Mbowe ni muongo, wapi kilo ya parachichi huuzwa kwa Tshs 20,000?

Mbowe ni muongo, wapi kilo ya parachichi huuzwa kwa Tshs 20,000?

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2020
Posts
1,809
Reaction score
1,692
WanaJf,
Salaam!

Amenukuliwa akisema hivi
“Kilo moja ya parachichi inakwenda kuuzwa Dola 8, karibu 20,000 hapa mnauza kilo moja Tsh 800. Maandiko Matakatifu yanasema watu wa MUNGU wanateseka kwa kukosa maarifa" -
Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa @chadematzofficial taifa.

Mbowe Freeman ninafahamu kuwa ni mfanyabiashara mzuri tu - kama avocado inalipa huko nje aje anunue parachichi zetu akauze huko apate faida.
(b). Atoe takwimu za uhakika kuhusu usafirishaji wa kilo moja kwa ndege;

(c)Gharama za kiufundi nk
Zaidi ya hapo aache kuupotosha umma.
 
Kuongea ni rahisi. Basi awatafutie wanunuzi.

Ni kweli bei inayotolewa ni ndogo lakini kuna vitu Freeman hajazingatia.

1. Ubora; watu wetu wanalima kiholela. Hawana traceability ya jinsi zao limelimwa.

2. Kuna gharama za kusafirisha hadi zifike kwenye destination yao.

3. Kuna kodi n.k.

Mfano Dubai Hass Avocado moja linauzwa shilingi 4600.

Nafahamu mwaka jana kilo iliuzwa kwa 1800 sawa na parachichi 4.

Hapo ni sawa na 450 kwa parachichi moja.

Sasa ongeza hizo cost zingine plus risk ya ambazo zitaharibika.
 
Parachichi hufanyiwa processing na kuuzwa ile end product mara chache parachichi huuzwa lenyewe kama lenyewe
 
Kuongea ni rahisi. Basi awatafutie wanunuzi.

Ni kweli bei inayotolewa ni ndogo lakini kuna vitu Freeman hajazingatia...
Huwa napenda wanaounga mkono au kupinga kwa ushahidi kamq wewe. Ni kweli na narudia ni kweli Parachichi moja supermarket liliuzwa 4600.

Kilo moja kwa maparachichi ya Njombe/Mbeya inachukua kama Parachichi 4/5 hivi. Nautafuta uongo wa Mbowe siuoni.
 
Kanda ya ziwa tu tunauziwa parachichi moja 500,Apple 1000.
 
Huwa napenda wanaounga mkono au kupinga kwa ushahidi kamq wewe. Ni kweli na narudia ni kweli Parachichi moja supermarket liliuzwa 4600. Kilo moja kwa maparachichi ya Njombe/Mbeya inachukua kama Parachichi 4/5 hivi. Nautafuta uongo wa Mbowe siuoni.
Huenda hujanielewa.

Yaani kabla hajawaza moto kuwa kule wanauza 20000 lazima wajue mambo mengi kwa mfano.

1. Kuna hatua za kufanya grading, cleaning and packaging.

2. Usafirishaji wake unahitaji refrigerated containers toka umezinunua na unazisafirisha hadi destin inayopelekea.

3. Kuna government charges mbalimbali hapa nchini na kule wanapopeleka.

4. Kuna gharama za clearing na forwarding hapa kwetu na kule zinapoenda.

5. Kuna gharama za usafirishaji toka Njombe hadi bandarini kisha bandarini kwa njia ya meli hadi zinapokwenda. Na kote huko lazima ziwekwe kwenye cold rooms.

Sasa ilitakiwa hao wananchi wapewe factors zote kwenye mnyororo huo wa thamani.

Pia awasaidie namna ya kupata soko bora na bei nzuri.

Kuzungumza tatizo bila kueleza visababishi na solutions zake ni kuendelea kufanya siasa za kuhadaana tu.
 
Palachichi eur ni buku tano...mbona tenga ishirilini ndogo sana...uliza watu wa eur..mkulima ndiye anaye umia
 
Unaijua bei parachichi moja supermarkets za US?
Yatajulia wapi majitu primitive ambayo hata kama hayana opportunities za kutoka nje na kujifunza hayataki?
Wamekalia ubishi tuu, mara Mbowe hivi Mbowe vile! Utadhani wana uwezo hata wa kushindana naye.

Vijana wengi watetea ccm na ni machawa hayana shughuli maalum na unakuta wengine hata huo mlo mmoja ni shida huku paka na mbwa wanaofugwa kwa Mbowe nyumbani kwake ni wanyama wenye uhakika na mlo wao.

Sio vizuri kulinganisha hilo, lakini wanaudhi sana hawa wajinga ambao wanapiganiwa lakini hawajitambui kabisa
 
Back
Top Bottom