Mbowe: Kwanini atashikiliwa kwa Muda Mrefu

Mbowe: Kwanini atashikiliwa kwa Muda Mrefu

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Kwa mujibu wa katiba yetu ambayo ina halalisha uwepo wa muhimili uliojichimbia zaidi, mahakama ni sehemu ya chombo cha dola.

Ni kwa sababu hiyo japo mahakamani kulipaswa kuwa ni sehemu huru na kimbilio ambako haki ingetegemewa kupatikana si nadra kwa polisi au mamlaka kutishia kuwapeleka watu mahakamani.

Kivyetu vyetu polisi na mahakama Wana ukaribu usio na afya. Si ajabu kukuta DPP alikuwa polisi. Mahakama na polisi ni ndugu moja. Wawili hao kivyetu vyetu wanaweza kukubaliana chini ya meza.

Kivyetu vyetu si ajabu kukuta mamlaka zikitumia mahakama kuwanyima haki watuhumiwa.

Kama ilivyo kwa misahafu pasipokuwa na mashinikizo ya kutosha kutokea upande wa watuhumiwa mahakama zinaweza kutumika kuhalalisha mahitimisho.

Kutegemea tu nia njema binafsi ya hakimu au jaji asiyelipa kodi wala kuwajibishwa katika uamuzi wake, ni kulalia mlango wazi kwa bahati ya mwingine.

Hatima ya Mbowe haiko mikononi mwa mahakama bali i mikononi mwetu.

Mwendelezo wa makongamano zaidi ya kudai katiba kutamuweka Mbowe huru.

Kwani kesi ikiahirishwa repeatedly na hata indefinitely zipo options gani?

Polisi, mahakama na mwita chokochoko wote ni ndugu moja.

Tunachosubiria labda kama ni dodo kwenye mnazi.
 
Ni uhuni tu na udikteta wa huyo wa KUDEMKA na amiri jeshi mkuu gaidi Mwigulu Nchemba na kundi lake la Axis of Evil Ndugai, mrundi, majaliwa, msigwa, diwani na Ndugulile...

Hawa ni wa kukomaa nao kivyetu vyetu.

Lazima tuelezane ukweli:

"Haitakuwa rahisi. Tujue wengine tutakamatwa, wengine tutafungwa, na hata wengine tutakufa."

Haipo njia rahisi. Haipo njia nyingine.

Afrika kusini iliwachukua miaka zaidi ya 80 kufika kuliko matunda.
 
Ngoja atimbe kwenye ndoo kwanza kwa muda ndo ajue madhara ya kutaka kuleta vurugu kwenye nchi kwa lengo la kutimiza personal interests zake. Hakuna aliyemlazimisha.

Kutimba Mbowe kwenye ndoo?

Hilo mbona dogo sana.

Achana na Mbowe sisi tuko tayari kutimba shimoni ndani ya choo na hata kufa sembuse kutimba kwenye ndoo?
 
5678901.jpg
 
Haki huwa ina nguvu ya ajabu sana, unaweza kujidai kiburi kwa mamlaka uliyonayo ukamnyima mtu haki yake lakini ukashangaa usiku ukilala usingizi hauji, utahangaika sana kwa waganga kutafuta dawa ya usingizi, kumbe usingizi utakuja kuupata tena siku ile utakayompa haki yake yule anayestahili, haki huleta amani ya moyo na afya njema huanzia hapo.
 
Kuna mtu aliwahi kuziita baadhi ya nchi za Afrika "shit-hole countries". Ni zile zenye raslimali nyingi, zina katiba, zina bunge na mahakama lkn zinaendeshwa kama vile mradi wa mtu fulani.

Watu wake ni maskini, hawana raha lkn viongozi wamenona wanaishi wapendavyo! Halafu Trump akiwatukana wanasema ni mwendawazimu!

Utawajua kwa midomo yao.

 
Kuna mtu aliwahi kuziita baadhi ya nchi za Afrika "shit-hole countries". Ni zile zenye raslimali nyingi, zina katiba, zina bunge na mahakama lkn zinaendeshwa kama vile mradi wa mtu fulani. Watu wake ni maskini, hawana raha lkn viongozi wamenona wanaishi wapendavyo! Halafu Trump akiwatukana wanasema ni mwendawazimu!
Utawajua kwa midomo yao

Katiba mpya ina maana kuhakikishwa kwa usawa, haki, uhuru na demokrasia zaidi kwa watu. Nani kwa dhati yake anaweza kupinga hayo kama si:

1. Mjinga, mburula asiyekuwa na mbele wala nyuma
2. Mnufaika wa hali iliyopo akiwa kama mtawala au mwajiriwa wa kuulinda utawala uliopo au ndugu wa hao.

Wanufaika wa Katiba Iliyopo hawahitaji elimu

Kwamba kuna mtu leo haihitaji haki, uhuru, usawa wala demokrasia? Thubutu!

Tunapoteza muda.

Elimu inayo hitajika kwa sasa ni kwetu sisi zaidi.

Lazima tuelezane ukweli:

"Haitakuwa rahisi. Tujue wengine tutakamatwa, wengine tutafungwa, na hata wengine tutakufa."

Habari ndiyo hiyo.
 
Back
Top Bottom