Mbowe, Lissu, Heche, Lema, Mnyika na Sugu wanazeeka, sioni Chipukizi mwenye Hekaheka na uwezo mwenye miaka 25-40. CHADEMA wanampango upi?

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Hamjambo.

Nimeona viongozi wa Chadema. Asilimia tisini wapo juu ya miaka 50+ huko.

Kwa umri huo sio umri tena wa kufanya harakati zile za hekaheka. Harakati zinazohitaji nguvu kubwa ya Mwili, akili na kuongea. Viongozi hao kimsingi wamejitahidi katika maisha Yao yote ya ujana kupigania kile walichokiamini.

Lakini wakati ni ukuta. Nimewaona mara kadhaa. Ingawaje bado wana ile shauku na ari lakini baolojia inakataa. Nyuso zao na miilo yao sasa inahitaji kufanya kazi zile za mezani. Na vijana kuingia katika nafasi.

Vijana kama Malisa, Martin Maranja, John Pambalu na kina Hilda ndio wakati wao huu kupokea kijiti kusukuma gurudumu. Swali linakuja wanao uwezo wa kutosha kupambana na Dude kubwa liitwalo CCM, dude lenye mizizi mirefu, joka lenye vichwa vingi, katili lisillo na huruma?

Au wanasubiri wakati CCM ikifa kifo cha asili?

Haya mjadala upo mezani​
 
Mbowe amekuwepo kwenye uongozi mpaka wamemchoka, Mnyika na Heche ndio wamepokea vijiti kwanini unakimbilia kusema wamezeeka wakati umri walio nao ni sahihi.
Kwanini usiwape ushauri ccm ya kna Wassira na Dr Migiro.
 
Ili kuwa fair kwa chadema mkuu, kwa chama kinachosakamwa usiku na mchana huo muda wa kugroom vijana wanaupata wapi?

Vijana wenyewe hawa wa kitanzania kama vile wewe ulivyojitangaza unaogopa NRNE mwaka jana?
 
CCM wao wanatumia Dola kama ni ushauri nitawapa ule wa kuwa na uadilifu.

CHADEMA haina Dola, Mfumo wao katika kutafuta Dola unategemea zaidi mbinu ya kufanya harakati.
Harakati zinafanywa na vijana. Msingi wa hoja Yangu upo hapo.

Unaweza kunitajia walau kikosi cha Kwanza hatari cha vijana wa chadema wenye miaka 25-40?
 
Ili kuwa fair kwa chadema mkuu, kwa chama kinachosakamwa usiku na mchana huo muda wa kugroom vijana wanaupata wapi?

Vijana wenyewe hawa wa kitanzania kama vile wewe ulivyojitangaza unaogopa NRNE mwaka jana?

Yeah upo sahihi kabisa.
Chadema imeandamwa kwa kiwango cha juu kabisa mpka kufikia baadhi ya makada wake kutekwa na kuuawa.
Pia misukosuko hiyo huenda imefanya wakose muda wa kuanda kikosi kingine cha pili kama Successors wa kikosi cha Kwanza na waasisi
 
Kwa siasa zile za Hilda na Mwaipaya ni ngumu sana kutoboa
 
Unataka watajwe ili wakatekwe? Ngoja wafanye kazi zao kimyakimya

Wanaharakati hawawagi siri mkuu.

Mbowe alipokuwa kiongozi moja ya vitu ambavyo alifanya atakavyosifiwa ni kusajili vijana na kikosi kazi. Kuwapa vijana wenye vipaji vikubwa vya kuzungumza. Yeye alichoongeza ni platform na mifumo.
Unaposikia nusu ya wapinzani wa Leo kuanzia Lisu, zitto na wengineo wengi. Wamepita kwa Mbowe.

Mbowe hata kama anamadhaifu yake lakini hapa aliweza. Hata uwepo WA chadema hivi Leo ni vijana aliowaandaa Mbowe.

Swali linakuja palepale ambalo lipo kwenye mada. Ni mkakati upi, uongozi wa chadema unao kuandaa vijana ngozi ngumu katika medani za siasa za nchi?

Unaona ingizo lolote jipya?
 
Hamjambo.

Nimeona viongozi wa Chadema. Asilimia tisini wapo juu ya miaka 50+ huko.

Kwa umri huo sio umri tena wa kufanya harakati zile za hekaheka. Harakati zinazohitaji nguvu kubwa ya Mwili, akili na kuongea. Viongozi hao kimsingi wamejitahidi katika maisha Yao yote ya ujana kupigania kile walichokiamini.

Lakini wakati ni ukuta. Nimewaona mara kadhaa. Ingawaje bado wana ile shauku na ari lakini baolojia inakataa. Nyuso zao na miilo yao sasa inahitaji kufanya kazi zile za mezani. Na vijana kuingia katika nafasi.

