Mbowe na Kigaila waipongeza Serikali kwa kutimiza ndoto ya Watanzania

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251

Your browser is not able to display this video.
Mbowe:
"Vilevile nawapongeza TANESCO kwa upande wao na Wizara wamefanya kazi kubwa kusimamia jambo hili na kutimiza ndoto ya Watanzania kupata umeme wa uhakika. Megawati 2,115 kwa wakati mmoja so sio jambo la kitoto, ni jambo kubwa sana. Hasa inapokuwa kwamba fedha hizo zinatokana na kodi za wananchi, mapato ya ndani ya serikali, ni jambo la kupongeza."

Kigaila:
"Umeme ni maendeleo. Mradi huu unapozinduliwa leo, kuweza kuleta umeme wa kutosha katika nchi wetu, tunajua uanzishwaji wa viwanda utawezekana, tunajua ajira zitapatikana, tunajua wanaofanya kazi zinazotegemea umeme wataweza kufanya hizo biashara na wataweza kuzalisha."
 
Asante uchaguzi, tulichuja mavi yakatokà na mikojo yake
 
Kupongeza pale yanapofanywa mazuri ni jambo jema, ila Sasa gharama za umeme zishuke ili watanganyika wafurahie uwekezaji mkubwa kuwahi kufanyika tz hio italeta maana
 
Mbowe amealikwa kama nani sasa hapo.!!?? Mstaafu wa CHADEMA au Mwekezaji?!!
 
Tunawatakia kila la heri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…