BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe anatarajia kuongoza mapokezi na mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho Godbless Lema, Machi Mosi mwaka huu, katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akiwa na viongozi kadhaa wa dini.
Lema aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini kuanzia mwaka 2010 hadi 2020, alikimbilia nchini Canada kupitia Nairobi nchini Kenya baada ya uchaguzi mkuu wa 2020 akiwa na familia yake kwa madai ya kutishiwa maisha yao.
Wengine wanaotarajia kushiriki katika mapokezi hayo ni pamoja marafiki wa Lema, Askofu Dk Benson Bagonza wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) jimbo la Karagwe na Sheikh Rajabu Katimba na Askofu wa Kanisa la Uamsho la Morovian, Emmaus Mwamakula.
Akizungumza na Mwananchi leo Februari 23 kwa simu, Lema amesema anawashukuru viongozi hao wa dini, kumuahidi kuja kumpokea anaporejea.
"Taratibu zote na kurejea nchini, zinaendelea vizuri na Mungu akipenda Machi mosi ntarejea nchini ambapo pamoja na mambo mengine tutakuwa na mikutano kadhaa barabarani na baadaye uwanja wa Relini jijini Arusha," alisema
Lema alisema anarejea nchini kuendeleza siasa na demokrasia na kuna mengi amejifunza akiwa nchini Canada ambayo anatarajia kuwa yatasaidia maendeleo ya jimbo la Arusha na Taifa kwa ujumla.
"Kuna kampuni nikifika natarajia kuizindua ambayo pamoja na mambo mengine itakuwa ikitoa ufadhili wa masomo na kubadilishana uzoefu," amesema.
MWANANCHI