Mbowe: Hatuna ndoa na CCM. CCM ni mahasimu wetu, hawatuamini na sisi hatuwaamini

Mbowe: Hatuna ndoa na CCM. CCM ni mahasimu wetu, hawatuamini na sisi hatuwaamini

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Screenshot 2023-07-14 160431.png

Mbowe amesema hayo katika mkutano wa CHADEMA na Waandishi wa Habari juu ya Maazimio ya Kamati Kuu juu ya DP World leo tarehe 14/7/2023, akiwa anajibu kuhusu CHADEMA kuwa mezani na CCM, akasema;

Russia na Ukraine vita vinaendelea huku mazungumzo juu ya namna ya kumaliza vita yanaendelea, maana yake ni kwamba mazungumzo ni lazima.

Akiendelea kuwa, Mazungumzo ya CHADEMA na CCM hayatakaa yazime koleo na ukali wa CHADEMA katika kutetea maslahi ya nchi. Nayeyote aliyekuwa anasema CHADEMA iko kwenye ndoa na CCM hilo sio kweli.

Akisema, "CCM hao ni maasimu wetu, tunawaangalia wakati wote kama maasimu wetu, hawatuamini na sisi hatuwaamini, lakini ni ushirika ambao ni lazima ufanyike ili tuitafute hatma nzuri ya nchi yetu."

Pia soma: Freeman Mbowe: Tunazindua "Operation +255 Katiba Mpya Okoa Bandari Zetu" kuwaambia watanzania ubaya wa Mkataba wa DP World
 
Kila mtu anaitaka Dola, kubaki na kuingia, hakuna urafiki zaidi ya kuviziana
 
CDM inaridhiana na wanaouza bandari zetu!!!

Kuna urafiki Gani kati ya Giza na Nuru?
 
Back
Top Bottom