Mbowe; Mchezaji mzuri asiyejua muda sahihi wa kuondoka jukwaani?

Mbowe; Mchezaji mzuri asiyejua muda sahihi wa kuondoka jukwaani?

Apiov

Platinum Member
Joined
Nov 13, 2023
Posts
8
Reaction score
37
UTANGULIZI
Katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi mkuu, tumeshuhudia purukushani, vuta nikuvute ya ugombezi wa nafasi mbalimbali za kisiasa katika vyama, hasa vyama vya Upinzani. Zoezi hili, liliambatana na uchaguzi wa Serikali za mitaa, Vitongoji na Vijiji, pamoja na Wajumbe, ambapo CCM iliibuka kidedea kwa zaidi ya asilimia 99, ikifuatiwa kwa mbaaaali na CHADEMA.

Ukiachilia mbali kelele za malalamiko zilizozuka wakati huo, hivi karibuni kumezuka kelele kubwa zaidi pale ambapo, Makamu mwenyekiti wa Tanzania Bara-CHADEMA, Mh. Tundu A Lissu (TAL), alipoamua kujitosa na kutangazi nia ya kugombea u-Enyekiti wa Taifa CHADEMA (CDM). Hatua hiyo inakuja wakati ambao, Mwenyekiti wa sasa wa CDM, Mh. Freeman A. Mbowe (FAM), bado yupo Madarakani, na hajatangaza nia ya kama anagombea au la, ameahidi kufanya hivyo Jumamosi hii ijayo. Lissu na Mbowe, wote ni miamba ya Siasa za Upinzani Tanzania, huku Mbowe akiwa amedumu kwenye nafasi hiyo kwa takribani miongo miwili sasa. Je, nini maoni ya Wanafalsafa, Wanazuoni, Wanasiasa, na Wapenzi na Wananchi wa Tanzania? Tumesikia mengi mpaka sasa. Sitasemea makundi yote hayo, nitajaribu tu kujikita katika Uchambuzi wa Kifalsafa, ambao unaweza kuangazia uwanda mpana zaidi hata kugusa makundi yote hayo. Hebu naomba tutafakari pamoja, uchambuzi huu ambao unatumia Fikra tunduizi (Critical Thinking):

NB: Kuanzia sasa, nitatumia maneno FAM, kumaanisha Freeman Aikael Mbowe. TAL, kumasnisha Tundu Antipas Lissu. CDM kumaanisha CHADEMA. CCM kumaanisha Chama Cha Mapinduzi.

👇👇👇👇
Je, FAM ni mchezaji mzuri asiyejua wakati sahihi wa kuondoka jukwaani, au TAL ni Mchezaji mzuri asiyejua wakati sahihi wa kuingia jukwaani? Ni nani kati ya yao anachelewa kutoka, kuingia? Kichokoo hiki kinachobeba kichwa cha habari cha uchambuzi huu wa Kifalsafa, kituongoze katika tafakari hii. Na hapa, makundi kadhaa, kama nilivyosema awali, yamejitokeza kutia neno:

Wapo watu wanaoona kwamba, FAM ni mchezaji mzuri anayechelewa kutoka, wakirejea kazi nzuri alizofanya kwa miongo kadhaa. CDM chini ya mikono yake, imeweza kuenea nchi nzima, na kutekeleza operesheni kadhaa zilizokiimarisha chama na hata kuwa tishio dhidi ya vyama vingine vya Siasa hasa CCM. Kama ilivyo kawaida ya Duniani, vitu vikubwa vinakuwa viwili viwili ili kubalansi mizania, yaani mfano Mungu na Shetani, jinsia KE na Me, Usiku na Mchana, Juu na Chini, Cocacola na Pepsi, Iphone na Samsung, Ukristo na Uislam, Simba na Yanga nk., ndivyo CCM na CDM zinavyotazamwa katika ushindani. Kundi hili linaona kuwa FAM anapaswa kupumzika kwa heshima ili afaidi kazi yake njema aliyoifanya. Lakini hapa pana shaka kidogo, unafikiri kundi hili linaona tu FAM apumzike kwa sababu hiyo tu? La hasha! Wana ajenda nyingine nyuma yake; ☹️☹️kwamba ‘Intergrity’ ya FAM, imeingia doa, ya kile kinachodaiwa kwamba amekua mshiriki wa Siasa ‘dangayifu’ za CCM ili kudhoofisha safari ya CDM kushika Dola.🤭Katika dhana hii, inapunguzwa makali na hoja kwamba FAM ni mpole na mwenye busara sana, na hivi anasikilizika au kama wasemavyo vijana wa mjini—anapigiga ‘sound’/anaongeleka. 😊

