Pre GE2025 Mbowe: Chama chetu hakina ukomo wa Madaraka na msitulazimishe kuwa kama CCM ama Act Wazalendo wenye ukomo wa Madaraka kwa viongozi

Pre GE2025 Mbowe: Chama chetu hakina ukomo wa Madaraka na msitulazimishe kuwa kama CCM ama Act Wazalendo wenye ukomo wa Madaraka kwa viongozi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
4,942
Reaction score
20,077
Mwenyekiti wa Chadema bwana Mbowe amesema chama chao cha chadema hakina ukomo wa madaraka na watu wasiwalazimishe kua kama CCM ana ACT wazalendo wenye ukomo wa Madaraka.

Mbowe anasema ukomo wa madaraka kwenye chama chao ni pale wanapofanya uchaguzi kila baada ya miaka 5 hivyo kama kiongozi anachaguliwa tena kwenye kila uchaguzi hilo halina shida ila kama wanachama watamkataa basi huo ndio ukomo wake unakua umefika.

Mbowe anasema chadema wasilazimishwe kua kama ccm ama act kuweka ukomo ama term limit ya viongozi, kiongozi atawale hadi pale wananchi watakapomchoka wenyewe.
 
Wanaotaka ukomo wa madaraka wanataka uwe miaka mingapi?
Miaka 3, 5, 7, 10, 15, 20, 25 au 30??
 
Wanaotaka ukomo wa madaraka wanataka uwe miaka mingapi?
Miaka 3, 5, 7, 10, 15, 20, 25 au 30??
Kama kiongozi hawezi kukamilisha Agenda zake muhimu ndani ya miaka 10, huyo hana vision na hata ukimpa miaka 25 hatofanya chochote

Kuna sababu kwanini “term limits” huwa zinawekwa na Mzee Mbowe anataka kutafsiri vibaya maana ya ukomo wa uongozi kwa sababu ana intetest kubwa
 
Mbona Urusi hakuna term limits??

Mbona mpaka 2008 Ufaransa haikuwa na term limits??

Mbona Canada, Ujerumani, Uingereza, India na Italia hakuna term limits?
 
Mbowe upo sahihi 100%. Hata CCM huwa hawachagui Mwenyekiti wao bali wanaletewa jina moja lililopendekezwa na watu wachache kisha mkutano mkuu unalipitisha - mbona sisi wananchi hatujawahi kusema kwamba hiyo siyo demokradia huru.
 
Back
Top Bottom