JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
“Chama chetu ni cha kidigitali yeyote anaweza kujiunga au kutoka lakini chama cha siasa ni chombo cha watu na sio klabu.
“Hakuna urafiki wa kudumu au uadui wa kudumu, kwa mtu aliyekuwa kiongozi mwandamizi kwenye chama kama Dkt. Slaa ujio wake hauwezi kuwa kama mwanachama mwingine wa kawaida.
“Sisi hajatufikia, yeye alikuwa Karatu, akazungumza na Wananchi wake, ametoa kauli kauli wakati mwingine dhidi yetu na wakati mwingine kutuunga mkono, hayo ni maisha na lazima yaendelee.
“Tunawakaribisha wote CHADEMA, hatuna geti la kuzuia Wanachama wapya lakini tunatamani walioondoka kwenye chama kwa kashfa, kukidhalilisha chama wanapotaka kurejea watafute uungwana wa kuzungumza na viongozi wenzao kipi kilienda tofauti.