Kauli imesimama, hajakatishwa tamaa angesema amekata tamaa hata mimi ningemshangaa, ningemwambia aachie uenyekiti arudi nyumbani.
Kweli Katiba Mpya ni mchakato; kuanzia kuundwa sheria yake, kuandaa rasimu, kuitisha bunge la katiba, na rasimu kupigiwa kura/kupitishwa, ila kila hatua lazima pawe na msisitizo wa kuifikia, sio kusema tu ni mchakato halafu wavivu wadhani upatikanaji wake unaweza kuchukua hata miaka mia.