Vijana kama Malisa, Martin Maranja, John Pambalu na kina Hilda ndio wakati wao huu kupokea kijiti kusukuma gurudumu. Swali linakuja wanao uwezo wa kutosha kupambana na Dude kubwa liitwalo CCM, dude lenye mizizi mirefu, joka lenye vichwa vingi, katili lisillo na huruma?

Au wanasubiri wakati CCM ikifa kifo cha asili?

Haya mjadala upo mezani​
Gentleman,
taasisi isiyo na maono na iliyojaa waropokaji na watu wa kuhitaji kusaidiwa maisha kila uchwao, haiwezi kamwe kua na maandalizi ya aina hiyo.

na kwa ubinafsi walionao hao wangwana, sidhani kama wanahitaji kua na mpango wa kumuandaa yeyote yule kushika hatamu za uongozi ndani ya taasisi hiyo isiyoaminika na iliyopeteza kabisa uelekeo wa kisiasa nchini.
 
Hofu imetanda,

Wasiwasi wa kutekwa na kupotezwa upo juu,hata kama Una ujasiri kiasi gani lazima urudi nyuma.

Deusdedith Soka Yuko wapi?

Mdude Nyagali Yuko wapi?

Hata wale waliopo wengi wapo nchi za nje.

Kilichobaki ni vijana kujipendekeza ,na kuwa machawa.

Naona vijana wametembea na msemo usemao.

Adui akikushinda nguvu,ungana naye.
 
Uliwahi kuwa kwenye shinikizo la Dola unapodai haki yako?
 
Hofu imetanda,

Wasiwasi wa kutekwa na kupotezwa upo juu,hata kama Una ujasiri kiasi gani lazima urudi nyuma.

Deusdedith Soka Yuko wapi?

Mdude Nyagali Yuko wapi?

Hata wale waliopo wengi wapo nchi za nje.

Kilichobaki ni vijana kujipendekeza ,na kuwa machawa.

Naona vijana wametembea na msemo usemao.

Adui akikushinda nguvu,ungana naye.

Ooh! Hatari Sana
 
Uko sahihi kabisa.

Mfumo wanaoutumia hasa wa matusi na uzushi unawaweka Kona mbaya kimaadili

Wanategemea zaidi chuki kuliko maarifa na hoja.
Tofauti na kaka na dada zao wakubwa kina Lisu na Heche
hasa hilo la matusi na uzushi hata ushauri hawapokei, inawezekana nguvu hii ya mitandao ndo inawapelekea hivyo. ika on the long run sio mpango mzuri watu hawawezi wakawa wanataka kuibadili ccm , alafu watu wakupokea kijiti wakawa hawajajiweka kwenye mazingira ya kupokea kijiti
 
Hofu imetanda,

Wasiwasi wa kutekwa na kupotezwa upo juu,hata kama Una ujasiri kiasi gani lazima urudi nyuma.

Deusdedith Soka Yuko wapi?

Mdude Nyagali Yuko wapi?

Hata wale waliopo wengi wapo nchi za nje.

Kilichobaki ni vijana kujipendekeza ,na kuwa machawa.

Naona vijana wametembea na msemo usemao.

Adui akikushinda nguvu,ungana naye.

Unajaribu kuelezea njia inayotumiwa na CCM kuidhibiti Chadema inatija na kuzaa matunda kwa CCM si ndio?

Kwamba waendelee nayo kwa sababu inawanufaisha.

Lakini upi mpango wa Chadema kujinasua dhidi ya mbinu chafu inayofanywa na ndugu zao?
 
hasa hilo la matusi na uzushi hata ushauri hawapokei, inawezekana nguvu hii ya mitandao ndo inawapelekea hivyo. ika on the long run sio mpango mzuri watu hawawezi wakawa wanataka kuibadili ccm , alafu watu wakupokea kijiti wakawa hawajajiweka kwenye mazingira ya kupokea kijiti

Upo sahihi Mkuu.

Sijui kwa nini Chadema hawalioni hili. Ingawaje kisaikolojia unaweza kuwatetea kwamba wamepitia mambo mengi magumu, mabaya yenye kuumiza
 
Nimeona viongozi wa Chadema. Asilimia tisini wapo juu ya miaka 50+ huko.
Asilimia 90? Upo serious kweli? Kwanza wape credit kwa kureplace "wazee" na kuweka vijana kwenye kurugenzi zote na secretariat nzima.

Pia Lissu ni right age same to Heche maana wana uzoefu mkubwa, katibu mkuu Mnyika hata 50 hajafika bado same to naibu wake wa zanzibar so basically ni vijana.

Na ukisema hakuna vijana unapotosha wapo wengi tu chipukizi kuanzia Sam welwel, Twaha mwaipaya, Pambalu, Edward Heche, Freddie Justin, Brenda rupia, Deo Mahinyila, Ibrahim juma, Pamela Massay n.k

Na hao niliotaja wana senior positions kitaifa. So vijana ni wengi sana na hao ndio waliomchagua Lissu so fanya research yako vizuri.
 
Back
Top Bottom