Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Mbowe leo amemshangaza karibia kila mtu mwenye uwezo wa kutafakari.
Mbowe ametumia muda mrefu sana kusifia mafanikio yaliyotokana na mwafaka uliofanywa kati yake na Rais Samia. Hakuthubutu kuzungumzia chochote kuhusiana na utekaji na mauaji ya viongozi na wanachama wa CHADEMA. Kwake yeye, baada ya mwafaka alioufanya na Samia, mambo ni safi. Mambo ya utekaji na mauaji ya wanachama na viongozi wa CHADEMA, yote yametokea baada ya mwafaka wa Mbowe na Rais Samia. Kwake vifo vya hawa wananchi waliokuwa wanatimiza haki yao ya kikatiba ya kutoa maoni na kuwakosoa watawala, siyo tatizo!! Mwafaka, kwa kadiri ya maelezo yake, umeleta faida nyingi. Kasoro ni ndogo ndogo kama vile uharibifu wa uchaguzi wa serikali za mitaa, lakini utekaji na mauaji ya wanachama wa chama chake, siyo tatizo!!
Nawapa pole sana familia zilizopoteza wapendwa wao walioamini wanapigania haki, kumbe kiongozi wao amekwisharidhika na yanayoendelea. Huenda hawakujua malengo ya kiongozi wao juu ya uwepo wa CHADEMA.
Kama Mbowe atakuwa Mwenyekiti tena, vijana jitafakarini sana, maisha na damu zenu isiwe burgaining power ya viongozi wa CHADEMA, kupata zaidi kutoka kwa watawala. Kwa namna CHADEMA inavyoenda, ni aheri ukabakia bila chama.
Kwa maelezo ya Mbowe, ni dhahiri kuwa ameridhika sana kuiona CHADEMA ilipofikia, anachosubiria ni apate wabunge wachache, na kura kidogo za Urais ili ruzuku isikatike. Na huenda hayo ndiyo malengo yanayokusudiwa kwa sasa.
Watu wasitarajie Kama Mbowe atakuwa mwenyekiti tena kwa miaka 5, wala wanachama wasitarajie kuwa eti atafanya makubwa katika kupigania haki. Kama ameshindwa kufanya kwa miaka zaidi ya 20, ni nini alicho nacho ndani ya miaka mitano kitakachoibadilisha CHADEMA? Labda kuining'iniza ifikie kule iliko NCCR.
Kumtarajia Mbowe afanye maajabu ndani ya miaka mitano, ni sawa na mfanyakazi anayeamini atakuwa tajiri jwa kulipwa kiinua mgongo toka NSSF. Kama mshahara wa 80% haukukufanya uwe tajiri muda wote ukiwa akazini, itawezekana vipi mchango wa NSSF wa 20% (10% toka kwenye mshahara wako, na 10% toka kwa mwajiri) itakufanya uwe tajiri?
Tujipe pole wote tuliokuwa tumeweka matumaini makubwa kwa CHADEMA.