Nyie chawa wa mama iwe ni Mbowe au Lissu mtahaha tu siku zote na uchawa hautawaisha.
Ndugu zangu Watanzania,
Kwa hakika Mheshimiwa Freeman Mbowe Mwamba na Jabali la Siasa za Upinzani katika ukanda huu wa Afrika Mashariki aliyekwepa mishale mingi kama Mbayuwayu Anapendwa na wana CHADEMA,huyu Mwamba anakubalika,anaaminika na wana CHADEMA sijapata kuona.
Huyu Mwamba Anapendwa na wana CHADEMA utafikiri Amewalisha Dawa.Nimeshuhudia kwa macho yangu wana CHADEMA wakibubujikwa na Machozi ya furaha utafikiri Wamekamuliwa Vitunguu Vibichi Machoni.Huyu Mwamba muacheni tu kama alivyo .
Ni kipenzi cha wana CHADEMA .Ukiona mtu mzima anabubujikwa na kutokwa na machozi ya furaha kwa sababu ya kumuunga mkono mtu basi ujue huyo mtu amegusa sana Maisha ya watu na kuteka hisia zao.
Wengi nilipojaribu kuwauliza sababu za wao kufikia hatua ya kushindwa kujizuia hisia zao na kujikuta wakibubujikwa na machozi.wamenieleza ni imani kubwa na upendo mkubwa walionao kwa Mwamba .wanasema Mwamba Amekitoa chama mbali sana,amekipigania kwa jasho na Damu.amepoteza na kutumia mali yake binafsi na rasilimali zake kwa ajili ya kuijenga CHADEMA mpaka kufikia kuwa chama kikuu cha upinzani na Chenye kuungwa mkono na wasomi hususani vijana.
Wanasema kuwa ni Mwamba Mbowe ndiye aliyeipatia umaarufu chadema mpaka kufikia kuanza kutamkika katika midomo na vinywa vya watanzania. Wanasema Mwamba ni mtu aliyekuza na kulea vijana wengi sana ambao baadaye wakaaminika kwa wananchi na kupewa nafasi za ubunge na udiwani na wengine walipoenda CCM wakapewa hadi uwaziri na wengine ukuu wa wilaya .wanasema hao wote wamepita mikononi mwa Mwamba Mwenyewe.
Wanasema Mwamba Amekuwa ni mtu Makini ,mtulivu, mnyenyekevu na kwenye subira na uvumilivu mkubwa sana katika kuijenga CHADEMA mpaka kufikia kuwa chama cha pili kwa ukubwa hapa Nchini baada ya CCM. Wanasema Mwamba hajawahi kuwaacha katika mapambano wala kukimbia mapambano au vita na kwenda kujificha kwenye balozi za kigeni au nje ya Nchi kama ambavyo wamekuwa wakifanya watu kama lissu.
Wanasema Mwamba ni kama Amekula kiapo kisichovunjika cha kuipigania CHADEMA Mpaka tone Lake la Mwiho la Jasho .Wanasema Mwamba amekaa Mahabusu kuliko pengine mwingine yeyote yule lakini bado hajawahi kukata tamaa wala kurudi nyuma katika kuijenga na kuipigania CHADEMA.
Wanasema Mwamba amepita katika kila aina ya majaribu lakini amebakia kuwa imara na Mwenye msimamo usio yumba wala kutetereka .Amekuwa ni Mbowe mwenye Maono na dira yenye kueleweka.Wanasema wangekata sana tamaa ikiwa chama kingekwenda mikononi Mwa mtu asiye na uchungu na chama.Wanasema Mwamba ameumia ,kuteseka na kupoteza vitu vingi sana kwa ajili ya CHADEMA.wanasema CHADEMA ipo kwa sababu ya jasho na Damu ya Mbowe.ni kwa kuwa Mwamba Amekubali kutumia Maisha yake kwa ajili ya CHADEMA.
Nami nawaunga mkono wana CHADEMA kuwa ni muhimu sana kumpigia kampeni Mwamba na kuja kumpa kura nyingi za ndio na za kishindo zitakazo itetemesha Dunia nzima ili kumpa moyo na faraja kwa kazi nzito ambayo amekuwa akiifanya kwa ajili ya CHADEMA.Mwamba ndio mboni ya CHADEMA na Nembo ya CHADEMA.Bila Mwamba hakuna CHADEMA na wala haitakuwepo hapa Nchini.
Mwamba akiachia ngazi hata kwa wiki moja tu basi chama kitabakia kipo vipande vipande utafikiri gari lililogonga Mwamba.Acheni Mwamba aendelee kuiongoza CHADEMA.achaneni na yule anayefikiri kuongoza chama kunahitaji uropokaji,kuzusha uongo,Mihemuko na kuongea kwa jazba na mahasira .Mwamba ni Mchungaji Mwema .Ni kiongozi kiasili aliyezaliwa akiwa na kibali cha uongozi mkononi pake.View attachment 3181896
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.