"Vilevile nawapongeza TANESCO kwa upande wao na Wizara wamefanya kazi kubwa kusimamia jambo hili na kutimiza ndoto ya Watanzania kupata umeme wa uhakika. Megawati 2,115 kwa wakati mmoja so sio jambo la kitoto, ni jambo kubwa sana. Hasa inapokuwa kwamba fedha hizo zinatokana na kodi za wananchi, mapato ya ndani ya serikali, ni jambo la kupongeza."
Kigaila:
"Umeme ni maendeleo. Mradi huu unapozinduliwa leo, kuweza kuleta umeme wa kutosha katika nchi wetu, tunajua uanzishwaji wa viwanda utawezekana, tunajua ajira zitapatikana, tunajua wanaofanya kazi zinazotegemea umeme wataweza kufanya hizo biashara na wataweza kuzalisha."