Uchaguzi 2020 Mbowe kugombea urais 2020 kupitia CHADEMA?

Uchaguzi 2020 Mbowe kugombea urais 2020 kupitia CHADEMA?

Chifyono

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2017
Posts
921
Reaction score
1,659
Habari wanaJF

Itakapofika October 2020 nchi itajihusisha na uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania

kwa upande wa CCM kama katiba yao unavyojinadi kwamba Magufuli atapewa nafasi bila kupingwa ndani ya chama ili aweze kumalizia muhula wake wa hali ngumu kwa watanzania wote, gharama kubwa za maisha, hakuna ongezeko la mishahara, kuwacha watu wajifie na covid19 na kuua democray pia uvunjifu wa haki za binadamu

Kitendawili kipo vyama vya upinzani, wao wanapambana vilivyo kuhakikisha wanaiangusha serikali ya ccm
Je upinzani wamejipanga vipi katika kusimamisha mgombea wa urais?
Je umoja wao kama ukawa upo awamu hii

Kwa upande wa CHADEMA teyari watu werevu tumekwishaanza kuona uoelekeo wa nani atasimama kuwania nafasi ya urais hapa nchini

kwa sasa CHADEMA kimejipanga na Freeman Mbowe ndiye atakayepeperusha bendera ya chama

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa kiongozi huyu kuwania kiti cha urais hapa nchini, itakumbukwa pia 2005 aliwahi kufanya hivyo kupitia chadema na akashindwa vibaya

Kwa sasa Mbowe amejifanya kuchukua hatua mbalimbali kuonesha uwezo wake kwa watanzania, ikiwemo kuhakikisha anapangua hoja zote zinazotolewa na rais Magufuli
Je Mbowe ataweza kumtikisa Magufuli?
Nafasi ya mgombea kupitia chadema ngazi ya urais haijaangaliwa ndio wataamua bora liende tu wamekata tamaa?

Yetu macho watanzania kuelekea uchaguzi wa 2020
 
Mbowe akigombea Urais magufuli awezi kupata hata 30% ya kura zote hapo labda ategemee Mbereko kutoka kwa Jecha.
 
October 2020 hakuna haja ya uchaguzi, hela ziwekwe kwa ajili ya kupambana na athari za kiuchumi zilozoletwa na corona.
 
Kupambana na Rais huyu kwenye urais kama mazingira ya ushindani ni sahihi, huhitaji kutumia akili na nguvu nyingi sana. Na wala huhitaji kuwa maarufu au mwenye uwezo wa kuongoza kama wa Mbowe.

Magu ni mwepesi mno kwenye uchaguzi halali. Sema tu Time ndiyo huamua nani awe raia nchi hii. Lkn isingekuwa hivyo, hata Joti angesimama naye na kumshinda mchana kweupe.

Magu ni mwepesi mno kwenye uchaguzi wa kweli. Sema
 
Kwa sasa Mbowe amejifanya kuchukua hatua mbalimbali kuonesha uwezo wake kwa watanzania, ikiwemo kuhakikisha anapangua hoja zote zinazotolewa na rais Magufuli
Je Mbowe ataweza kumtikisa Magufuli?
Nafasi ya mgombea kupitia chadema ngazi ya urais haijaangaliwa ndio wataamua bora liende tu wamekata tamaa?
Sheria ya uchaguzi Tanzania inataka mgombea urais,walau awe na degree moja,vipi sultani Mbowe ali reseat mitihani yake ya form six?
 
Habari wanaJF
Je Mbowe ataweza kumtikisa Magufuli?
Nafasi ya mgombea kupitia chadema ngazi ya urais haijaangaliwa ndio wataamua bora liende tu wamekata tamaa?

Yetu macho watanzania kuelekea uchaguzi wa 2020
Mkuu Chief Yono, Duh...!, Mhe. Mbowe akiamua kugombea urais, kwanza itakuwa kubwa na kali ya mwaka kwasababu ndani ya Chadema yote, mtu pekee anayeweza kusimama na Magufuli na Magufuli aka feel at least some heat ni Tundu Lissu pekee
Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli! - JamiiForums

Lakini mpaka sasa bado hakuna dalili zozote za Tundu Lissu kurejea
Kwa mliomsikia Tundu Lissu kwenye Hard Talk, unadhani atarejea nchini? Mimi sina hakika na akirejea, atakuwa ni shujaa kuliko hata Nelson Mandela! - JamiiForums

Yeye Tundu Lissu aliposema yuko tayari kurejea nyumbani ila ahakikishiwe usalama wake, nimemkaribisha
Kamanda Lissu, Usisubiri Jibu la IGP Kuhusu Usalama Wako, Aliyekulinda na Shambulio Lile Yupo, Yeye Aweza, na Ataendelea Kukulinda, Welcome Back Home! - JamiiForums

Ila kama Mhe. Mbowe atagombea kufuatia kuukubali ukweli huu
Swali la Ukweli Mchungu: Je, 2020 Magufuli ana mpinzani au mshindani, au Ni Magufuli tu?!. - JamiiForums

Na pia kuukubali ukweli huu
Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible & mature enough opposition?!. - JamiiForums

Na baada ya kuvunjwa kwa Bunge hizi trends nilizoeleza hapa Mhe. Mbowe amezikubali
Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja? - JamiiForums

Then uamuzi wa Mhe. Mbowe kugombea urais 2020 kwa tiketi ya Chadema, ni uamuzi wa busara sana, ili kulinda hadhi na heshima yake kwa kuutumia ugombea huo kama a honorable exist door from active politics za ndani ya Bunge.

P
 
Back
Top Bottom