Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amesema iwapo atafanikiwa kushinda uongozi wa juu wa chama hicho, atapeleka mapendekezo kwenye mkutano mkuu ili uchaguzi wa ndani uwe unafanyika kila baada ya miaka mitatu badala ya mitano.
Mbowe, anayetetea nafasi hiyo aliyoiongoza kwa miaka 21, amesema hatua hiyo itakifanya chama hicho kujiandaa kwa uchaguzi wa serikali za mitaa na miaka miwili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu ili kuepuka kinachotokea sasa.
Soma: Mbowe: Uchaguzi kila baada ya miaka mitano ndiyo uomo wa madaraka
Mbowe amesema hayo na mengine mengi katika mahojiano yake na wahariri na waandishi wa habari wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) leo Ijumaa, Januari 17, 2025, kuelekea uchaguzi wa Chadema utakaofanyika Januari 21, 2025 jijini Dar es Salaam.
"Ikiwa uongozi wa sasa utaingia mwaka 2025, ina maana Januari 2028 mpaka Desemba tuanze mwaka wa uchaguzi ndani ya chama ili 2029 tuwe na uongozi mpya ndani ya chama.
“Uongozi uwe na mwaka mmoja kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa na miaka miwili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu ili kuondoka katika hili ambalo limetokea," amesema Mbowe.
Katika uchaguzi huo, Mbowe anashindana na wagombea wenzake watatu, Charles Odero na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho bara, Tundu Lissu. Hali hiyo imeibua minyukano ndani na nje ya chama.