mkalamo
JF-Expert Member
- Sep 7, 2013
- 343
- 359
Kabla ya Uchaguzi mkuu wa 2020 baadhi ya viongozi wa Chadema akiwemo Nusrat Hanje walikamatwa na kufunguliwa kesi Mkoani Singida.
Kesi yao mara kadhaa ilikuwa ikitajwa na wakati mwingine kuahirishwa hadi pale walipokuja kuachiwa na baadae Hanje kuteuliwa katika ubunge wa viti maalum kupitia Chadema akitokea katika nafasi ya katibu mkuu wa Baraza la vijana (Bavicha).
Baada ya uamuzi huo Wafuasi na viongozi wa Chadema walimjia juu kuwa amewasaliti na kwenda kupewa ubunge,huku wakihoji namna alivyoachiwa.
Wakati mjadala huo ukiendelea Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe nae akakamatwa na kukaa ndani kwa miezi minane na baadae kuachiwa katika mazingira yanayofanana na Yale ya Hanje.
Baada ya kuachiwa Mbowe, alioga na moja kwa moja akaenda kushukuru Kwa Rais Samia Ikulu jijini Dar pamoja na kuongea masuala mengine.
Mwisho wamazungumzo Mbowe alitoka hadharani na kueleza kuwa ni wakati wa kufanya siasa za kistaarabu kwa ajili ya kuijenga nchi
Na akaahidi kushirikiana na Rais katika hilo, sawa sawa na anachofanya Hanje Bungeni.
Kwa bahati mbaya katika watu hawa wawili wanaofanya tukio linalofanana mmoja anaitwa shujaa na mwingine Msaliti, ila kwenye mizani ya kukamatwa, kuachiwa kwao na kwenda kuahidi kuitumikia serikali na utii wa viongozi wote wapo sawa.