Pre GE2025 Mbowe: Chama chetu hakina ukomo wa Madaraka na msitulazimishe kuwa kama CCM ama Act Wazalendo wenye ukomo wa Madaraka kwa viongozi

Pre GE2025 Mbowe: Chama chetu hakina ukomo wa Madaraka na msitulazimishe kuwa kama CCM ama Act Wazalendo wenye ukomo wa Madaraka kwa viongozi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mwenyekiti wa Chadema bwana Mbowe amesema chama chao cha chadema hakina ukomo wa madaraka na watu wasiwalazimishe kua kama CCM ana ACT wazalendo wenye ukomo wa Madaraka.

Mbowe anasema ukomo wa madaraka kwenye chama chao ni pale wanapofanya uchaguzi kila baada ya miaka 5 hivyo kama kiongozi anachaguliwa tena kwenye kila uchaguzi hilo halina shida ila kama wanachama watamkataa basi huo ndio ukomo wake unakua umefika.

Mbowe anasema chadema wasilazimishwe kua kama ccm ama act kuweka ukomo ama term limit ya viongozi, kiongozi atawale hadi pale wananchi watakapomchoka wenyewe.

View: https://www.instagram.com/p/DEZq5LeuFlW/?igsh=MTl4ZmRpYTZtY2pzcA==

Mbowe ashauliwe sio kila kitu cha kuongea kwa sasa kuna vitu anaviongea sasa vinafifisha harakati zake alizopigani miaka mingi iliyopita.

Kwaheshima apumzike tu awaachie wengingine.
 
Mfano Mbowe angejibiwa: NCHI YETU SIYO LAZIMA IWE NA KATIBA MPYA,MSITULAZIMISHE TUFANANE NA KENYA , sijui angekuwa kwenye hali gani muda huu
Huo ni uvivu wa kufikiri. Anashindwa kujua kama tunatakiwa kujilinganisha na standards na sio mtu. Mfano yeye anatoa hoja gani ya kutokuwa na ukomo au just msitulinganishe tu
 
M
Mbowe upo sahihi 100%. Hata CCM huwa hawachagui Mwenyekiti wao bali wanaletewa jina moja lililopendekezwa na watu wachache kisha mkutano mkuu unalipitisha - mbona sisi wananchi hatujawahi kusema kwamba hiyo siyo demokradia huru.
Mbowe ameshachokwa na wanachadema huku site.
Wanaona hana mapya kwa sasa.
Hao wajumbe anaojisifia wanamuunga mkono ni 0.0001 % ya wanachama wote.
 
Mwenyekiti wa Chadema bwana Mbowe amesema chama chao cha chadema hakina ukomo wa madaraka na watu wasiwalazimishe kua kama CCM ana ACT wazalendo wenye ukomo wa Madaraka.

Mbowe anasema ukomo wa madaraka kwenye chama chao ni pale wanapofanya uchaguzi kila baada ya miaka 5 hivyo kama kiongozi anachaguliwa tena kwenye kila uchaguzi hilo halina shida ila kama wanachama watamkataa basi huo ndio ukomo wake unakua umefika.

Mbowe anasema chadema wasilazimishwe kua kama ccm ama act kuweka ukomo ama term limit ya viongozi, kiongozi atawale hadi pale wananchi watakapomchoka wenyewe.

View: https://www.instagram.com/p/DEZq5LeuFlW/?igsh=MTl4ZmRpYTZtY2pzcA==

CCM hawana ukomo wa kugombea nafasi ya uongozi.

Amandla...
 
Mbona Urusi hakuna term limits??

Mbona mpaka 2008 Ufaransa haikuwa na term limits??

Mbona Canada, Ujerumani, Uingereza, India na Italia hakuna term limits?
Mbona ujerumani wanaume wanaolewa, vipi nije nikuchumbie ?
 
Toka ccm waanze kubadilisha mwenyekiti ufisadi umekwisha, ubaguzi umekwisha..ni ujuha kukariri mambo bila kuelewa matokeo yake kwa jamii..
Ndugu yangu wewe na yeye ni aina ya watu wanaokiuka makubaliano na kubadilisha maana ya jambo mpaka mnaharibu
Ukiambiwa kuku atage wewe unakataa na kusema azae
Mwisho wa siku kuku anachanika msamba
 
Kama kiongozi hawezi kukamilisha Agenda zake muhimu ndani ya miaka 10, huyo hana vision na hata ukimpa miaka 25 hatofanya chochote

Kuna sababu kwanini “term limits” huwa zinawekwa na Mzee Mbowe anataka kutafsiri vibaya maana ya ukomo wa uongozi kwa sababu ana intetest kubwa
Wajumbe wa CDM ,wanawajibu mkubwa wa wakuokoa chama kutoka mikono yaMbowe namuheshimu ila umetosha Kwa siasa ya sahivi nchini Tundu lissu anafaa kuongoza CDM apate safi ya Heche, Lema etc
 
Mbowe namkubali sana, lakini pia sioni kama Lisu anatosha kuwa kiongozi mkuu wa chama.
Lakini kwa hili.....
Bowe ameonyesha Ulafi wa madaraka... Bladi hell...🤨
Sasa wajumbe wapige kura kwa LISU........ndio utakuwa mwisho wa MBOWE...........tutaendelea kulalamika kwenye mitandao bila kupata jibu kama wajumbe watamchagua tena MBOWE. 😀 😀
 
Huyu ndo alikua namba moja kumsakama Magufuli kwenye masuala ya ukomo wa madaraka aiseee
Amesahau tayari,term limits ni muhimu sana tuna avoid Strong personality au one man army , kwenye demokrasia kitu kinacho matter ni strong institution, ni makosa sana kuacha mtu Mmoja tu hata awe genius kiasi kuwa kiongozi muda mrefu atatapata temptation tu za entitlement kujisahau kupo, thus why Mbowe keshaona CMD ni yeye ni chama chake haimbiliki. Hapa ni jambo mawili tu Tundu lissu ashinde chama kiendelee au Mbowe ashinde azame na chama chake watanzania wengi hawatakuwa na Trust Tena na CDM chini ya Mbowe ,kiufupi Mbowe kaegeuka kuwa M7 wa Uganda Madaraka matamu
 
Kweli kabisa ukomo ni relative term, kama mtu bado anafaa achaguliwe jambo muhimu sana uchaguzi uwe huru na haki
 
Ni ujinga kuendeleza lawama kwa Mbowe na Chadema kuhusu mambo yao ya uchaguzi wa ndani wakati ccm imeiingiza nchi kwenye ufukara, madeni na kukosa uzalendo na bado wanaharibu..hivi damages za chadema unaweza linganisha na damages walizofanya ccm kwa nchi?
 
Mbona Urusi hakuna term limits??

Mbona mpaka 2008 Ufaransa haikuwa na term limits??

Mbona Canada, Ujerumani, Uingereza, India na Italia hakuna term limits?
“Bado wanachama wengi wananitaka niendelee….”, forgetting kwamba kuna nyomi kubwa ya watu isiyo na kadi za chama ila inasupport just leadership

IMG_6055.jpeg
 
Back
Top Bottom