Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Mbowe anaweza kulaumiwa kwa mambo yote lakini jambo moja kubwa ambalo hawezi kulaumiwa nalo ni kung'ang'ania au kukaa madarakani muda mrefu. Lissu mwenyewe ambaye ndiye mpinzani mkuu wa Mbowe katika nafasi ya mwenyeketi kwa sasa na anayetaka ukomo wa kushika madaraka ndani ya CHADEMA uwekwe anasema alishiriki kikamilifu kupendekeza na katika maamuzi ya kuondoa ukomo wa uongozi ndani ya CHADEMA mwaka 2006 kwa sababu ya uchanga wa chama na ukosefu wa viongozi wa kutosha katika kugombea na kushika nafasi za uongozi ndani ya CHADEMA.
Mara zote ambazo Mbowe amegombea uenyekiti wa CHADEMA hakujawahi kuwa na washindani wa maana kumpa changamoto katika uchaguzi. Lissu anasema Zitto, Kitilia na Chacha Wangwe(ambao waliwahi kuonekana kama wangempa changamoto) walikuwa wanataka kufanya mapinduzi ya uongozi ndani ya chama badala ya kufuata taratibu rasmi za wazi za chama za uchaguzi kama anavyofanya yeye sasa