali anajua uwezekano wa kushinda ni mdogo? Pia alishatanganza kugombea Umakamu, ni nini kimembadilika? Je, anatafuta exit door au? Na ataelekea wapi?? Chama Kipya? Atafanikiwa achilia mbali kukubaliwa kukianzisha??
Zipo tetesi kuwa, Mh Lissu aliamua ku ‘change gear’ angani kwa sababu kuna mpango ulikua wa kumtoa kwenye system (nafasi yake ya Umakamu) na kundi la watu aliowatuhumu kwa makosa ya rushwa ndani ya chama. Na akaona kuwa kundi hilo ni kama lina support ya Mwenyekiti wake.
Swala hili linapata nguvu kwasababu ni kweli kuwa mmoja wa watu hao waliotuhumiwa nae, alichukua form ya kugombea nafasi ya Lissu. Je, ina maana Mh Lissu anaogopa Uchaguzi? Au anajua usingekuwa wa Haki? Je, anaamini Uchaguzi wa Mwenyekiti Taifa utakua wa Haki? Kama sivyo, ni kwanini aamue kugombea?
Mh. Lissu akiwa yupo aware kuwa, kwa kugombea kwao wawili kunaenda kukipasua Chama, ina maana Lissu haoni kuwa atakosa platform ya kufanya mageuzi? Ana plan gani? Ni kwanini ameamua kugombea?
Muundo wa swali kama hilo pia linamuhusu Mbowe. Kama kweli yeye ni Mwanamapinduzi, aliyekijenga chama kwa zaidi ya miaka 20, pasipo kushika Dola, ni kqanini asione Lissu ambaye anaonesha kuungwa mkono ndani na nje ya chama, kuwa ni kete yake turufu ya kutimiza ndoto yake na ya chama, ya kushika Dola??
Ni kwanini Mbowe alivuta gape ya siku mbili only kuja kusema kuwa anaendelea na kugombea? Wadadisi wanahoji kuwa imekuaje Mbowe kwa miaka yote hii ya maandalizi ya Uchaguzi hakujua kuwa atagombea au la? Ndani ya siku mbili hizi, alikua anafanya tathmini gani zaidi? Amesikiliza uahauri wa nani?
Ni nini hatima ya Chadema sasa? Je ndio kinajizika au kimezikwa? Kwanini mambo haya yatokee kuelekea Uchaguzi Mkuu? Kwanini watu wa nje ya Chadema wahusishwe?
Kwa Wapenzi wa Demokrasia, hawafurahii sana kifo na mwisho mbaya hivi wa CDM, kwasababu CDM ni sehemu mbadala na rasmi ya Wananchi kutoa maoni yao pasipo kutumia njia haramu za haki zao za Kisiasa. Huenda kukaibuka chama kipya au kingine chenye jukwaa pana na huru kama ilivyo kwa CDM hivi sasa. Huenda pia kusiibuke chama hicho, je Serikali imejipanga vipi ku accomodate maoni na mitazamo kinzani ya Wananchi wasiokubaliana na mawazo ya vyama vingine au na Serikali?
Yote kwa yote….katika hii Vita, kama Mbowe atashinda, nionanvyo mimi, Mbowe bado atakua ndiye Looser, kwa sababu reputation yake itashuka, intergrity ya Lissu imekua kubwa kumzidi, na hivi inaharibu heshima na uaminifu wa Mbowe na Chadema ambayo imejengeka kwa muda mrefu. Na hivi Chadema itapungua umaarufu na kubakia kama vyama vingine vilivyowahi kuwika—CUF, TLP nk.
Wasalaaam.!
Apiov S Lwiwa, PhD.
Email: apiovlwiwa@gmail.com