Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 16,003
- Thread starter
- #21
Kamanda jikite kwenye hoja acha kubwabwaja
Ni vema kwa sasa kila mgombea wa udiwani afanye uhakiki wa vituo katika kata yake ili kubaini vituo hewa. Ni vema kuhakiki wapiga kura kubaini walioongezwa na kuhakikisha kuwa mawakala wanatambua vituo vyao kabla ya siku ya uchaguzi. Kila mgombea ubunge hali kadhalika afanye hivyo kwa jimbo lake. Tume imehalalisha kuingiza karatasi nyingi za kupigia kura na kudai kuwa mtu anaweza kuomba karatasi nyingine kama akibadilisha uamuzi au kuharibu ya awali. Huku ni kuhalalisha kuingiza balot papers nyingi vituoni kwa nia ya wizi. Si kuna kura zinazoharibika ambazo nazo huhesabiwa? Kuna kila dalili kuwa tume inaratibu wizi wa kura badala ya kuzuia. Kwa kusema mtu hata anaweza kutumia leseni ya udereva kupigia kura hiyo nsyo ni nini kama sio kuruhusu mwanya wa wizi wa kura???