Kundi hili linarejea sakata la maridhiano yaliofeli kwa baadhi ya mambo, kutosimamisha wagombea wa kutosha wa Uchaguzi uliopita, madhila mbalimbali ya Wanachama na Viongozi wa CDM na misimamo ya kutotumia nguvu ya Umma katika kusonga mbele. 🤔🤔

Hapa ndipo Rais Samia anapoingia kwenye hili sakata la miamba hii miwili, kwani mara baada ya Mama huyu kushika Madaraka ya Rais, alifanya jitihada za kuifungua nchi na hivi akaja na R4 yaani 4R, ambazo zikawa ndio moja kati ya msingi wa maridhiano, na kusaidia kesi kadhaa za Wanachama wa CDM ikiwemo TAL kufutwa, kufutwa kwa tangazo haramu la mikutano ya hadhara, kuwapa upinzani ruzuku, kubadili sheria ya Uchaguzi na Tume, nk. Ingawa katika hayo bado baadhi ya Wana CDM hawakuyaunga mkono, akiwemo TAL aliyepinga mara kadhaa kuhusu maridhiano. Hapa FAM anaonekana kuwa mshirika mzuri wa CCM, na hivi baadhi ya watu kutomuamini. Lakini pia wengine wakahoji, kwani yalikuwa ni maridhiano ya nini? Ya nani? Dhidi ya nani na nani? Na sisi wengine tunahoji, ni kwanini maridhiano (kama yalikuwepo) yalivunjika?? 🤔🤔 majibu watakuanayo wanasiasa.

TAL, Mwanasiasa mwenye msimamo mkali wa kati, mthubutu na asiyeonea jambo soni, rekodi yake ipo wazi, akaibua sakata la rushwa kwenye Chaguzi za ndani ya CDM, akatangaza juu ya ‘Mapesa’ aliyowahi kupelekewa ili ahongwe. Alijaribu kuwataja baadhi (mmoja) hadharani kuwa ndiye aliyefanya hiyo koneksheni, na kwamba ‘mapesa’ hayo yamewavuruga kweli! Bado swali likabaki, ni nani aliyeruhusu fedha hizo kumwagwa ndani ya chama, zikisadikika kutokea upande wa pili? 🤔

Pia kundi hili hudhani kuwa uwezo binafsi wa fedha wa FAM unatumika kutokuwa na uwazi wa dhati na fedha za chama. Hivyo wanahisi kuna harufu ya ‘upigaji.’

Hoja dhidi ya TAL, zinahusu aina yake ya Siasa yenye ukali na isiyo na simile. Yaani siasa za heka heka na mtiti mtiti 😀 kwamba kama alivyosema mwenyewe wakati akihojiwa, ‘Siasa za heavy duty machine’, Siasa za nginja nginja!😂
Aina hii ya Siasa inaonekana kukosa busara na kwamba akiwa Mwenyekiti, italeta fujo?

Swali la Kifalsafa ni kwanini TAL abadili gia angani, (kama alivyofanya FAM) kipindi cha Uchaguzi wa 2015, kwa kumleta hayati Mh. Lowassa kugombea Urais CDM, kwa kuamua kugombea Uenyekiti Taifa, ilihali alishatangaza kugombea Umakamu?? 🤔🤔 ni nini kimemsukuma? Au ndio ataleta fujo na uvunjifu wa amani kama baadhi wanavyodai? Au atakua mkombozi kwa wale wanaoteseka kwa yale ambayo huwa anayapigania? 🙂🙂

