Usipotoshe, huyo Hanje na wenzake walikwenda bungeni kwa ruhusa ya Ndugai na CCM sio kilichokuwa chama chao Chadema, wakaapishwa haraka kwenye turubai ili kutimiza malengo haramu waliyotumwa na watawala.
Kwa upande wa Mbowe, yeye ametoka magereza, akaenda kuoga kama unavyosema halafu ikulu kuongea na Samia. Hilo ndilo lilikuwa lengo lake kutaka mazungumzo hata kabla hajapelekwa gerezani, sasa iweje akatae mazungumzo kisa alipelekwa gerezani?
Kama angesusa kwenda angekuwa kiongozi asiyeeleweka, haiwezekani utake mazungumzo halafu unapopata fursa ya kukamilisha lengo lako, ususe eti kisa walikubambikia kesi ya uongo wakakupeleka gerezani, huu utakuwa mfano wa kiongozi muoga na mviziaji asiyejiamini na asiefaa kuongoza chama kikuu cha upinzani tena cha demokrasia na maendeleo.