Mbowe hawezi kupambana na matakwa ya muda

Li ngunda ngali

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2023
Posts
707
Reaction score
2,572
Muda huwa ni Mwalimu sahihi kwa lolote jambo, Mfalme mpya bwana Mbowe yampasa atambue.

Bwana Mbowe anaweza kuhonga pesa kwa wapambe akidhani atabadiri upepo umtakao aondoke.

Bwana Mbowe anaweza kuahidi vyeo kwa vyawa wake ili kwa kujidanganya huenda watampigania ili labda ile kukubalika kwake kama zamani kutarejea, pengine.

Yote hayo hayatawezekana tena bwana Mbowe atambue.

Bwana Mbowe asichokielewa pengine ni kwamba wakati na matamanio ya watu kwake hayapo upande wake tena!

Ni wazi yapo mengi mazuri amefanya, lakini nyakati sizo za upande wake.

Hayupo na hatakuwepo awaye wa kupata kushindana na matamanio ya watu kwa muda watakawo.
 
Sidhani kama mbowe hayajui haya isipokuwa kitu pekee anachokitegemea kushinda uchaguzi ni backup ya CHAMA na serikali.
 
Mbowe akishinda huu uchaguzi, maana yake CHADEMA inaenda kufa.

Mbowe angekuwa kocha wa timu ya mpira tungesema amepoteza ushawishi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
 
Muda huwa ni Mwalimu sahihi kwa lolote jambo, Mfalme mpya bwana Mbowe yampasa atambue.

Bwana Mbowe anaweza kuhonga pesa kwa wapambe akidhani atabadiri upepo umtakao aondoke.

Bwana Mbowe anaweza kuahidi vyeo kwa vyawa wake ili kwa kujidanganya huenda watampigania ili labda ile kukubalika kwake kama zamani kutarejea, pengine.

Yote hayo hayatawezekana tena bwana Mbowe atambue.

Bwana Mbowe asichokielewa pengine ni kwamba wakati na matamanio ya watu kwake hayapo upande wake tena!

Ni wazi yapo mengi mazuri amefanya, lakini nyakati sizo za upande wake.

Hayupo na hatakuwepo awaye wa kupata kushindana na matamanio ya watu kwa muda watakawo.
Nikuulize swali? Na je nikiuliza utalijibu?
 
Umenena vyema,

CCM wasilazimishe kutuletea mgombea asiyekubalika na wananchi 2025.
 
Back
Top Bottom