Bushesha jr
JF-Expert Member
- Apr 26, 2020
- 675
- 690
Yesu Mwokozi wa Wakristo enzi za harakati zake za kufundisha alifika mji aliozaliwa Bethelehemu akiwa amebebwa na Farasi ikiwa aina ya usafiri aliotumia.
Farasi yule alishangaa kwa furaha wakati akiingia katika mji ule kuona watu wamejitokeza wamejipanga barabarani na wengine wakitandika nguo zao katika njia aliyokuwa anapita naye akawa anapita akikanyaga zile nguo (ingekuwa sasa tungesema red carpet)
Farasi yule alifurahi huku akiwa na Imani kuwa hizo anatandikiwa yeye hakujua kuwa ni kwa ajili ya aliyembeba.
Baada ya ziara hiyo Siku moja, Farasi aliamua kurudi tena katika mji ule akiwa pekee yake, safari hii alishangaa sana maana hakuna watu waliojitokeza kumlaki wala hakuna mtu aliyemtandikia nguo, na mbaya zaidi alivyojaribu kujipenyeza katika mji huo alifurushwa kwa bakora za kutosha bila huruma.
Mh. Spika amenukuliwa akisema kwamba Mbowe amejitengenezea ufalme ambao haukubaliki; ambapo Mhe. Ndugai alifananisha amri na zile za jeshi "wabunge kushoto, kulia, nyuma geuka, simama inama" n.k
Nakubaliana kabisa na Mhe. Spika katika hili, Mbowe hajakugundua kuwa hali imebadilika wakati ule alipokuwa na washauri wazuri na wakati wakiwa agenda muhimu kwa Taifa alipokelewa vizuri kwa sababu ya agenda za Utaifa na washauri wazuri waliokuwa wamemzunguka sasa alilewa akifikiri ni yeye.
Leo anataka alivyokuwa anasikilizwa wakati ule iwe hivyo hivyo; anajidanganya atafurushwa kila mahali.
Chadema waache udalali wa nchi, waache udikteta ni upuuzi kuimbisha watu kila anayetofautiana na wewe eti amenunuliwa au msaliti. Kwanini wasaliti wawe wengi kiasi hicho? Kwanini usifikirie kwamba tatizo somewhere.