Mbowe: Mimi Watanzania wananipenda sana, tatizo hii Mitandao inapotosha na hii ni kazi ya kakikundi kadogo ka watu wabaya

Mbowe: Mimi Watanzania wananipenda sana, tatizo hii Mitandao inapotosha na hii ni kazi ya kakikundi kadogo ka watu wabaya

Vibe lote hili bado anashupaza shingo? Akubali ukweli na uhalisia anatakiwa apishe mtu mwingine kuongoza chama
 
Freeman Mbowe amesema katika mahojiano yake na Azam TV kuwa anafanyiwa character assassination na wabaya wake kwenye Mitandao ili aonekane hakubaliki ila ukweli ni kwamba yeye anakubalika sana na bado anasifa za kuendelea kuwa kiongozi wa Upinzani.

Mbowe anasema wale wote wanaonesha tabia zisizo za Kichadema watashughulikiwa baada ya Uchaguzi.

Usiondoke Jf kwa habari motomoto

View attachment 3204258
Kwani Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, naye ni mtu wa mitandaoni tu?
 
Chadema siku zote harakati zake huwa zinakuwa pushed na mitandao ya kijamii. CCM siku zote huwa wanaiponda chadema kuwa umaarufu wake zaidi uko mitandaoni na chadema huwa inabisha kwa kusema walioko mitandaoni ndio hao hao wapiga kura.
Leo mwenyekiti anakandia mitandao kuwa inapotosha. Kweli hakuna kibaya wala kizuri inategemea unasimamia wapi kwa wakati huo.
AMECHANGANYIKIWA. Hajui kwamba wajumbe wa chadema karibu wote wapo humu mitandaoni.
 
Tundu Lisu ndio mamlaka ya nidhamu Chadema, anashindwa kutimiza wajibu wake anakuja kubwatabwata mitaani.
This logical fallacy is called non sequitur.

Sijasema namtetea Tundu Lissu, sijasema Tundu Lissu katimiza wajibu wake, sijasema Tundu Lissu hakubwabwaja.

Mimi mwenyewe nishamkosoa Tundu Lissu.

Nimekuuliza hiviii.

Kwani Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, naye ni mtu wa mitandaoni tu?

Hujajibu swali nililokuuliza, na ulichojibu kuhusu Tundu Lissu si nilichokuuliza.
 
Mimi nimeanza kumjuwa Lisu kama mwanaharakati na ameshatetea kesi za watu bure bila malipo.

Ni wa mitandaoni au siyo wa mitandaoni hilo sijui lakini Lisu ni well popular fiqure in Tanzania.
 
Mimi nimeanza kumjuwa Lisu kama mwanaharakati na ameshatetea kesi za watu bure bila malipo.

Ni wa mitandaoni au siyo wa mitandaoni hilo sijui lakini Lisu ni well popular fiqure in Tanzania.
Katika muktadha wa mazungumzo ya Mbowe, Lissu kuwa wa mitandaoni tu au si wa mitandaoni tu kuna umuhimu.

Kwa sababu kama Lissu si mtu wa mitandaoni tu, ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, ama Mbowe ni muongo anadanganya kwa makusudi, ama Mbowe ni mjinga sana haelewi kuwa Makanu Mwenyekiti wa CHADEMA anayempinga si mtu wa mitandaoni tu.

Sasa obviously Lissu si mtu wa mitandaoni tu, ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA.

Kwa hiyo, Mbowe ni muongo ama mjinga?
 
Katika muktadha wa mazungumzo ya Mbowe, Lissu kuwa wa mitandaoni tu au si wa mitandaoni tu kuna umuhimu.

Kwa sababu kama Lissu si mtu wa mitandaoni tu, ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, ama Mbowe ni muongo anadanganya kwa makusudi, ama Mbowe ni mjinga sana haelewi kuwa Makanu Mwenyekiti wa CHADEMA anayempinga si mtu wa mitandaoni tu.

Sasa obviously Lissu si mtu wa mutandaoni tu, ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA.

Kwa hiyo, Mbowe ni muongo ama mjinga?
Sijaelewa mantiki ya swali lako, hakuna kwenye interview Mbowe amemtaja Lisu kuwa wa mitandaoni.

Kauli ya Mbowe mitandao ina faida na hasara kwa jamii ikitumika vyema au vibaya.

Mfano kama kura zinapigwa mtandaoni Lisu ameshashinda huu uchaguzi, lakini ukienda field huu uchaguzi wa Lisu na Mbowe ni hitimisho tu, safu zilishapangwa tangu uchaguzi wa mikoa na kanda.

Huu ni uchaguzi wa hesabu wala hakuna influence ya mitandao kupinduwa matokeo.

Aliyeandaa network yake vizuri tangu uchaguzi wa mikoa na kanda huyo ndio mshindi.

Kwa majabari ya siasa kura za simple majority kuna wataalam wa kucheza nazo vizuri tu hakuna baunsa mbele ya njaa.
 
Back
Top Bottom