Mbowe kuachiwa Huru: Leo mshitaki, mshitakiwa na refa, wote wanasherehekea

Mbowe kuachiwa Huru: Leo mshitaki, mshitakiwa na refa, wote wanasherehekea

Michezo ya kisiasa huwa iko complex kiasi kwamba huzalisha conspiracies nyingi. Kwa bahati mbaya na kwa heshma ya msemo wa "the majority are always not right" huwa tunaangalia kile tu tunaona(patent).

Mi kwa mtazamo wangu

1. Serkali na CCM kama chama tawala ndo washindi No moja katika sakata hili maana wameweza kuzima joto la baada ya uchaguzi wa 2020 kwa namna ulivyofanyika.

Pia wakazima vuguvugu la katiba mpya wakat wa kipindi kigumu cha mpito kwa rais aliyeko madarakan. Na zaidi morale ya kudai katiba mpya iko chini, ongezea na hali ya wananchi tulivyo hoi kifikra na kiuchumi.

Itafika 2025 hakuna hata kiraka cha katiba mpya wala katiba yenyewe. CCM wameshapata uhakikisho wa kuendesha nchi na chaguz kwa namna ile ile. Kiufup ccm wamei "contain" nchi kwa ufanis mkubwa. Alichoanzisha sabaya na uncle magu kimewalipa!
Pia kelele za ndan na nje dhidi ya serkali na chama zitapoa. Mission accomplished!

2. Mshindi wa pili ni waliokuwa ndan. Mzee Mbowe na wenzake. Wamepewa uhuru wao kujumuika na familia zao na jamii.
HATA HIVYO KUPEWA UNACHOSTAHILI SI KUPATA! Kisheria mawakili wameifanya kaz yao vzuri.

Hata hivyo nahis walikuwa wakipambana kupiga deadsnake! Wakijua Mbowe anatakiwa kushinda kesi na upande wa 2 wakijua mbowe alitakiwa kufungwa gavana ya kisiasa kwa muda flan ambao ulishatosha!

3. Mshindi wa tatu ni jaji na timu yake kimahakama. Hii kesi ilikuwa kubwa kwa sababu ya jamii na wahusika. Hukumu ya jaji huyu ilikuwa au jaji maarufu katika kutoa haki au awe jaji wa ovyo katika historia.

Ni kesi yenye precedent muhim. Kesi kuishia hajaihukum amepumua na posho kashakula ya kutosha. Amemaliza vizuri. Kama angefikishwa mwisho huenda angepatwa na stress za kunawa mikono mtu asulubiwe!

Kwahiyo kila upande unasherehekea kwa namna yake! Kila upande una ushindi mkononi.

Mbona rasimu ya katiba mpya ipo inasubiri kupigiwa kura?. Na ilizunduliwa na Rais kiwete kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma 2014. Sema imekuwa ngumu kutokana na kutoungwa mkono na makundi mengi.
 
Mbona rasimu ya katiba mpya ipo inasubiri kupigiwa kura?. Na ilizunduliwa na Rais kiwete kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma 2014. Sema imekuwa ngumu kutokana na kutoungwa mkono na makundi mengi.
Rasimu ile inasaidia tu kutukumbusha tulishahitaji katiba mpya lakin si rasimu ya katiba tunayohitaji maana ilichakachuliwa. Huenda tukaruka mkojo kukakanyaga mavi! Ila kiukweli kwa sasa bora tuweke kiraka cha tume huru ya uchaguz, na kupinga matokeo ya urais. Ili tupate viongoz bora watupe mwelekeo wa mchakato wa katiba bora. Hata mzee wangu mkwere aliendesha zoez la katiba kisanii. Hadi ikazaliwa ukawa
 
kwakweli nimeshangaa sana yaani hali duni kwa wananchi ndio raha yao eti...hahahahah kwakweli watz tuna safari ndefu
Ccm ni washinde KWA kuwa wamezuia katiba mpya?? Dah hii hatari Sana

Ccm wameicontain nchi kwa kuwafanya watu masikini zaidi ? Sawa bana

Munga ataingilia kati
 
Kwan huko kitaa unakoishi umejitoa wapi! Ulipo ndo unapopaswa kuwa. Jaji yupo kwenye ujaji ndiko anapopaswa kuwa. Mengine ni changamoto tu za kaz. Maisha ya kujifanya mshumaa waachie wasio na cha kupoteza. Serkali sio zumarad. Unaweza kujitoa na bado kitaa usiishi!
Njaaa mbaya Sana
 
Back
Top Bottom