Mbowe: Mbunge na Madiwani walioapa hawakutenda jinai, ila ni wakaidi

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amesema Madiwani na Mbunge mmoja wa CHADEMA, ambao wameapa baada ya kushinda katika Uchaguzi Mkuu, Oktoba 2020 hawajatenda jinai.

Lakini amesema viongozi hao wamekaidi misimamo ya chama, hivyo chama kitatenda haki kwa kuwasikiliza kila mmoja wao kabla ya kuchukua uamuzi stahiki kwa muda muafaka.

Pia kuhusu wabunge 19 wa viti maalum amesema vikao maalumu vya chama vitakaa kusikiliza rufaa ya wabunge hao walifutwa uanachama na nyadhifa zao zote.

Mbowe ameyazungumza hayo jana katika mkutano wake na waandishi.
 
Wawasamehe hao wamama, tunahitaji ruzuku kuendesha chama
 
Cdm ilikuwepo hata kabla ya kuwa na diwani hata mmoja,hatuna haja ya kuwalea virus wa ccm ndani ya cdm
Hampendi kupeleka virusi ccm?..siasa ni strategy sio emotional..
 
Hampendi kupeleka virusi ccm?..siasa ni strategy sio emotional..
Hao washaonyesha madhaifu yao tayari.
Cdm ni wazoefu sana maana tulianza na Zitto na sasa hao covid 19
 
Mngemjua adui yenu msingepata tabu ya kugombana
 
[emoji3][emoji16][emoji23][emoji1787][emoji2][emoji1][emoji28][emoji3][emoji23][emoji1787][emoji2][emoji1][emoji28][emoji3][emoji16][emoji23][emoji1787][emoji2][emoji1][emoji28]
 
Kwahiyo kuna uwezekano wa wakaendelea na hizo nafasi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…