Je, ni nani atakua mgombea Urais wa CDM 2025? CDM inamuandaa FAM baada ya kutokugombea au kugombea na kukosa Uenyekitu au TAL, baada ya kuhombea na kupata au kukosa Uenyekiti?
Je, CDM itabaki salama kama FAM akiamua kugombea pia? Au itasambaratika kama ilivyowahi kutokea kwa CUF imara na TLP? 🤔🤔

Haya ya pili yakitokea, je, imani kwa Wananchi juu ya vyama vya Siasa itabaki vile vile au? Vipi kuhusu CCm i ayodhaniwa kuwa nyuma ya saga hili? Je, inafurahia hali hii au inachukizwa? Au imetulia pembeni, kama Bondia machachari anayejisemea kimoyomoyo “Nyie gombaneni mnavyoweza, mkishakubaliana juu ya bondia wenu wakupambana na mimi, basi mleteni nimbonde Kichama na Ki-Uchaguzi”. 😇😇

Lakini hapa kuna mtego mkali….!
👇👇👇👇
Kama FAM ataamua kutokugombea, ina maana anakubaliana na Shutuma zote dhidi yake zilizotolewa na TAL na zinazosemwa na baadhi ya Wanachama na Wapenzi? 🤗🤗

Na kama akikataa, ina maana atakua amekubali pia kuwa anasapotiwa na mahasimu wa CDM ili wasishike Dola na kwamba anakomaa kwakua ananufaika na Upigaji?? 🤔🤔

Ni nini kitabadilika katika Siasa za Tanzania nje ya CDM? Unaonaje, ni rahisi kiasi kwa TAL kuwa Mwenyekiti wa CDM Taifa, kuliko kuwa Mgombea Rais wa Tanzania? Au ni Ngumu kiasi gani kwa TAL/FAM kuwa Mgombea Urais wa Tanzania kuliko kuwa Mwenyekiti wa Taifa?

Kama FAM atakubali kutokugombea na kukubali kubeba lawama zote hizo dhidi yake; basi kweli atakua ni Baba wa Siasa za Upinzani Tanzania. Maana atakua hajakipasua Chama na amemuhifadhi TAL chamani. Maana nionavyo mimi wote wanahitajiana kutokana na tofauti ya Character zao Kisiasa.

MAONI YA MWANDISHI
👇👇👇

Siasa ni kama Mawimbi ya bahari, sometimes yanatulia na sometimes yanatibuka. Yanapotulia, anahitajika nahodha mtulivu mpole, pale yanapotibuka, anahitajika nahodha Machachari na mdhubutu…..swali, je, mawimbi ya bahari yametibuka? Je, mawimbi ya bahari yametulia? Anahitajika nahodha wa namna gani? Katika hili CDM wanapswa kutazama asili ya hasimu wake kisisasa, kwani si vyema kutoa panga alani, ilihali hasimu wako amekuja kwa amani. 🎼Aliimba Selemani Msindi—Afande Sele na Philipo Nyandindi—O Ten mtoto wa Kola Hill Morogoro) 🎼🎤

Nawatakia kila la kheri Wanachama wa CDM wanapoelekea kwenye Uchaguzi wao wa chama hapo January 2025. Hata hivyo kwakua Vyama vya siasa ni moja kati ya wadau wa kulinda amani, nashauri pia Serikali (kama haifanyi) basi iwawekee Ulinzi wa ziada Waheshimiwa hawa wawili kwa sababu watu wenye nia mbaya wanaweza kuingilia kati kuvuruga amani kwa kuwaumiza, kama mmoja wapo TAL, alivyokwisha kusema. 😎😎

Sisi wapenda Demokrasia tunatamani kuona wakionesha dhana hiyo, kufanya siasa za Demokrasia na Maendeleo.

Wahenga walisema, Mchezaji mzuri hujua muda muafaka wa yeye kushuka jukwaani (kabla hajaboa watazamaji), je Vipi, Wahenga walisema chochote kuhusu muda sahihi wa Mchezaji Mzuri kupanda Jukwaani?? 😃😃

Tchao.!

Dr. Apiov S. Lwiwa, PhD
Ni Daktari wa Falsafa katika Falsafa
Mchambuzi na Mtafiti wa mambo ya Kijamii na Maendeleo
Barua Pepe: apiovlwiwa@gmail.com
 
Back
Top Bottom